Turbulence
Senior Member
- Apr 24, 2012
- 153
- 30
Wabunge wengi wanapenda posho. Kama una event unamwalika mbunge kamwe hatakuja kama huna posho! Na akifika usipompa posho basi ni ugomvi. Kama watoto. Mimi nimeyaona --- mara nyingi. Lakini pamoja na hayo, ninyi Zitto na Lema, acheni up.umbavu wa kutupiana mipasho hadharani. Kuna mambo mengi ya msingi ya kitaifa ya kuyajadili na kuyashughulikia. Kwa upande wangu, janga la kwanza la matumizi mabaya ya Serikali ni manunuzi (procurement). Zaidi ya asilimia 85 ya bajeti ya Serikali inatumika kwa manunuzi. Na huko ndipo wizi unapofanyika. Bei zinakuwa inflated hadi asilimia 1,000 (elfu moja). Sasa Zitto na wenzake waliangalie pia hili. La posho ni tatizo, lakini ni jepesi ukilinganisha na hilo la procurement. Again, achene upuuz.i wenu wa kupashana hadharani.