Zitto akera wajumbe kamati kuu CHADEMA - Tanzania Daima

Zitto akera wajumbe kamati kuu CHADEMA - Tanzania Daima

Status
Not open for further replies.
The true zitto is now showing up, naanza kuamini kung usaliti kifuani wake.
 
Halafu hakuna la maana lilolojadiliwa la msingi mpaka Tanzaniadaima kuandika hii taarifa isiyo na tija yoyote? Naona linaendeleza siasa za kumchafua zitto.

Ulitaka hiyo habari iandikwe kwenye Uhuru?
Chamvigaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
WAKATI Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiendelea na kikao chake jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, amekacha.

Zitto ambaye katika siku za hivi karibuni aliibua mjadala kwenye vyombo vya habari, hasa alipoingia kwenye malumbano na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amekacha kikao hicho na badala yake ametoa taarifa ya kusafiri nje ya nchi.

Kwa mujibu wa habari hizo, taarifa iliyotolewa kwa wajumbe wa mkutano huo na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe, ilisema kuwa Zitto yuko safarini nchini Sudan, lakini anatarajia kuhudhuria mkutano huo wakati wowote.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho kinachofanyika kwenye Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam zilieleza kuwa baadhi ya wajumbe wameonyesha dhahiri kukerwa na hatua ya naibu katibu mkuu huyo kutoshiriki.

Waliolalamikia hatua hiyo walisema kuwa limekuwa jambo la kawaida kwa Zitto kutohudhuria vikao muhimu vya chama huku akijua fika kwamba yeye ndiye msaidizi mkuu wa katibu mkuu wa chama taifa.

Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho aliliambia gazeti hili kuwa moja ya ajenda zilizowasilishwa jana na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi ni kuhusu mapato na matumizi ya chama ambayo alidai ingefaa Zitto awepo kuisikiliza.

Mjumbe huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema ajenda hiyo ilikuwa muhimu kwa Zitto kuwepo kwani akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), amekuwa akidai kwamba CHADEMA na vyama vingine hawana hesabu za mapato na matumizi ya fedha za ruzuku wanazopata kila mwezi.

Mkutano huo unaendelea leo.
Pamoja na maneno yaliyopachikwa na mleta mada, MODS unganisheni thread hii na nyingine.
 
Ripoti kuipata sio mpaka uwepo kwenye kikao. Andikeni ripoti wapeni wanachama na viongozi wazione. Acheni porojo kwenye masuala ya pesa.

Hayakuhusu haya mlifikiri anaweza kupata uenyekiti ndani ya cdm mmechemsha vijana wa lumumba.
 
Ngoja niwaamshe mods waiunganishe hii thread ya kijinga yenye heading ya kipashkuna.
 
Inashangaza sana,

Hiivi,,kama wana vigezo vya maana vya kumfukuza uongoz na uanachama wanasita nini kufanya hivyo??

Mara wakimbile mitandaoni,mara wakimbilie kwenye vyombo vya habari,shida yote ya nini??
 
Mtu kukimbia kikao cha chama chake kwa sababu za kiusalama; ni hali ya kawaida?
Tatizo la usalama limeanzxa lini?Mbona huyu jamaa ni kawaida yake kutokuhudhuria vikao vya chama!
 
Mtu kukimbia kikao cha chama chake kwa sababu za kiusalama; ni hali ya kawaida?
Ya CDM yanakuhusu nini? Hebu shughulikieeni kwanza ile kesi yenu ya ubakaji wa mtoto wa miaka 14 kabla ya kuparamia mambo ya CDM.
 
Ni kuhusu Zitto kabwe, huyu kijana anakivuruga sana chama kwa mwenendo wake anao ufanya ndani ya chama, unaopelekea kukidumaza chama. Kiukweli zito ni kirusi kinacho kimaliza chama.Hivyo mimi binafsi naomba kamati kuu kuchukua maamuzi magumu dhidi ya zito

Kumchinja Kobe kunahitaji timing
 
Hawajui wanacho hitaji hao, matokeo yake wanabaki wana weweseka tu.. mara ooh! ni katibu mkuu masidizi amabe ni muhimu kwao, mara ooh! msariti, sasa tuwaeleweje?.. yaani hiki chama kinapoteza dira kwakweli

Inashangaza sana,

Hiivi,,kama wana vigezo vya maana vya kumfukuza uongoz na uanachama wanasita nini kufanya hivyo??

Mara wakimbile mitandaoni,mara wakimbilie kwenye vyombo vya habari,shida yote ya nini??
 
Inaelekea akina Mbowe wanamtega Zitto. Ndo maana wanaandaa kikao mara nyingi akiwa nje ya nchi

Habari ya India umeshatoka mahakamani? Jitahidi mumsafirishe huyo mwenzenu aliyekufa kwa sembe usimkimbie kama yule wa mbeya.
 
Wa Kaskazini wanapozidiwa ujanja na wa Kusini magharibi.

Kila hila, kila mbinu, yeye huyoooooooooo, one man army.

Kwi kwi kwi teh teh
 
yaani zitto aache kuhudhuria vikao vya maana vyenye kubeba mustakabali wa nchi. ili aje kwenye vikao vya kupigana na matofali?

vikao gani vyenye kubeba mustakbali wa nchi? Au ametumwa na Kinana?

Andrea Cordes A/c online
 
Huko sudani kusini katumwa na chama chake ama ni safari binafsi, halafu si aliendaga na jk huko wakati fulani wajameni? huyu kijana ni hatari hatari hatari, hatari kuliko shibuda.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom