Zitto amshukia Lema kuhusu Posho

Zitto amshukia Lema kuhusu Posho

Status
Not open for further replies.
Siku hizi umebadili jina?

Vya halali huli ila haramu kwako halali,

Huna usafi wowote katika ardhi ya dunia hii,

Wafanyie usanii watanzania wasiokujua, lakini tangu sasa maovu yako yote tutawapa watu wajionee wenyewe,

Mahakama bora kuliko zote duniani ni mahakama ya umma tu,
 
Kuna mada huju JF niliyoleta kwamba Lema afungwe gavana, lakini utetezi uliokuja na kunirushia mawe wanajua wanachadema wenyewe. Ukweli unabaki mgema akisifiwa tembo hulitia maji. Ile ya kumrushia tofati Mwigamba Arusha haijaishia huko na sasa Lema anaanza kupambana na viongozi wa Chadema mitandaoni, hiyo ndiuyo niliyosema Lema hana busara, ana kiherehere, hafikirii kitu anachokifanya kabla ya kuchukua uamuzi, anashindwa kutumia vizuri ubongo wake. Afungwe GAVANA.
aka viroba akili ataipata wapi
 
Kwanini buku 7 fc wame dominate uzi huu ? Ningekuwa mimi ningejisikia AIBU sana kusifiwa na CCM !
 
CHADEMA wana mengi sana ya kujifunza kutoka CCM. sema kinachowafanya wasitake kujifunza ndio kitakachowafanya wasikae wachukue dola maisha yao yote!
 
Tunataka arudishe mamilioni yetu aliyoficha uswisi, so kukataa posho tu
 
lema hana lolote wivu kwa mh zitto kama umepigika sio unakuwa na wivu tafuta lakin sio kwa posho shame on u
 
huo msimamo najua hauungwi mkono kwa vitendo na wabunge wengine wa upinzani. Zittoooooooooo! Kabweeeeeeeeee!
 
Haya yote ni maneno tu. Kama kweli Zitto ana waonea huruma wananchi asingetembelea gari aina ya Range rover na VX auze na hayo awanunulie watu hata ki pick up cha kubebea wagonjwa arafu yeye a anunue Lav 4 au Suuzuki nitamwona mzalendo kweli siyo kuishia kupigana vijembe kwenye mitandao
 
Zitto umeongea Jambo la busara sana, kama LEMA ameamua kuchukua Posho achukue akiwa kimya, hizi porojo zake zisizo na tija asizilete hapa JF. Godbless J Lema umesikia?
 
...teh teh nayale mamilioni yaliyofichwa ujerumani ungeyakataa ningejua kweli wewe ni muungwana,kwa siri unatafuna,vinavyoonekana unavikana. Kumbuka wanaokusaidia ndo wanatoa siri ikiwa pamoja na mmoja wa wahasibu wa Mohamed enterprises jina kapuni kwa usalama wake...

gefu copy na kun aguero ubarikiwe
 
Uroho wa madaraka:Mtu mwenye njaa anaamimi kupitia madaraka aliyonayo anaweza kutimiza malengo(mahitaji) yake.

Kung'ang'ania madaraka:Mtu mwenye njaa ana sifa ya kung'ang'ania madaraka kwani akiacha njaa yake haitaisha.

Majungu,fitina,uongo na umbeya:Mtu mwenye njaa siku zote hutumia mbinu chafu ili kumuhujumu yule ambae anaamini kuwa ni kikwazo kwake katika kuondokana na njaa yake.

Ubinafsi:Ubinafsi siku zote ni matokeo ya njaa.

Sasa wakati tunatamani na kulilia ukombozi tunapaswa kujiuliza kama wanasiasa wetu si watu wenye sifa hizo za mtu mwenje njaa.

Chama cha siasa ni "team work",hivyo kama kuna mchezaji ana njaa na akaamua kuhujumu wenzake ushindi ni ndoto.

Yani ukiwa na njaa unakuwa na majungu na mbinafsi?

Yani hizo tabia ni tabia za mtu mwenye njaa kweli?

Kwahiyo makamanda wanatakiwa wawe kama Ndesamburo, Mbowe and the likes wenye mawe yao ya kutosha sio?

Hii aina yako mpya ya kufikiri inafurahisha.
 
Wakati mjadala huu unapamba moto nadhani mwaka 2011 au mwanzoni mwa mwaka 2012 niliwahi kusema kwamba posho zitatutagawa lakini wana JF wakanibeza kwa kusema kuwa zitanigawa mimi! Haya sasa yanaonekana wazi. Nilijua tangia mwanzo kwamba ndani ya CHADEMA Zitto ataonekana adui kwa sababu ya kukataa posho. Ilipoonekana kwamba Zitto anapata umaarufu kwa kukataa posho KUB akaja na santuri ya kulikataa shangingi la Serikali! Muda si muda tukaambiwa jamaa kalirudia analitumia lakini msiimamo wa Zitto ukabaki pale pale kwamba hataki posho hadi leo. Huu kwangu ni ushujaa badala ya usaliti. Kwa jambo hili la posho Zitto anabaki kuwa shujaa tu.

Tunaacha masuala ya msingi tunaanza kugombea posho! Zitto kasema hapokei na wengine wanapokea si waendelee kupokea tu bila kupiga mayowe.
 
viva zito kabwe the man of the people

CCM mnampenda sana Zitto! Hongereni na 2015 muhakikishe anagombea urais kwa tiketi ya ccm

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
yote haya watanzania tunayaona. na pia ni uzalendo kutoka kwa mzalendo mwenye uchungu na nchi yake.

shida iko pale anapokataa posho halafu anachukua mabilioni gizani, ambayo ndiyo malipo ya hovyo kabisa kupita zote. kuna maana gani ya kukataa posho za wazi halafu gizani anapokea mabilioni ambayo ni kodi za watanzania?
Watanzania wa wapi sema wana Arusha wa maeneo ya Sakina na Stendi ya vifodi.
 
kukataa posho sio kipimo cha uadilifu, ni vyema pia ukaviweka wazi vyanzo vyako vya mapato, ili ijulikane wazi kuwa unaishi kwa kipato kinachojulikana.
Pia hata misaada ya kusaidi jimbo lako pia ijulikane inatolewa na akina nani isje ikawa kampuni ya madini iliyoko mkoa mwingine wanachi wanaogeshwa na kunyweshwa maji ya sumu halafu misaada ipelekwe kwako huo ni uadilifu au majanga?

sidhani kama issue hapa kati ya lema na zitto ni juu ya posho kwa mtazamo wangu hii itakuwa ni uadilifu na uaminifu ndani ya chama, kama mtu ameamua kuwa popo unategemea nini.
jogoo awike asiwike kutakucha tu , this is the point of no return, with or without him.
jemedari ametusaliti katikati ya mapambano lakini hatutarudi nyuma
 
Wakati wakoloni wanafurushwa kutoka Tanganyika , hakuna Mtanganyika yeyote aliyekuwa ameshiba wala hapakuwa na mwananchi mwenye cheo !
 
Lema na wenzake wanasema kuchukuwa posho siyo dhambi. Kumbe Zitto kwenye posho kaishatoka yupo kwenye misamaha

Mkuu huyu jamaa nayeitwa Zitto yeye anapiga mambo kimya kimya. Anatenda anavyoamini na si kusema asichokiamini.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom