Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
TIMING

TIMING

JF-Expert Member
21,844
1,250
Jamani, tuwe waangalifu... hivi mnadhani zitto aliishia hapo kwenye hiyo hotuba??? Mbona tunakurupuka sana siku hizi

Ili kukamilisha hotuba na pia kuwa na mawazo wazi we must read the whole speech

Kumbukeni hata kwenye changamoto na hasa kwenye siasa huwa tunaanza na pongezi na baadae ndio tunaweka changamoto.... Lets not be like simba na yanga jamani, politics ni kwa faida ya watanzania na si chadema, kafu au ccm

msimamo mkali haujawahi kuleta maendeleo popote pale
 
Smiles

Smiles

JF-Expert Member
1,231
1,195
Kama sitaki kuamini vile....
Lakini mmh....inawezekana eeh>?
:confused2::confused2::confused2:
 
Emma Lukosi

Emma Lukosi

Verified Member
929
195
Heshima kwako Jeykeywaukweli,

Hapana hayo maneno hakutamka Zitto sipati picha kwenye kampeni naibu katibu mkuu wa chama cha upinzani anasifu serekali iliyoko madarakani ?.Ingekuwa Mzee wa Kiraracha kasema nakwambia mitusi ingemiminika kama maji ya mto Ruvu.

Nasubiri michango ya wanajamvi wengine mimi nimeishiwa nguvu.
Hiyo habari mi mwenyewe Nimeisikia :confused2:
 
Smiles

Smiles

JF-Expert Member
1,231
1,195
Jamani, tuwe waangalifu... hivi mnadhani zitto aliishia hapo kwenye hiyo hotuba??? Mbona tunakurupuka sana siku hizi

Ili kukamilisha hotuba na pia kuwa na mawazo wazi we must read the whole speech

Kumbukeni hata kwenye changamoto na hasa kwenye siasa huwa tunaanza na pongezi na baadae ndio tunaweka changamoto.... Lets not be like simba na yanga jamani, politics ni kwa faida ya watanzania na si chadema, kafu au ccm

msimamo mkali haujawahi kuleta maendeleo popote pale
Well said
 
Pundamilia07

Pundamilia07

JF-Expert Member
1,434
1,195
Safi sana Zitto, tunataka wapinzani wenye vision na kufikiria kwa upeo mkubwa.

2015 jina lake likipita kwenye urais nadhani atakuwa amejitayarisha vema kuongoza nchi na wala sio wale wanaokurupuka.
 
Mundali

Mundali

JF-Expert Member
749
195
Hii ndio taabu ya uchakachuaji wa maneno ktk kampeni.

Ambacho uhuru wamefanya ni simple propaganda, chukua maneno fulani yachochee simple. Ukiangalia kwa undani wake Zitto amesifia utendaji wa serikali ya Mkapa. Kwa hili hata mimi namuunga mkono, yaliyofanyika kwa kiasi kikubwa tumeyaona.

Tatizo hapa si CCM kama chama wajameni, tatizo ni utendaji wa viongozi wake katika kusimamia majukumu ya serikali kwa miaka mitano iliyopita. Hapo ndio upuuzi unapoonekana. Mkapa alijenga uchumi ndio na akapunguza mfumuko wa bei. Akapaisha uchumi toka 4.2% mpaka 6.7% mwaka 2000 hadi 2005.

Msiba tulionao sasa ni JK, kashusha uchumi toka 6.7% aliyoachiwa na Mkapa. Mkapa aliacha kilo ya sukari Tshs. 600/- leo ni ngapi? Mafuta ya petrol lita ilikuwa Tshs. 580/- leo ni kiasi gani?
 
J

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
1,237
1,250
Source yenyewe "UHURU". Ngoja niendelee na threads nyingine.
 
Mfamaji

Mfamaji

JF-Expert Member
6,639
2,000
Hii ndio taabu ya uchakachuaji wa maneno ktk kampeni.

Ambacho uhuru wamefanya ni simple propaganda, chukua maneno fulani yachochee simple. Ukiangalia kwa undani wake Zitto amesifia utendaji wa serikali ya Mkapa. Kwa hili hata mimi namuunga mkono, yaliyofanyika kwa kiasi kikubwa tumeyaona.

Tatizo hapa si CCM kama chama wajameni, tatizo ni utendaji wa viongozi wake katika kusimamia majukumu ya serikali kwa miaka mitano iliyopita. Hapo ndio upuuzi unapoonekana. Mkapa alijenga uchumi ndio na akapunguza mfumuko wa bei. Akapaisha uchumi toka 4.2% mpaka 6.7% mwaka 2000 hadi 2005.

Msiba tulionao sasa ni JK, kashusha uchumi toka 6.7% aliyoachiwa na Mkapa. Mkapa aliacha kilo ya sukari Tshs. 600/- leo ni ngapi? Mafuta ya petrol lita ilikuwa Tshs. 580/- leo ni kiasi gani?


Point. Msiba ni huu wa Jk
 
Sidanganyiki10

Sidanganyiki10

Member
95
95
Mmhh!

Sijashangaa sana.Kwa waliosikiliza au kufuatilia mikutano ya Zitto huko jimboni kwake Kigoma,hususan kwenye mkutano wake wa kampeni pale Kidahwe bila shaka walishaanza kujiuliza maswali pale zitto alipoanza kijipigia vijembe vya urais mwaka 2015!Huyu jamaa inawezekana ana ajenda ya siri.

Na hii haitakuwa mara ya kwanza kwa CCM kuinfiltrate ngome za upinzaji ili kuzidhoofisha.Wafuatiliaji wengi tulishaanza kutilia shaka kupungua kwa kasi na intensity ya michango yake bungeni.Na kwa vile hajakanusha habari hivi za gazeti la uhuru bila shaka ni za kweli.

Ninachojua ni kuwa watanzania wa leo hawadanganyiki!Na akicheza na trust - ambayo kwa ukweli ndio mtaji wake mkuu kisiasa - ambayo watanzania wapenda mabadiliko ya kimaendeleo wamempa basi ataishia kama Mrema. Si ndege si mnyama!
 
TIMING

TIMING

JF-Expert Member
21,844
1,250
Safi sana zito, tunataka wapinzani wenye vision na kufikiria kwa upeo mkubwa.

2015 jina lake likipita kwenye urais nadhani atakuwa amejitayarisha vema kuongoza nchi na wala sio wale wanaokurupuka.
Pole sana mkuu... najua unaumia sana siku hizi

you cant just conclude kwamba hotuba yake hakuzungumzia mapungufu ya ccm... na kama uko makini utagundua kwamba hakuna sehemu amesifiwa jk hata kwenye hicho kipande mlichokiokota kwenye hotuba ndefu zaidi na timilifu

My takes:

  1. Zitto hakuishia kwenye hizo sifa
  2. Zitto is smart and he knew what to say when and where... huwezi kwenda kwa mtu halafu ukaanza na kuporomosha lawana, we call it constructive criticism ndivyo alivyoanza
  3. Uhuru ndiyo source ya habari, kwahiyo bias tayari iko pale... DO WE EXPECT MTANZANIA DAIMA KUANZA KUKANDYA CHADEMA?
  4. tumepoteza analytical qualities na tuko zaidi kishabiki... sijui ni intentional au non-intentional
  5. Nasubiri hotuba nzima iwe posted
 
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
48,629
2,000
CCM lSIPOTOSHE UKWELI, ALICHOKISEMA ZITTO NI HIKI HAPA
Zitto anayewania ubunge Kigoma Kaskazini, alisema hayo juzi jioni katika Uwanja wa Mashujaa, alipomnadi mgombea ubunge wa Mtwara Mjini, kwa tiketi ya chama hicho, Jetha Othuman. Akizungumzia mafanikio ya serikali ya CCM, Zitto alimmwagia sifa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, akisema amefanya mambo makubwa katika uongozi wake na kama kuna makosa ni ya kibinadamu.


Source: UHURU[/SIZE][/FONT]
 
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
7,276
1,195
Zitto amvulia kofia Kikwete

Wednesday, 15 Sept 2010



NA MWANDISHI WETU, KIGOMA

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), amekiri kwamba, serikali ya awamu ya nne chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete imeleta maendeleo Kigoma, ambayo hayajawahi kutokea tangu Uhuru upatikane.

Zitto alisema hayo juzi, alipomkaribisha Rais Kikwete, aliye ziarani mkoani humo kuzungumza na wananchi katika Shule ya Sekondari ya Nyarubanda, ambayo aliifungua katika jimbo hilo.

"Mabadiliko tunayoyaona Kigoma hayajawahi kutokea tangu Uhuru. Ulipoingia madarakani, Kigoma ilikuwa na barabara yenye urefu wa
kilomita sita, leo tuna barabara mbili za lami, na kwa bahati zote ziko jimbo la Kigoma Kaskazini," alisema Zitto.

Rais Kikwete aliyeanza ziara juzi mkoani hapa kukagua shughuli za maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005, alizindua huduma ambazo zilikuwa kero kwa wananchi kwa muda mrefu.

Alisema CCM kiliahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana Kigoma, ili kuondokana na dhana Kwamba, mkoa huo umetengwa.

Rais alitaja baadhi ya ahadi hizo ni kupatikana kwa umeme katika wilaya za Kigoma Mjini, Kasulu na Kibondo.

"Tumefanya kila liwezekanalo na sasa umeme umekuwa mwingi Kigoma Mjini na tayari makandarasi wako katika wilaya za Kasulu na Kibondo, ambapo umeme utapatikana na utakuwa wa uhakika," alisema Rais.

Rais Kikwete alisema serikali inafanya mpango wa kuunganisha mkoa wa Kigoma kwenye gridi ya taifa.

Ahadi zingine kwa mkoa huo ni barabara, ambapo Rais Kikwete alikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mwandiga -Manyovu yenye urefu wa kilomita 60, inayojengwa kwa kiwango cha lami.

"Lengo letu ni kuiunganisha kwa lami mikoa ya Kigoma na Rukwa, Tabora, Singinda na Dodoma, kazi ambayo imekwishaanza na shabaha ya serikali ni kuunganisha maeneo yote ya mipakani kwa barabara za lami," alisema.

Akizungumzia ahadi ya kuwapatia wananchi huduma ya afya, Rais alisema hospitali zote za mikoa zitajengewa uwezo wa kuwa hospitali za rufani, ili ziwahudumie wananchi. Rais alitoa mfano wa Hospitali ya Maweni mkoani Kigoma, ambayo inakarabatiwa.

Alifungua maabara yenye uwezo wa kufanya utafiti na vipimo kwa magonjwa mbalimbali.

Awali, akiwa njiani kwenda Nyarubanda, Rais alilazimika kusimama njiani kuwasalimia na kusikiliza matatizo ya wananchi, ambapo katika tarafa ya Mwandiga, alisema serikali haitanii inaposema itatatua matatizo yao.

"Tuliposema tutatatua matatizo ya Kigoma hatukuwa tunatania na tutafanya zaidi ya haya," alisema.

Katika hatua nyingine Rais Kikwete amewataka viongozi wa mkoa wa Kigoma kuchukua maamuzi magumu kuhakikisha wanazuia wananchi kuendeleza ujenzi holela katika vilima vinavyozunguka Bandari ya Kigoma.

Alisema bandari ni muhimu kwa maisha ya wananchi wa Kigoma na ukanda wa nchi za Maziwa Makuu, hivyo serikali iko imara kuhakikisha inafanya kazi kwa ufanisi na kwa maslahi ya kiuchumi ya mkoa na taifa.

Rais alipotembelea bandari hiyo mwaka 2007 alijionea athari za kupungua kwa kina cha maji kutokana na kujaa mchanga katika eneo la kuegeshea meli, kutokana na makazi ya watu yaliyojengwa milimani na kusababisha mmomonyoko wa udongo.

Alisema serikali imetoa fedha na kazi ya kuchimba kwa ajili ya kuongeza kina inaendelea, hivyo ni vyema kuzuia na kulaumiwa kuliko kuacha mazingira ya bandari yaendelee kuharibiwa.
 
N

Ndinani

JF-Expert Member
5,917
2,000
I am not surprised if Zitto spoke those words in praise of ccm because he has always been angling for a position within the Kikwete government. Fortunately, the chadema top brass discovered long time ago that he is a ccm mole within their ranks and they treat him deservedly!!
 
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
7,276
1,195
Zitto: JK ni muungwana

Wednesday, 30 June 2010
Na Peter Orwa, Dodoma




MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA), kwa mara nyingine amemmwagia sifa Rais Jakaya Kikwete, akisema ana matendo na kauli za kiungwana zinazohitajika katika demokarsia kokote duniani.

Zitto amesema uungwana huo wa Rais Kikwete umejidhihirisha zaidi kutokana serikali yake kuwezesha mageuzi makubwa ya maendeleo jimboni kwake, bila ya kujali kwamba linawakilishwa na mpinzani.

Akisoma hoja ya ya kambi ya upinzani wakati wa kujadili makadirio ya matumizi ya Wizara ya Miundombinu, Zitto alisema Rais Kikwete amekuwa msikivu juu ya shida zinazowakabili wakazi wa Kigoma. "Napenda kurejea shukurani za dhati kwa Rais kwa niaba ya wakazi wote wa Kigoma kwa kutusikiliza," alisema Zitto, ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara hiyo.

Alitoa mfano kuwa kilomita 72 za mtandao wa barabara zimejengwa na serikali ya awamu ya nne tangu iingie madarakani, asimilia 90 zikiwa ni jimboni mwake. Awali kulikuwepo kilomita nane tu. Zitto alimsifu Rais Kikwete kwamba alipotembelea huko hivi karibuni, mbali na miradi iliyozinduliwa katika ngazi ya mkoa, mingine iliyobaki ilikuwa ya Kigoma Kaskazini, jambo linaloashiria ushirikiano mkubwa bila ya ubaguzi wa kisiasa.

Wakati huo huo wakati serikali ikitangaza kuvuka lengo la ajira ya watu milioni moja kama ilivyoahidiwa na Rais Kikwete, sekta za afya na huduma za fedha zimetia fora kwa kuwa na idadi kubwa ya wanawake katika ajira.

Hayo yamo katika ufafanuzi uliotolewa na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Makongoro Mahanga, aliyeliambia Bunge jana kuwa katika ajira mpya zilizofikia 1,313,561, asilimia 81.7 inatoka katika sekta isiyo rasmi.

Kwa mujibu wa Dk. Mahanga, sekta ya afya yenye asilimia 2.89 ya ajira zote, imeajiri wanawake 25,949 na wanaume 10,827 wakati katika huduma za fedha ina asilimia 0.61, wanawake wakiwa 3,908 na wanaume 3, 879.

Majibu hayo ya Dk. Makongoro kwa swali la William Shellukindo (Bumbuli- CCM), alisema sekta binafsi imeajiri asilimia 90.2 ya idadi yote ya ajira mpya.
 
babu M

babu M

JF-Expert Member
4,451
2,000
HWGA........tick...tick...tick...tick......
 
Mr. Zero

Mr. Zero

JF-Expert Member
11,741
2,000

"Wanaosema serikali ya CCM inabagua katika kugawana keki ya taifa hao ni waongo, imefikisha maendeleo hata kwa wapinzani," alisema huku akitoa mfano wa maendeleo yaliyofanyika katika majimbo ya Karatu, Kigoma na Sumbawanga. Alisema Kigoma ni ngome ya upinzani, lakini imepiga hatua kubwa katika maendeleo, akitaja miradi mikubwa iliyotekelezwa ya barabara, maji na umeme.


Source: UHURU
SOURCE: UHURU!!!!

Alivyokusanya umati hivyo siamini kama atasema hayo maneno. Nitaamini ikija source nyingine. Since ni member na hakika atakuja kujibu kama alivyofanya kwa Augustione Moshi!!

Ila dalili ni njema, Zitto anavuta umati kuliko hata JK!!
 
TUNTEMEKE

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
4,587
1,225
Huyu jamaa amepania leo kumtumia zitto kuinadi ccm..ila kaka zitto kwa vile yuko humu ndani atatueleza ukwel wa mambo..gazet la uhuru km ulikuwa haujui ni gazeti kongwe la chama cha mapinduzi..watu makini huwa hawasomi gazeti ili bwana mdogo.
 
babu M

babu M

JF-Expert Member
4,451
2,000
Labda kwenye mkutano mmoja wa kampeni tutamsikia J kikwete akisema,JAMANI TUSIMPUUZE DR SLAA MACHANGO WAKE BUNGENI ULIKUWA NI MKUBWA HASUSANI KUWAUMBUA MAFISADI WA EPA.
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics


Threads
1,424,986

Messages
35,078,036

Members
538,184
Top Bottom