William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
Great Thinker William;
1. Zitto kutofautiana na wenzie sio tatizo, na Chadema walijua wanatofautiana kwa hilo na ndio kisa wakaamua Demokrasia ichukue mkondo wake kwa kupiga kura
2. watu wanachomlaumu Zitto ni kwenda public na kuongea issue za siri za kichama, na kama Chadema walitaka kuliongea hilo kuna Viongozi wakuu kuliko Zitto
Please elewa hapo, 3. hata kama ni wewe kiongozi ungemfanya nini mtu anayeku-bypass
Hiyo intellegence ya zitto, naitilia mashaka!!!, Intelligent:tape2: people they are smart always.:tape2:Kwa mtazamo wangu, Zitto kuongea na media kuhusu kilichotokea sioni kama ni tatizo. Tatizo ninaloliona kwa Zitto ni pale anaposema kuwa si sahihi kutoka wakati rais anahutubia eti kwa sababu rais ndiye symbol ya taifa, amiri jeshi mkuu... Anasema kuwa yeye na wapiga kura wake waliona si sahihi kutoka kwa kuwa kati ya marais wote hakuna aliyekwisha ifanyia mambo makuu kimaendeleo Kigoma kama Kikwete. Hapa naona kama kuna kuchanganya mambo kwani kilichokuwa kinagomba ni jinsi Kikwete alivyoshinda urais wake na si performance yake kwa kipindi kilichopita.
Zitto ni kijana intelligent na mwenye kusimamia kile anachoamini, lakini kwa hulka yake ni rahisi sana kutumiwa na watu wenye nia mbaya na chama chake bila yeye mwenyewe kujua kuwa anawatumikia. katika sakata hili la kususia hotuba ya Kikwete kauli za Zitto zimekuwa faraja na msaada mkubwa kwa CCM.
- Mkuu kama ninakuelewa kura ilipigwa ndani ya Chadema kufuata Demokrasia, sasa ni Demokrasia gani hiyo inayomnyima Kiongozi msaidizi wa Upinzani bungeni kutoizungumzia hiyo Demokrasia to the public? Demokrasia haifanywi kwa siri mkuu wala kuzuiwa waliohusika kutosema to the public, rekebisha hilo mkuu!
- Kilichofanyika ilikuwa ni Demokrasia au siri? Chagua moja mkuu!
William.
Kwa mtazamo wangu, Zitto kuongea na media kuhusu kilichotokea sioni kama ni tatizo. Tatizo ninaloliona kwa Zitto ni pale anaposema kuwa si sahihi kutoka wakati rais anahutubia eti kwa sababu rais ndiye symbol ya taifa, amiri jeshi mkuu... Anasema kuwa yeye na wapiga kura wake waliona si sahihi kutoka kwa kuwa kati ya marais wote hakuna aliyekwisha ifanyia mambo makuu kimaendeleo Kigoma kama Kikwete. Hapa naona kama kuna kuchanganya mambo kwani kilichokuwa kinagomba ni jinsi Kikwete alivyoshinda urais wake na si performance yake kwa kipindi kilichopita.
Zitto ni kijana intelligent na mwenye kusimamia kile anachoamini, lakini kwa hulka yake ni rahisi sana kutumiwa na watu wenye nia mbaya na chama chake bila yeye mwenyewe kujua kuwa anawatumikia. katika sakata hili la kususia hotuba ya Kikwete kauli za Zitto zimekuwa faraja na msaada mkubwa kwa CCM.
Hiyo ndiyo sera ya Chadema?
Hon Zito ameng'amua kuwa uongozi wa Chadema umewehuka na mafanikio waliyoyapata, sasa ni kukurupuka kwa kwenda mbele.
Hon, If I may give an advice;
....achana na wasanii wa kisiasa. Mungu amekujalia talanta ya uongozi na tunakujua kuwa una uchungu wa dhati kwa nchi yako. You are our potential next president.
So go for real serious politics!
CCM is one of the living examples in that domain.
mh! Sijui.
Siku zote nasema namkumbuka Zito toka Daruso, hajabadilika, sidhani kama atabadilika. Huyo ndio Zito.
Demokrasi ndani ya chama na uhuru wa kutoa maoni ni jambo la msingi sana. Kwa kufuata utaratibu chama uliojiwekea ktk kufikia maamuzi yake kama vile vikao halali vya chama na panapobidi kupiga kura ili kupata majority view pia ni jambo la msingi. Tatizo ni pale mtu mmoja [zittø) anapokubali bila ruhusa au kufuata utasatibu wa chama kuzungumzia yatokanayo na vikao vya chama ambavyo naamini vilifanyika kwa siri ili kuweza kupata msimamamo wa pamoja.
Yeye size mzungumzaji mjuu wa chama na tena ikibidi au ikimlazimu kuzungumzia resolusions za vikao vya chama anapaswa kutoa msimamo au muafaka ulikubaliwa na chama na si wa mtu mmoja mmoja kwamba eti mimi sikukubali kutoka nje ya bunge n.k n.k . Hii mimi naona usaliti mkubwa kwa chama na wenzako tena kujiweka juu ya chama na viongozi wake na hata wenzako.
Ni lazima watu waende pamoja watu wanapokubaliana by majority. Mara nyingine majority wanaweza kuwa wamekosea lakini dawa si kujitenga na kupublicise maoni yako. La muhimu ni kusonga mbele kama wamoja then kutumia fursa ya vikao vya chama kupeleka hoja zako na kama zina mshiko utasikilizwa.
Aluta continua CDM....HAKIKA WATANZANIA WA ITIKADI MBALIMBALI BILA KUJALI DINI, KABILA, CHAMA WAKO NYUMA YENU KTK KUDAI UHURU KAMILI WENYE KULETA MAGEUZI KTK NCHI TANYANIA
inauma eee?? Toka mwanzo nilishasema. Kigoma wanatoaga vifaa. Kgm hatuchagui chama bali mtu. Ndio maana kgm ina karibu vyama vyote kasoro cafu.zito ni kichwa. Very brilliant. Ni mtanzania. Ni mzalendo. Hekima na busara na utaifa kwanza. Sio kususa tu. Yatawatokea puani wale wanaoshabiokia bila kufikiri. Sasa habari hii inawauma. Wanajuta aliyeileta jamvini. Lakini si ndio ukweli?? Kwani zito sio kiongozi wa upinzani bungeni? Kwa nini achicheme yaliyo moyoni mwake???
i fully support him 100%.
besides chadema bila dr. Mfuko wa cement 5000/= inaweeekana!
- Mkuu kama ninakuelewa kura ilipigwa ndani ya Chadema kufuata Demokrasia, sasa ni Demokrasia gani hiyo inayomnyima Kiongozi msaidizi wa Upinzani bungeni kutoizungumzia hiyo Demokrasia to the public? Demokrasia haifanywi kwa siri mkuu wala kuzuiwa waliohusika kutosema to the public, rekebisha hilo mkuu!
- Kilichofanyika ilikuwa ni Demokrasia au siri? Chagua moja mkuu!
William.
Nadhani wewe una matatizo makubwa. Hii sio habari ya kuandika, usidhani ni Kigoma tu wanachagua watu na sio Chama, kama unadhani ndivyo basi umekosea sana. Zito kama angekuwa na akili kama unavyosema angeliingia bungeni na kukaa kumsikiliza mshikaji wake JK. Kitendo cha yeye kutokufika bungeni ni unafiki wa hali ya juu na kiuongozi ni usaliti. Ingekuwa Chadema ni chama cha kijeshi, angeshapigwa risasi siku nyingi
Zito in all aspects ni mvurugaji wa chama, kuna mambo anafanya ambayo sidhani kama yanamsaidia. Lakini kiongozi makini ni yule mwenye msimamo na asiyekubali kuyumbishwa, sioni kama hilo analo Zito. Kuna kipindi alisema hatogombea tena ubunge, mara atachangua jimbo la kugombea, mara akagombea, mara niko shule. He can not be trusted. Wakati kampeni za uchaguzi zinaendelea, alitangaza kugombea uraisi 2015 very strange, bila kujua outcome ya uchaguzi huu. Zito alishaweka kichwani kuwa Dr Slaa hatoshinda, na ndio maana haoni kama kilio cha Chadema kina maana.
Hili na kupiga kura ndani ya chama sidhani kama alipashwa kulileta mitaani, anajikosha kwa watu, na anataka kugombea uraisi 2015, kweli, kwa mazingira haya haya, au anadhani bila pressure mambo yatakuwa tofauti, loh, amekosa weledi wa kutambua hii hali yote
Kwa wanaokumbuka kilichoivuruga NCCR ni kila mmoja kati ya Mbatia, Marando na Mrema, Selasini kuwa wasemaji wa Chama. Zito hakupaswa kukimbilia kwenye vyombo ya habari na kuteta kilichofanyika katika vikao vyao vya ndani. Huko ni kukosa kuheshimu mamlaka husika ndani ya chama na nadhani Chadema wanapaswa kumchukulia hatua kali. Hujamsikia mjumbe wa kamati kuu ya ccm akienda kwenye mtanzania daima na kueleza kilichotokea ndani ya kamati kuu kumuengua Sitta.
Nakubaliana na wanaosema kuwa Zito ni wa kumuangalia sana, he is cheap and he can easily be seduced. He has tried several times kupingana na mwenyekiti wake, na nadhani ana bifu na Mbowe. I think the best way watanzania watamheshimu ni kwa yeye kuondoka Chadema kwa amani kama hakubaliana na mwenyekiti wake na viongozi wenzake, kuliko kukivuruga chama. Asingojee kupewa adhabu, kwa kuwa ndicho anasubiri kifanyike, Chadema, dont waste time na huyu mtoto, wala hakuna haja ya kumchukulia hatua, kwani mtakuwa mmefanya kile anachokitaka, cha msingi ni kumsideline, kwa kuwa hawezi kutunza siri za chama, basi awekwe pembeni tu, this time is critical na sidhani kama kuna muda wa kupoteza na huyu mlimbwende Zito