Elections 2010 Zitto akabwa koo jimboni

Kama kweli Zitto kasema hivyo basi ni kioja kikubwa na kashfa ingine kwa wapenda demokrasia na ni uvunjaji wa wazi wa katiba yetu hasa provision isemayo "kila mtu ana haki ya kuchaguwa na kuchaguliwa"

By the way kama Dunia aliye mgombea wa CUF ana 'damu ya CCM' vipi kuhusu wagombea wa CHADEMA waliotoka pia CCM kama akina Thomas Nyimbo,Ngwatura,Shibuda na wengineo wengi akiwemo hata Ntagazwa aliyewahi hata kuwa Waziri ktk serikali inayoundwa na chama cha CCM?
 
MGOMBEA ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe anakabiliwa na upinzani mkali kutoka vyama vya CCM na CUF huku yeye mwenye akijibu mapigo akisema mkakati huo wa CUF unalenga kuudhoofisha upinzani na kuipa ushindi CCM.

CUF ilitangaza mkakati wake huo juzi na kumtambulisha Omar Musa Nkwarulo maarufu kama Dunia, ambaye atamvaa Zitto katika Jimbo la Kigoma Kaskazini.

Lakini Zitto jana alisema "Nimeshangaa CUF kumpokea Dunia na kumsimamisha kugombea ubunge Kigoma Kaskazini."

"Huyu hajawahi kuwa mpinzani wa kweli, niliwapigia kabla (Profesa Ibrahim) Lipumba, (Ismail) Jussa na Maalim Seif kwamba, huyu si mpinzani wa kweli, lakini nimeshangaa wamempokea na kumsimamisha. Naamini bado ana damu ya CCM.

hapa unanipa shaka dubo, kasema kweli maneno haya?
 
kuwa kawapigia kabla viongozi wa CUF kuomba wamuondoe huyo Dunia.

kazi tunayo
 
Kama kweli Zitto kasema hivyo basi ni kioja kikubwa na kashfa ingine kwa wapenda demokrasia na ni uvunjaji wa wazi wa katiba yetu hasa provision isemayo "kila mtu ana haki ya kuchaguwa na kuchaguliwa"

By the way kama Dunia aliye mgombea wa CUF ana 'damu ya CCM' vipi kuhusu wagombea wa CHADEMA waliotoka pia CCM kama akina Thomas Nyimbo,Ngwatura,Shibuda na wengineo wengi akiwemo hata Ntagazwa aliyewahi hata kuwa Waziri ktk serikali inayoundwa na chama cha CCM?
.

Kutoka ccm na kwenda Chadema sio kwamba damu yako baado ni ccm.kuna wengine walikuwa ccm kutokana na system ilivyokuwa na hawakuwa na jinsi ya kujitoa.Lakini kuna wanaojitoa ccm kwenda kuvuruga upinzani
 
Kama anajiamini kwa nini analalamika. Ajipange kwa kampeni na kutangaza sera za chama chake
 
inategemea makubaliano yao kabla

inawezekana kabisa palikuia na makubaliano ya siri kwenye baadhi ya majimbo ndani ya upinzani... hakuna haja ya kuleta mpinzani sehemu ambapo mpinzani toka chama kimoja anaonekana ana nguvu

Hata siku moja wapinzani hawafika mbali kwa kupambana wenyewe kwa wenyewe....
 
Hayo ni majibu ya CUF kwa Chadema, baada ya Chadema kumsimamisha Slaa kwenye Uprez
 
Msimamo wa CUF ulikuwa wazi tangu walipofikia muafaka na CCM. Sijui Zitto alitegemea jibu gani toka kwa hao aliowapigia simu. Could it be out of desperation? Aende Kigoma kusini kumsaidia Kafulila kuchukua jimbo!
 
Na ashindwe na kulegea huyo zitto
Mzee Ngabu, tema mate chini ndugu yangu, kwa nini? Au ni agemate wako, maana agemates ukimzidi jua hapo kuna uadui tayari. Mimi nampenda sana huyu Bwana mdogo, anafanya kazi nzuri sana. Au wewe unataka wapinzani wazee kama akina Cheyo na Mrema?
 
MGOMBEA ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe anakabiliwa na upinzani mkali kutoka vyama vya CCM na CUF huku yeye mwenye akijibu mapigo akisema mkakati huo wa CUF unalenga kuudhoofisha upinzani na kuipa ushindi CCM.

CUF ilitangaza mkakati wake huo juzi na kumtambulisha Omar Musa Nkwarulo maarufu kama Dunia, ambaye atamvaa Zitto katika Jimbo la Kigoma Kaskazini.

Lakini Zitto jana alisema "Nimeshangaa CUF kumpokea Dunia na kumsimamisha kugombea ubunge Kigoma Kaskazini."

"Huyu hajawahi kuwa mpinzani wa kweli, niliwapigia kabla (Profesa Ibrahim) Lipumba, (Ismail) Jussa na Maalim Seif kwamba, huyu si mpinzani wa kweli, lakini nimeshangaa wamempokea na kumsimamisha. Naamini bado ana damu ya CCM.

Mimi ninachojua ni kuwa CUF ni wapinzani halisi Zanzibar, Bara wapo kwa ajili ya kuvuruga wapinzani wengine tu basi (destructive upinzani, If I am to term it)!
 
Juzi mgombea wa CCM amesema kuwa atamng'oa Zitto asubuhi tu, kwa hiyo hana budi kukaza buti kama ana nia ya kurudi bungeni. By the way nimesikia pia gari lake Zitto limepata ajali huko Kigoma, wenye taarifa za uhakika watujuze !
 
Huyu lazima arudi ujermany akasafiche vyoo vya mawaziri asubiri moto wa ccm mwaka huu
 
Kama kweli Zitto kasema hivyo basi ni kioja kikubwa na kashfa ingine kwa wapenda demokrasia na ni uvunjaji wa wazi wa katiba yetu hasa provision isemayo "kila mtu ana haki ya kuchaguwa na kuchaguliwa"

By the way kama Dunia aliye mgombea wa CUF ana 'damu ya CCM' vipi kuhusu wagombea wa CHADEMA waliotoka pia CCM kama akina Thomas Nyimbo,Ngwatura,Shibuda na wengineo wengi akiwemo hata Ntagazwa aliyewahi hata kuwa Waziri ktk serikali inayoundwa na chama cha CCM?
HAwa wana mifupa ya CCM!
 
huko kote ni kutokomaa kisiasa na hasa kidemokrasia maana kila mtu anyo haki ya kuchaguliwa.
kama aliwafanyia kazi nzuri wana kigoma kaskazini, kwa nini aanze kuweweseka mapema yote hii?
 
Ni mawazo na mtazamo wake. Ni vizuri kushindana na kushinda kwa hoja. Nadhani kama Zitto aliwakilisha jimbo lake vizuri atapita kwa kura nyingi tu. Lakini kama alijisahau basi ndo hivyo wananchi watamwadhibu. All in All tunamtakia kila la kheri.
 
Back
Top Bottom