Zitto amshukia Lema kuhusu Posho

Zitto amshukia Lema kuhusu Posho

Status
Not open for further replies.
Si busara kumpinga mtu kisa achukui posho. Swala la posho lisitugawe.

Kwakweli lema amekosea na ni ungwana kumwambia ukweli.
 
Mkuu hao ni mabuku7 wenzako sema hujawaelewa tu sababu una akili ndogo kama wao
Mmebaki kupiga majungu ya kike bila ushahidi,zitto angekuwa anapiga kimya na nyinyi ushahidi mnao thubutu wachaga wangekesha mitandaoni kumwaga ushahidi ili aondoke kulinda shamba la mahindi(chadema)ili manyani yamalize kula mahindi .
 
Siku hizi umebadili jina?

Vya halali huli ila haramu kwako halali,

Huna usafi wowote katika ardhi ya dunia hii,

Wafanyie usanii watanzania wasiokujua, lakini tangu sasa maovu yako yote tutawapa watu wajionee wenyewe,

Mahakama bora kuliko zote duniani ni mahakama ya umma tu,

Toeni hizo facts hadharani vinginevyo mna chuki binafsi na Zitto.

Mnasita nini kama sio wanafiki na waongo wakubwa??!!!
 
Yani ukiwa na njaa unakuwa na majungu na mbinafsi?

Yani hizo tabia ni tabia za mtu mwenye njaa kweli?

Kwahiyo makamanda wanatakiwa wawe kama Ndesamburo, Mbowe and the likes wenye mawe yao ya kutosha sio?

Hii aina yako mpya ya kufikiri inafurahisha.
Hujui kuwa mbowe na slaa ndiyo waliobadilisha katiba ya chadema kinyemela ili wabaki madarakani milele jitambue hujui unalosema mkuu.
 
Hapa Arusha wenye akili zao hawataki hata kumsikia, wanatamani uchaguzi ufanyike leo waondoe hii kadhia mjini kwao, amebaki na kundi la vijana anaowanunulia viroba ili waandamane na kufanya fujo ili ionekane ni NGUVU YA UMMA ambayo bado inamuhitaji. Lema kaikuta Arusha ikiwa na Amani, aiache ikiwa na Amani. atuachie ARUSHA YETU ikiwa shwari! Fujo akazifanyie huko MOSHI, si ndio kwao?

arusha ipi unazungumzia mkuu? Kweli mfa maji haachi ........ Leo arusha wamkatae Lema, labda wadanganye walioko mbali na arusha
 
Ni msimamo mzuri wa kutenda unachohubiri.Naupongeza.Wabunge wanachukua mishahara isiyokatwa kodi.Ni mbunge gani aliyewahi kugomea mshahara usiokatwa kodi?

Ongezeko la mshahara kwa wabunge halijawahi kupingwa pamoja na kuwa ni wizi kwa wananchi Tunahubiri tunachotenda?
 
Toeni hizo facts hadharani vinginevyo mna chuki binafsi na Zitto.

Mnasita nini kama sio wanafiki na waongo wakubwa??!!!
Hapa upumbavu ndiyo unaosumbua watu kweli kila mtu anayo mapungufu yake lakini hawa wanaomsemea mabaya zito waseme zitto kafanya nini na wapi kama wakinipa mifano nitaelewa lakini kupanga kumchafua zito kijinga bila ukweli wowote ni upumbavu kamwe hawataweza kumwathiri zito kirahisi kwa uroho wao tu wa kutaka kuwa viongozi wa chadema wa milele.
 
Toeni hizo facts hadharani vinginevyo mna chuki binafsi na Zitto.

Mnasita nini kama sio wanafiki na waongo wakubwa??!!!

Unataka fact gani?

Nenda chadema makao makuu,

Ukishindwa
Muone invisible atakupa kahifadhi kwenye sever yake,

Ukishindwa na huko basi nitumie barua pepe yako nikupe full fact
 
...teh teh nayale mamilioni yaliyofichwa ujerumani ungeyakataa ningejua kweli wewe ni muungwana,kwa siri unatafuna,vinavyoonekana unavikana. Kumbuka wanaokusaidia ndo wanatoa siri ikiwa pamoja na mmoja wa wahasibu wa Mohamed enterprises jina kapuni kwa usalama wake...

Kabwela anajua kula na kipofu huku anawaada wananchi wenye uwezo mdogo wa kufikiri! Ki ukweli jamaa ni Kirusi hatari hata kubenea alimwandika sana na akatoa ushahidi wa mawasiliano yake na mafisadi!
 
Ni msimamo mzuri wa kutenda unachohubiri.Wabunge wanachukua mushahara isiyokatwa kodi.Ni mbunge gani aliyewahi kugomea mshahara usiokatwa kodi?

Ongezeko la mshahara kwa wabunge halijawahi kupingwa pamoja na kuwa ni wizi kwa wananchi Tunahubiri tunachotenda?
Mkuu umeuliza swali zuri sana,

Kuna wapuuzi wachache hapa wanatushangaa tulisema Zitto ni mnafiki,

Anatafuta huruma ya kiraia kwakuficha ufedhuri wake
 
Mmebaki kupiga majungu ya kike bila ushahidi,zitto angekuwa anapiga kimya na nyinyi ushahidi mnao thubutu wachaga wangekesha mitandaoni kumwaga ushahidi ili aondoke kulinda shamba la mahindi(chadema)ili manyani yamalize kula mahindi .
Ushahidi ulitolewa na Jason Bournie hapa jukwaani na Mods wakaondoa bandiko hilo ndani ya masaa mawili...kutokana na bandiko hilo Zitto alijibu haya kwenye huzi huu hapa >>>>https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ngu-zenye-lengo-la-kunichafua-kupitia-jf.html


Katika majibu ya Zitto ...hakuna alipodhibitisha kuwa tuhuma dhidi yake hazikuwa za kweli. maana kwa umakini wa Zitto alitakiwa ali'refute' tukio moja baada ya lingine katika bandiko lile...na hapo tungeweza kumuamini kuanzia hapo.
 
yote haya watanzania tunayaona. na pia ni uzalendo kutoka kwa mzalendo mwenye uchungu na nchi yake.

shida iko pale anapokataa posho halafu anachukua mabilioni gizani, ambayo ndiyo malipo ya hovyo kabisa kupita zote. kuna maana gani ya kukataa posho za wazi halafu gizani anapokea mabilioni ambayo ni kodi za watanzania?

Mungi ninani anayejua kwahakika kuwa Zitto anapokea hela za gizani? Mimi nashauri vijana tujikite kwenye kujadili facts, na siyo speculations! Tukianza kuwahuku watu based on mere speculations hatutakuwa tunatenda haki! Mimi kwasasa najifunga speed governor kwenye kusema ovyoo bil aushahidi!
 
Last edited by a moderator:
Ushahidi ulitolewa na Jason Bournie hapa jukwaani na Mods wakaondoa bandiko hilo ndani ya masaa mawili...kutokana na bandiko hilo Zitto alijibu haya kwenye huzi huu hapa >>>>https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ngu-zenye-lengo-la-kunichafua-kupitia-jf.html


Katika majibu ya Zitto ...akuna alipodhibitisha kuwa tuhuma dhidi yake hazikuwa za kweli. maana kwa umakini wa Zitto alitakiwa ali'refute' tukio moja baada ya lingine katika bandiko lile...na hapo tungeweza kumuamini kuanzia hapo.

Hili suala mods walishalitolea ufanunuzi,hata huyo yericko alipoombwa ushahidi hajatoa,hivi unajua sababu ya mods kuitoa ile mada ubaoni? Niyale yale majungu,ulitaka zitto ajibu majungu yasiyo na ushahidi?
 
ni msimamo mzuri wa kutenda unachohubiri.wabunge wanachukua mushahara isiyokatwa kodi.ni mbunge gani aliyewahi kugomea mshahara usiokatwa kodi?

Ongezeko la mshahara kwa wabunge halijawahi kupingwa pamoja na kuwa ni wizi kwa wananchi tunahubiri tunachotenda?
ile sumu bado unayo
 
Shida ni kwamba zitto anachukua mkwanja sirini,wenzake wao wataishije? Nia ya kuwadhoofisha wasipate hata ya vocha,Ataje miradi yake mbadala ya kipato
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom