Zitto akutana na wahariri usiku huu Dar

Zitto akutana na wahariri usiku huu Dar

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,506
Zitto Kabwe ambaye ni Kiongozi mkuu wa ACT Tanzania usiku huu amefanya mkutano na wahariri wakuu wa vyombo vya habari Tanzania.

Mkutano na wahariri umeenda sambamba na chakula cha jioni katika hoteli moja katikati ya jiji.

Zitto ametumia nafasi hiyo kuwaomba wahariri wamsaidie kuitangaza ACT Tanzania ili kiwe chama kikuu cha upinzani na kilete mapinduzi ya kweli katika siasa za Tanzania

Katika mkutano huo Zitto aakiwa amefuatana na Prof Mkumbo na Mwenyekiti wa chama, amesema ACT itawashangaza wengi kuanzia Julai mara baada ya bunge kuvunjwa kwani makumi ya wabunge wa sasa watahamia ACT toka CCM, Chadema na Cuf. Amesema ACT itasajili wabunge wenye majina kama ya Messi na Yaya Toure na wala haitasajili vidagaa kwa maana ya wabunge wasio na makali.

Akaongeza kuwa ACT inaweza kuwa na mgombea urais mwaka hui tena mgombea tishio hasaaa lakini watu wasubiri wakati utakapofika. Zitto na Mwenyekiti wake wameahidi kuanza ziara ya mikoa kumi wiki hii kukitangaza chama katika awamu ya kwanza.

Nitawapa taarifa nyingine baadae katika thread mpya ya jambo lisilo la kawaida lililojitokeza baadae katika mkutano huo na kuleta mgawanyiko mkubwa kwa wahariri kupitia Jukwaa lao la Wahariri
 
zito ni mashine ya kusaga na kukoboa Kazi hio anaiweza ya kisiasa ccm na cdm wakae mkao Wa kula na mda mrefu bunge la budget likiisha anaondoka na watu cdm Kazi kwao
 
watu walivyo wa ajabu hii hdith isiyo na evidence/source yoyote wanaimin,watanzania tuna shida sana kama humu ndo tunajiita ma great t sijui huko nje kukoje


we uliepost huu uharo wako sio timamu
 
chama hujengwa na ujenzi wake huchukuwa muda mashinani mpk matawini
 
ACT hakiwezi kuwa chama kikuu Tanzania.

Na zaidi ya Ayatollah sidhani kama kinaweza kushinda kiti kingine cha ubunge.

Nadhani wana uhakika na viti viwili mpaka sasa, cha Zitto na Arfi Mbunge wa Mpanda.
 
mkuu na mhariri wetu wa gazeti la chadema alikuwepo maana asije kutusaliti
 
Back
Top Bottom