Zitto aitaka serikali kutangaza njaa nchini

Zitto aitaka serikali kutangaza njaa nchini

Tofautisha kuwepo kwa njaa na bei ya chakula kuwa juu! it is a matter of price settled at the market. soko lina chakula, tatizo ni bei? mkulima anatakiwa naye afurahie bei ya juu! gunia la mahindi likiwa shs 30,000 sawa na kilo tano za nyama ndo mnafurahi? halafu wala gunia hilo kwa miezi mitatu? mkulima akipata bei ya soko DC wa longido anasema ni ulanguzi!
 
Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameitaka Serikali itangaze hali ya hatari kwa upande wa chakula kwani hali ni mbaya kulingana na upungufu wa wa chakula uliopo nchini.

Kama ni kweli je ni sahihi kwa serikali mpaka isukumwe na wanasiasa katika mambo muhimu kama chakula? Kwanini kama chakula hakuna nchini tusiambiwe ili tujiandae?
Kuisukuma serikali ndo kazi ya wanasiasa!
 
Halafu kuna hii kampuni ya MO imenunua mahindi mengi kuliko NFRA wameyapeleka wapi?
 
Ukichoandika ni hisia zako bila facts halafu umeconclude...

Njaa ipo kwa Mafisadi waliozoea vya kunyonga na sasa vya kuchinja vimewashinda.
Ahsante mkuu.
Sikuwa na ugomvi bali ni personal views.
You can as well disregard them and I won't feel offended.
Nashukuru kwa mchango wako mzuri.
 
Tofautisha kuwepo kwa njaa na bei ya chakula kuwa juu! it is a matter of price settled at the market. soko lina chakula, tatizo ni bei? mkulima anatakiwa naye afurahie bei ya juu! gunia la mahindi likiwa shs 30,000 sawa na kilo tano za nyama ndo mnafurahi? halafu wala gunia hilo kwa miezi mitatu? mkulima akipata bei ya soko DC wa longido anasema ni ulanguzi!
Bidhaa yoyote inapoadimika sokoni matokeo yake kilichopo kinapanda bei haiwezekanin bidhaa irundikane sokoni na bei iwekubwa
 
Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameitaka Serikali itangaze hali ya hatari kwa upande wa chakula kwani hali ni mbaya kulingana na upungufu wa wa chakula uliopo nchini.

Kama ni kweli je ni sahihi kwa serikali mpaka isukumwe na wanasiasa katika mambo muhimu kama chakula? Kwanini kama chakula hakuna nchini tusiambiwe ili tujiandae?
atakayetangaza njaa atatumbuliwa siku hiyohiyo kama aliyetangaza zika. hii serikali sio ya spoti spoti ndugu. you do me i do you.
 
Njaa mpk uambiwe na serikali si inaonekana tu kwani huko kwenu haionekani hiyo njaa?
... Ni hivi kwa hii Sheria mpya ya habari ambayo wabunge wale majority walivuta 10 M, ukijitangazia kwamba kuna njaa, hata kama ni kweli, unaitwa mchochezi na waweza jikuta lupango...
 
Wajibu wa serekali ni upi ktk hili
Huyu anaonekana hata haja kubwa ikimbana atasubiri serikali iseme nenda chooni.Serikali ilisema kutakua mvua kidogo,wananchi tupande mazao ya muda mfupi na yanayostahimili ukame.Ulitaka waseme hapo nyumbani kwako unga umeisha?
 
Zitto some time huthibitisha kuwa ni Mwanasiasa wa hovyo hovyo sana
... Tatizo la UKWELI ni kwamba pamoja na kuwa huwa unapanda ngazi, wakati uongo hutumia lift, bado ukweli huwa haupendwi, lakini ukweli hutuweka huru...
 
... Tatizo la UKWELI ni kwamba pamoja na kuwa huwa unapanda ngazi, wakati uongo hutumia lift, bado ukweli huwa haupendwi, lakini ukweli hutuweka huru...

Ukiona Mwanasiasa anakuambia Ukosefu wa Mvua za December Ina maanisha kuna Njaa December hiyo hiyo Na Wewe ukaamini tambua kakuona Zoba wa Viwango vya Standard gauge.
 
Optimists na Pesimists hizi n pande mbili zinazokuwapo katika mjadala wowote unaoendelea nchini ngoja tuone upande gani utakuwa sahihi....mimi niko upande wa ma-Optimists wewe mtoa maada uko upande gani?....yan siamini kama kutakuwa na upungufu wa chakula
... Ulishawahi kulima? Huku Mvomero mashamba yalilimwa tokea Disemba last yr but till now no rains. Nimetoka Moshi, via Tanga, Pwani hali ya ukame ni nomaa... Ukiona mtu machozi yanamlenga lenga halafu wewe ukiendelea kukomaa kwamba kitakachofuata si kilio then jua kuna shida...
 
Zitto some time huthibitisha kuwa ni Mwanasiasa wa hovyo hovyo sana
Haha. wakisema chadema mnasema , mbowe anamuogopa kijana mwenye uwezo.Akisema kwenu mnasema SOMETIMES. hiyo simetimes ni ikiwa kwa ccm tuu ?
 
"Serikali haina chakula cha msaada, nchi ni ya kijani." - JPM

Hivi mbona nyie Watanzania ni wagumu sana kuelewa?! Mshaambiwa hakuna chakula cha bure bali mfanye kazi, bado mnataka serikali iwatangazie!? Iwatangazie nini?!
Hawa sio wale wa tetemeko, ni wale waliolima wafugaji wakafungulia mifugo, ni wale tembo walipita wakala, ni wale waliolima mvua ikaja kiduchu. Ni wale walioshiriki anzishwa kwa ghala la taifa kwa chakula cha dharura?
 
Back
Top Bottom