Zitto anasema uhuru anaopata kwa sasa unatosha

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,636
2,000
“Nimekua nyakati ambazo siasa ni ushawishi wa hoja. Nimejifunza siasa na kushiriki siasa wakati huo. Miaka 6 iliyopita ilikuwa migumu sana kwangu kwani siasa ilikuwa nguvu, vurugu, uporaji, mauaji nk. Ninafuraha sasa naona siasa za ushawishi zinarudi. Kwangu Mimi Uhuru huo UNATOSHA.” Zitto Kabwe.

NB:
Uhuru haupimwi kwa uchaguzi wa majimbo mawili, kwangu uhuru utapatikana siku tunapata, Tume huru ya uchaguzi uhuru wa vyombo vya habari, serikali inayoheshimu haki za binadamu, freedom of expression, Katiba Mpya.

Zitto ajue uhuru sio hisani anayopata kwa kiongozi aliye madarakani, akumbuke pia uhuru anaosema unatosha ulipiganiwa na wengine ambao bado hawajaupata.
 

Abuu Dharr

JF-Expert Member
Dec 28, 2017
2,631
2,000
“Nimekua nyakati ambazo siasa ni ushawishi wa hoja. Nimejifunza siasa na kushiriki siasa wakati huo.Miaka 6 iliyopita ilikuwa migumu sana kwangu kwani siasa ilikuwa nguvu, vurugu, uporaji, mauaji nk. Ninafuraha sasa naona siasa za ushawishi zinarudi. Kwangu Mimi Uhuru huo UNATOSHA”. Zitto Kabwe.
Wanatupigia tu makelele kwa kutaka kula huku sisi tumelala....
 

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,083
2,000
Uhuru wa kweli ni uhuru aliotuletea Magufuli.

Wananchi wamepelekewa zahanati almost kila kijiji. So wapo huru kupata huduma ya afya.

Wananchi wamepelekewa umeme kwa sasa wapo huru kutumia umeme kufanya uzalishaji na matumizi ya nyumbani.

Wananchi wanapita kwenye barabara nzuri, wapo huru kusafiri bila kikwazo cha barabara mbovu.

Maji kila kona ya miji.

Amejenga bwawa la umeme litaloingiza umeme mwinngi kwenye gridi ya taifa hivyo wananchi watakuwa huru zaidi kutumia umeme kuzalisha mali.

Ujambazi ulikomeshwa kuanzia kwenye mitaa, mabenki mpaka kwenye biashara.

Vijana watafutaji kama machinga, mamalishe, bodaboda nk walipewa uhuru wa kufanya biashara za kujitafutia popote ilimradi awavunji sheria.

Uhuru wa kweli ni kumpa maisha bora mwananchi wa kawaida.

Huu uhuru wa Zitto na wenzake ni wa kufanya siasa za chuki huku wao wakijaza matumbo yao.
 

JAY MTAALAM

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
1,585
2,000
Wachumia tumbo haitajiki digrii moja wala mbili kuwatambua..
Kama Mh.Lowassa alichafuliwa na kusafishwa..Mama Suluhu naamini ataongeza umakini na hawa wafuata upepo la sivyo tushageuzwa mnada wa watu kupigania madaraka badala ya kuleta maendeleo ya kweli..
Maana unafiki unataka kumshushia Hayati lawama utafikiri mamlaka yake ilitoka nje ya Dunia..yawezekana labda ndio maana safu inabadilishwa..mwisho wa siku kila kitu kitajulikana TU!
Mwenyezi Mungu atujalie UHAI
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom