Elections 2010 Zitto akabwa koo jimboni

Afanye booking ujermany mapema asije kosa ubunge akakosa na kazi za vibarua ujerumani
siasa kazi kweli kweli
 
Kuna wakati Zitto alituaminisha kwamba angeweza kugombea kokote Tanzania hii na akashinda. Akaanzisha na "utafiti" kabisa ni wapi agombee!! Tambo nyingine bwana.
 
Kama kweli Zitto kasema hivyo basi ni kioja kikubwa na kashfa ingine kwa wapenda demokrasia na ni uvunjaji wa wazi wa katiba yetu hasa provision isemayo "kila mtu ana haki ya kuchaguwa na kuchaguliwa"

By the way kama Dunia aliye mgombea wa CUF ana 'damu ya CCM' vipi kuhusu wagombea wa CHADEMA waliotoka pia CCM kama akina Thomas Nyimbo,Ngwatura,Shibuda na wengineo wengi akiwemo hata Ntagazwa aliyewahi hata kuwa Waziri ktk serikali inayoundwa na chama cha CCM?

Mbona CHADEMA wamewapokea watu kibao kutoka CCM na wamewasimamisha kugombea ubunge? hao waliowapokea wametumia scanning machine gani kujua bado hawana damu ya CCM? au kunya anye kuku?
 
CUF sio pumba Unguja, kwani katika majimbo 31 walipata jimbo 1 ambayo ni sawa na 3.33% na Chadema katika majimbo 182 ya bara walipata 5 ambayo ni sawa na 2.74%. Changanua mwenyewe
MMh! kweli safari ni ndefu
 
CCM ni CHAMA CHA MAJAMBAZI asikuambie mtu bwana, Mwaka huu CCM hawatangazi sera ila wanatangaza pingamizi kwa wagombea wengine.Dr Slaa juuuuuuuuuuuuuuu.
 
Ama kweli uongozi wa kibongo ni dil.. una corrupt hata minds of the strongest!!!!!!!! wana CHADEMA wenzetu mnaanza kuonyesha your true colour. through this forum,i one time questionned the democratic credibility of our party CHADEMA.It was during enterparty election.
kwenye nafasi ya uenyekiti ZITTO KABWE aliwekewa zengwe na watu wanaojiona wenye chama mpaka akajitoa.
AJABU.. Zitoo huyuhuyu, huyuhuyuuuu leo hataki ushindani jimboni kwake??? from ccm to chadema= uzalendo, from ccm to cuf=usaliti.
AM VERY DISAPPOINTED

]
 
Mzee Ngabu, tema mate chini ndugu yangu, kwa nini? Au ni agemate wako, maana agemates ukimzidi jua hapo kuna uadui tayari. Mimi nampenda sana huyu Bwana mdogo, anafanya kazi nzuri sana. Au wewe unataka wapinzani wazee kama akina Cheyo na Mrema?

Hakuna hata robo alichonizidi. Mimi ni private person yeye ni public figure. I am doing quite well in the career I chose to follow.
 
Hakuna mwenye hati miliki ya kuongoza isipokuwa..............zito km wengine tu wala msituletee nijadala hewa....zito mwenyewe ccm walimlegeza kidogo tu na tuvyeo na tupesa walipoamua kumshawishi ili apigie debe mitambo ya richmond,,,,,huyu zito naye haaminiki hata kidogo siamini kama ni ridhiki kwa kuwa ni mrahisi wa kushawishika na kaonesha hilo kwa matendo yake..............tunaweza kupata mpiganaji mwingine wa kweli hata kupitia ccm.....lakini tuondoe akili ya mgando kwamba kuna mtu yeye ndiyo hastaili kupingwa........changamoto ni muhimu sana kwenye maisha yetu,ngoma ni pale tunapozifanya changamoto kuwa matatizo basi hiyo mwisho wa siku inazaa uoga kama wa zitto
 
MGOMBEA ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe anakabiliwa na upinzani mkali kutoka vyama vya CCM na CUF huku yeye mwenye akijibu mapigo akisema mkakati huo wa CUF unalenga kuudhoofisha upinzani na kuipa ushindi CCM.

CUF ilitangaza mkakati wake huo juzi na kumtambulisha Omar Musa Nkwarulo maarufu kama Dunia, ambaye atamvaa Zitto katika Jimbo la Kigoma Kaskazini.

Lakini Zitto jana alisema "Nimeshangaa CUF kumpokea Dunia na kumsimamisha kugombea ubunge Kigoma Kaskazini."

"Huyu hajawahi kuwa mpinzani wa kweli, niliwapigia kabla (Profesa Ibrahim) Lipumba, (Ismail) Jussa na Maalim Seif kwamba, huyu si mpinzani wa kweli, lakini nimeshangaa wamempokea na kumsimamisha. Naamini bado ana damu ya CCM.

"Mbona sijasikia Shibuda kapelekwa somewhere kutolewa ile damu ya sisiem akawekewa ya upinzani wa kweli?' Bw mdogo aache uoga kama anaona hawezi angeachia mwingine yeye akasubiria wa kuteuliwa ataupata tu." Mnieleweshe jamani hivi huwezi kuwa mpinzani mpaka uwe mbuge?
 
CHADEMA ni chama cha ajabu saana. Mtu kama Zitto ni wazi kabisa anajilazimisha kuwepo CHADEMA lakini practically hahitajiki. Maana maneno hayo angekuwa ameongea kiongozi mwingine wa CHADEMA (japo hayajathibitishwa) angetetewa kwa nguvu zoote.
 
MGOMBEA ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe anakabiliwa na upinzani mkali kutoka vyama vya CCM na CUF huku yeye mwenye akijibu mapigo akisema mkakati huo wa CUF unalenga kuudhoofisha upinzani na kuipa ushindi CCM.

CUF ilitangaza mkakati wake huo juzi na kumtambulisha Omar Musa Nkwarulo maarufu kama Dunia, ambaye atamvaa Zitto katika Jimbo la Kigoma Kaskazini.

Lakini Zitto jana alisema "Nimeshangaa CUF kumpokea Dunia na kumsimamisha kugombea ubunge Kigoma Kaskazini."

"Huyu hajawahi kuwa mpinzani wa kweli, niliwapigia kabla (Profesa Ibrahim) Lipumba, (Ismail) Jussa na Maalim Seif kwamba, huyu si mpinzani wa kweli, lakini nimeshangaa wamempokea na kumsimamisha. Naamini bado ana damu ya CCM.

Atajifunza kuwa kun marafiki wa kweli na wa uongo. Kama alisapoti mitambo ya Dowansa kwa nini RA hakutumia connections zake za cuf kukutomsimamisha Dunia?Ndio hapo anatakiwa ajifunze kuwa kuna maamuzi ya kiserikali ambayo ukiyasapoti ni sawa na kukisapoti na chama hicho tawala....Ndo ukweli huo...Kila kheri ndg Zitto,hopefully uliwafanyia wananchi wa jimbo lako yale waliyokutuma kuyafanya.
Na pia next time kumbuka kuspoti mazuri yatakayotokana na wizi wa serikali ya ccm ni sawa na kuisapoti ccm.
 
CUF ilitangaza mkakati wake huo juzi na kumtambulisha Omar Musa Nkwarulo maarufu kama Dunia, ambaye atamvaa Zitto katika Jimbo la Kigoma Kaskazini.
Jamani mliowahi kuwapo pale Mbeya, enzi zile timu ya soka ya TAZARA ilipokuwa inavuma, naombeni mnifafanulie kama huyu jamaa ndiye yule mshambuliaji wa kati aliyekuwa anaitwa Dunia Nkwarulo, ambaye amecheza na akina Amri Said 'Stam'. Kuna kipindi pia aliichezea Ujenzi ya Rukwa, ila alikuwa anapaisha sana mipira juu ya lango kila mara hata kama goli liko wazi, hadi kocha akaamua aanze kumpanga wingi ya kulia ili hata kama atapaisha krosi, walau mpira utabaki uwanjani. Je, ndiye huyu Dunia wa CUF? Kama ndiye basi naombeni namba za pale Uhamiaji.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom