Zitto amshukia Lema kuhusu Posho

Zitto amshukia Lema kuhusu Posho

Status
Not open for further replies.
zito aeleweki kweli ok fine anakataa posho ya bungeni kinafiq wakati hapohapo yeye na zoka wakikaa wanampatia mamilion ya fedhwaaa kupitia benki za ndani na.kwa classmate wake huko Germany. Refer thread ya jasorne bourne

Ha haa JASON BOURNE Unajifanya humjui huyu mnafiki mwenzako aliingia na ID fake eehhh!
 
Kutochukua posho haitoshi kuthibitisha Uzalendo na Uongozi wa Mtu, bado naamini suala sio posho suala hapa ni kutokueleweka kama u wa baridi au moto..
 
Lema na wenzake wanasema kuchukuwa posho siyo dhambi. Kumbe Zitto kwenye posho kaishatoka yupo kwenye misamaha

Aanzishe chama chake cha kikomunist,sisi chadema hatuamini upuuzi wa zitto.
 
"kuwa masikini si uzalendo" lema (mp) zito mnafiki tu yeye mbona hatumii vikao anatumia mitandao ya kijamii
 
Zitto wewe na Lema nyie wote ni WANAFIKI wakubwa tofauti ni kwamba wewe kiasi umefuta ujinga huyo Mangi hajagusa kabisa darasani Kama alivyo mr. Chairman wa Chama cha kaskazini,, kidumu CCM mtangoja sana.
 
Zitto kumbe hata misamaha ya magari umekataa duu!

hivi lile sakata la zitto kuvuta mshiko toka kwa wazee wa system (TISS) ili asiendelee kuibana serikali liliishia wapi humu JF?
 
Last edited by a moderator:
Kwa vita hivi naamini muda siyo mrefu tutaujua ukweli, na kwa utaratibu huu mliouanzisha wa kuacha kufanyia kazi matatizo yenu vikaoni na kukimbilia mitandaoni utafikiri ofisi zenu ziko huku tutayajua mengi. Endeleeni kutupiana mawe ili baadae tumjue nani MNAFIKI.
 


Zitto katika Facebook wall yake leo.


Kuchukua au kutochukua posho za vikao kama mbunge ni suala la misingi (principles) na sio suala la uwezo kifedha. Kuna wabunge matajiri sana lakini wakachukua posho na wengine wa kawaida kabisa hatuchukui posho.

Sio posho tu, hata msamaha wa kodi wa kuingia magari nimeukataa sababu ya misingi tu, kwamba siwezi kuwa Waziri kivuli ninayepinga misamaha ya kodi wakati huo huo nikachukua misamaha ya kodi. Ninaamini katika siasa za kutenda ninachosema. Mjadala wa posho kwangu mimi nimeufunga toka Juni 8, 2011 nilipoacha kupokea posho za vikao.

Mwaka huo pia nilikataa msamaha wa kodi ya kuingia gari. Ni msimamo tu, hapa mtu hupendi msimamo wangu isiwe uadui, wewe endelea kuchukua posho, omba ziwe nyingi zaidi na wala sitatia neno kwenye msimamo huo japo nitaudharau maana posho za vikao ni kuwaibia wananchi ambao hawana maji safi na salama, watoto wao hawana walimu sababu Serikali haiwalipi walimu vizuri, kina mama waja wazito wanakufa kutokana na huduma mbovu za afya huko vijijini nk.

Haya ndio masuala ya wananchi wetu na sio kudai kuongezewa posho.

Mimi nadhani Ndg Zitto angezichukua tu hizo Posho na kwenda kutatulia matatizo hayo kwenye Jimbo lake maana hata akiziacha bado hazielekezwi huko anakotaka yeye ziwe. Ndg Chukua posho, saidia madawati, maji, hospitali, barabara za mitaa Jimboni kwako Kigoma - kisha tuambie kabisa kuwa Posho za kipindi hiki nimefanya hivi otherwise watu wataendelea kukuona kuwa pengine unatafuta tu Sifa binafsi kwenye kivuli cha Uzalendo. NI USHAURI TU
 
Jamani tuache fitina zitto yuko sahihi kwa hili Lema na Co yake wameingia chaka kabisa.
 
Hivi ni kwa nini ccm wanamsifia sana Zitto? Kuna jambo hapa!!!!
 
Kuna mada huju JF niliyoleta kwamba Lema afungwe gavana, lakini utetezi uliokuja na kunirushia mawe wanajua wanachadema wenyewe. Ukweli unabaki mgema akisifiwa tembo hulitia maji. Ile ya kumrushia tofati Mwigamba Arusha haijaishia huko na sasa Lema anaanza kupambana na viongozi wa Chadema mitandaoni, hiyo ndiuyo niliyosema Lema hana busara, ana kiherehere, hafikirii kitu anachokifanya kabla ya kuchukua uamuzi, anashindwa kutumia vizuri ubongo wake. Afungwe GAVANA.

Huyu kiburi chote anapewa na uongozi wa juu, mwenyekiti na katibu mkuu. Niliwaleza jana kwenye post yake ingine kwamba ndani ya chadema upo huru kufanya kosa lolote madamu umtukane Zitto tu. Kosa pekee ni kuunga mkono msimamo au chochote anachofanya Zitto. Hivyo hawezi kufungwa gavana, na kwa post hizi atakuwa anasifiwa sana huko aliko!
 
supporters wa zitto ni Ccm Aiseee hata Lukuvi alisema wanamuheshimu aiseee. hamia kule sasa. Cdm waachie mwenyewe. kidumu cha Mapinduzi.
 
Lema na wenzake wanasema kuchukuwa posho siyo dhambi. Kumbe Zitto kwenye posho kaishatoka yupo kwenye misamaha

Huko nyuma niliwahi kuandika kuwa tatizo kubwa la Zitto ni kuwa he is in many instances incosistent; sawa kama anavyosema kuwa kutokuchukua posho ya shs 70,000 ya vikao vya bunge ni kutokana na principles zake na vivyo hivyo kwa kukataa misamaha ya kodi ya magari. Sasa kama principles zake zinamfanya asamehe kuchukua hizo fedha kwa sababu zinaathiri maisha ya wananchi wa kipato cha chini, je kuchukua fedha hizo hizo toka kwenye mashirika ya uma hakuathiri utoaji huduma za dawa,maji elimu etc kwa wanannchi maana the end result ya kuchukua pesa whether ni kutoka bungeni,serikalini au kwenye mashirika ya uma ni ile ile!!! If he was really principled and consistent then he would also abstain from pocketing allowances from parastatal institutions!!!
 
Huyu jamaa aache kuhadaa wananchi.

Ameacha kuchukua posho baada ya kujilimbikizia mali zikiwemo zile za "kazi maalum".

Angetaa tangu 2005 wakati anaingia bungeni kwa mara ya kwanza, kidooogo angeeleweka!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom