Zitto anasema uhuru anaopata kwa sasa unatosha

Zitto ajue uhuru sio hisani anayopata kwa kiongozi aliye madarakani, akumbuke pia uhuru anaosema unatosha ulipiganiwa na wengine ambao bado hawajaupata.
ukifika uchaguzi atabadilika tu huyo mrundi
 
Zitto ni mmojawapo wa watu wanaochangia pakubwa kukwamisha maendeleo endelevu ya demokrasia. Amekuwa sio mwanasiasa anayetazama mbali linapokuja suala la upatikanaji wa madaraka.
 
Wachumia tumbo haitajiki digrii moja wala mbili kuwatambua..
Kama Mh.Lowassa alichafuliwa na kusafishwa..Mama Suluhu naamini ataongeza umakini na hawa wafuata upepo la sivyo tushageuzwa mnada wa watu kupigania madaraka badala ya kuleta maendeleo ya kweli..
Maana unafiki unataka kumshushia Hayati lawama utafikiri mamlaka yake ilitoka nje ya Dunia..yawezekana labda ndio maana safu inabadilishwa..mwisho wa siku kila kitu kitajulikana TU!
Mwenyezi Mungu atujalie UHAI
Naam!

Mama asikubali kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa kama kwamba akuwepo awamu iliyopita.

Afanye maamuzi kama kiongozi wa nchi kwa manufaa ya wananchi sio wanasiasa wachumia tumbo mwisho wa siku hao watamgeuka tu.
 
“Nimekua nyakati ambazo siasa ni ushawishi wa hoja. Nimejifunza siasa na kushiriki siasa wakati huo. Miaka 6 iliyopita ilikuwa migumu sana kwangu kwani siasa ilikuwa nguvu, vurugu, uporaji, mauaji nk. Ninafuraha sasa naona siasa za ushawishi zinarudi. Kwangu Mimi Uhuru huo UNATOSHA.” Zitto Kabwe.

NB:
Uhuru haupimwi kwa uchaguzi wa majimbo mawili, kwangu uhuru utapatikana siku tunapata, Tume huru ya uchaguzi uhuru wa vyombo vya habari, serikali inayoheshimu haki za binadamu, freedom of expression, Katiba Mpya.

Zitto ajue uhuru sio hisani anayopata kwa kiongozi aliye madarakani, akumbuke pia uhuru anaosema unatosha ulipiganiwa na wengine ambao bado hawajaupata.
Hta mimi kwaleo uhuru huu umenitosha. Maana tulibanwa mbavu ajabu. Unajua njaa ikikushika kikamilifu, ukapewa ugali na kisamvu kisichoungwa kitakutosha na wala hutakuwa na muda wa kuuliza wali na nyama au Pilau. Hayo tutajuana kesho lakini kwa leo inatosha.

Mama mi 5 tena.
 
Back
Top Bottom