Zitto ameshanunuliwa huyu, ukifuatilia kauli zake toka kipindi kile ambacho mama yake mzazi pia alihusika katika kale ka "mgogoro" Chadema na kuwa anabwabwaja hovyo utaanza kupata picha Zitto amekuwa ni mtu wa namna gani. Nafahamu kwamba ana mashabiki wake wengi tu humu ndani na mimi nilikuwa mmoja wao ila kijana wameshamharibu huyu kwa sasa. Mfano mwingine halisia ni siku ile alivyozindua kampeni zake jimboni kwake na moja kwa moja kuanza kuongelea habari ya yeye kugombea urais 2015 bila hata ya kuulizwa.
JF bana, yaani mtu akipost tu kitu hapa tunakurupuka kuchangia hata kama akisema source ni wapi. Kuna mwenye gazeti hilo la uhuru aweke scnanned copy hapa? Hiyo habari imeandikwa na aliyepost na sio kuwa ameichukua na akacopy kutoka kwenye gazeti moja kwa moja. Kabla sijaweza kufikia hatua ya kusema kuwa zitto keshanunuliwa, kwanza ningependa kuiona hiyo nakala ili nijue maudhui yote ya hiyo habari
Pili, kama Zito amenunuliwa, basi nadhani price atakayopewa ni ndogo sana, because market yake na umuhimu wake viko at the bottom right now. Chadema kwa sasa ipo beyond positiion iliyokuwepo NCCR, wakati ule. Kuna kipindi Zito angeweza kuidamage chadema, kipindi amechukua fomu ya kuomba Uenyekiti, wazee wa chadema kwa busara zao wakamsimamisha, that was a very material time
This time Chadema hawana muda wa ugomvi, wana kazi moja tu kuichukua nchi, hata Zito leo atoke Chadema na kuingia CCM hatakuwa na damage yeyote kwa sababu no body will care for that, sana sana watamtukana na kuendelea mbele, moto unawaka vibaya sana wajamani, tone moja la Zitto haliwezi kuzima huu moto.
CCM wenyewe wamenywea jinsi public ilivyorespond kuhusu suala la mjinga yule Mshumbushu, ndio maana hawaliongelei tena, kwa kuwa liliwadamage wao kuliko lilivyo idamage chadema. So pay no attention na huu ujinga wa sijui zito kafanyaje, yeye ana kibarua cha kutetea jimbo lake kule Kigoma. akishindwa, bei yake itazidi kuporomoka, so he is very carefully na anachokiongea. Bottom line siamini hii habari kama kweli imetolewa kwenye gazeti kama ilivyoandikwa!!!