Zitto aitaka serikali kutangaza njaa nchini

[QUOTE="K M S, post: 19195909, member: 404570"]Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameitaka Serikali itangaze hali ya hatari kwa upande wa chakula kwani hali ni mbaya kulingana na upungufu wa wa chakula uliopo nchini.

Kama ni kweli je ni sahihi kwa serikali mpaka isukumwe na wanasiasa katika mambo muhimu kama chakula? Kwanini kama chakula hakuna nchini tusiambiwe ili tujiandae?[/QUOTE]
Labda mimi nimepitwa na wakati, kumbe Zitto ndo mwenyekiti wa ACT wazalendo? Kile cheo ayatollahhhkhomeney kamwachia nani?
 
"Serikali haina chakula cha msaada, nchi ni ya kijani." - JPM

Hivi mbona nyie Watanzania ni wagumu sana kuelewa?! Mshaambiwa hakuna chakula cha bure bali mfanye kazi, bado mnataka serikali iwatangazie!? Iwatangazie nini?!
Nchi ya kijani? ukpanda leo unavuna kesho?
 
Hakuna baunsa kwenye njaa its a matter of time kila kitu kitaeleweka
 
Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameitaka Serikali itangaze hali ya hatari kwa upande wa chakula kwani hali ni mbaya kulingana na upungufu wa wa chakula uliopo nchini.

Kama ni kweli je ni sahihi kwa serikali mpaka isukumwe na wanasiasa katika mambo muhimu kama chakula? Kwanini kama chakula hakuna nchini tusiambiwe ili tujiandae?
Wakuu tulijadili hili kwa umakini tukiwa SOBER/ TUMETULIA kimawazo. Maana njaa haiangalii chama.

Ukweli ni kuwa hali ya chakula/FOOD SECURITY PROJECTION ni MBAYA sana na haihitaji KULAUMIANA bali KUAMSHANA. Bila kujali KAULI tata zilizotolewa hapo awali na wanasiasa maana zitatufanya tusiwaze yajayo.

Mimi NASHAURI kuwa rais Magufuli ALIZUNGUMZIE hili kama AJENDA maalumu katika baraza lake la MAWAZIRI.

Halafu AWAITE MABALOZI wa nchi za JUMUIA ya ULAYA, UINGEREZA na MAREKANI na kutoa TAARIFA safi iliyoandikwa SAFI ya kuitangaza Tanzania kuwa INAKUBWA na BAA la NJAA/NATIONAL DISASTER.

Na inahitaji MISAADA ya DHARURA ili KUYANUSURU maisha ya mamilioni ya watu ambao kama JUMUIA ya KIMATAIFA hataingilia kati,
Serikali hawataweza peke yao na watu watakufa!

Taarifa hiyo ITOLEWE hasa baada ya TRUMP KUAPISHWA kwa sababu zilizo wazi.

Jambo lingine serikali iruhusu WAFANYABIASHARA kuagiza CHAKULA kulingana na METRIC tones defecit ya chakula hitajika hapo tutapona.

Lakini jambo hili la kutupiana mpira, sijui mara ni CCM walisema hivi, mara ni Upinzani wanataka hivi, haitasaidia matokeo yake tutawaumiza bure wananchi maana wao wanachohitaji ni chakula na si SIASA!
 
Ukiona hivyo ujue Zitto ameshapenyezewa taarifa nyeti na watu kutoka serikalini na sio kama anaropoka tu.
 
Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameitaka Serikali itangaze hali ya hatari kwa upande wa chakula kwani hali ni mbaya kulingana na upungufu wa wa chakula uliopo nchini.

Kama ni kweli je ni sahihi kwa serikali mpaka isukumwe na wanasiasa katika mambo muhimu kama chakula? Kwanini kama chakula hakuna nchini tusiambiwe ili tujiandae?
Zitto siyo Mwenyekiti wa ACT Wazalendo.
 
Wakuu tulijadili hili kwa umakini tukiwa SOBER/ TUMETULIA kimawazo. Maana njaa haiangalii chama.

Ukweli ni kuwa hali ya chakula/FOOD SECURITY PROJECTION ni MBAYA sana na haihitaji KULAUMIANA bali KUAMSHANA. Bila kujali KAULI tata zilizotolewa hapo awali na wanasiasa maana zitatufanya tusiwaze yajayo.

Mimi NASHAURI kuwa rais Magufuli ALIZUNGUMZIE hili kama AJENDA maalumu katika baraza lake la MAWAZIRI.

Halafu AWAITE MABALOZI wa nchi za JUMUIA ya ULAYA, UINGEREZA na MAREKANI na kutoa TAARIFA safi iliyoandikwa SAFI ya kuitangaza Tanzania kuwa INAKUBWA na BAA la NJAA/NATIONAL DISASTER.

Na inahitaji MISAADA ya DHARURA ili KUYANUSURU maisha ya mamilioni ya watu ambao kama JUMUIA ya KIMATAIFA hataingilia kati,
Serikali hawataweza peke yao na watu watakufa!

Taarifa hiyo ITOLEWE hasa baada ya TRUMP KUAPISHWA kwa sababu zilizo wazi.

Jambo lingine serikali iruhusu WAFANYABIASHARA kuagiza CHAKULA kulingana na METRIC tones defecit ya chakula hitajika hapo tutapona.

Lakini jambo hili la kutupiana mpira, sijui mara ni CCM walisema hivi, mara ni Upinzani wanataka hivi, haitasaidia matokeo yake tutawaumiza bure wananchi maana wao wanachohitaji ni chakula na si SIASA!
Huwa sio rahisi kulizungumzia mpaka watu waanze kufa kwa njaa.
 
Zitto some time huthibitisha kuwa ni Mwanasiasa wa hovyo hovyo sana
Nadhani akhui huko vijijini mpaka sasa mvua hakuna na mbegu zinakauka juu kwa juu juzi nilienda ifakara na vijiji vyake yaan mchele pia wamepunguz wakulima kukoboa kwa kuhofia mvua sasa kwa miji kame unategemea nn hii anaofanya zitto ni kama kualert serikali lkn uhalisia mvua hkn na panicking ishaanza kwa wakulima
 
dscn0425.jpg

Kiongozi wa Chama cha ACT –Wazalendo, Zitto Kabwe ameitaka Serikali kutangaza rasmi baa la njaa kwa mujibu wa sheria kutokana na hali ya chakula kuwa mbaya nchini.

Kauli ya Zitto imetolewa wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisisitiza utunzaji wa chakula baada ya kukagua maghala ya nafaka yanayomilikiwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Kanda ya Songea.

Agizo la Majaliwa pia limetolewa siku mbili baada ya Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba kutofautiana na Zitto kuhusu hali ya chakula ambapo Waziri huyo alisema hali ya chakula nchini ni shwari huku Mbunge huyo wa Kigoma Mjini akisema ni mbaya.

Jana, mbunge huyo akihutubia mkutano wa kampeni ya kumnadi mgombea udiwani Kata ya Nkome, Geita aliendelea kupigilia msumari kauli yake akisema, “Hali ya chakula ni mbaya, ni mbaya, ni mbaya.”

Alisema baada ya ziara ya Waziri Mkuu kwenye maghala ya Taifa na kujionea hali ya chakula nchini, ni vyema Serikali ikachukua hatua.

“Ninapendekeza Serikali ichukue hatua muhimu ya kisheria ya kutangaza baa la njaa nchini. Tamko la baa la njaa litaisaidia Serikali kupata bajeti ya dharura ya kununua chakula na kutoa uhuru kwa wakuu wa wilaya kutangaza bila woga kuwa maeneo yao yana njaa,” alisema Zitto huku akimpongeza Majaliwa kwa ziara hiyo.

Chanzo:Zitto ataka Serikali kutangaza baa la njaa
 
Nadhani akhui huko vijijini mpaka sasa mvua hakuna na mbegu zinakauka juu kwa juu juzi nilienda ifakara na vijiji vyake yaan mchele pia wamepunguz wakulima kukoboa kwa kuhofia mvua sasa kwa miji kame unategemea nn hii anaofanya zitto ni kama kualert serikali lkn uhalisia mvua hkn na panicking ishaanza kwa wakulima

Kutangaza Njaa na Ukame ni vitu viwili tofauti Ndugu yangu. Ukiona kuna Ukame Muda huu basi Njaa yake si ya Leo ni Mwezi wa Sita kwa kuwa ndio Mwezi wa Mavuno ya kinachopandwa sasa.

Kama kuna Njaa sasa hivi ni Matokeo ya ukosefu wa Chakula cha Mavuno yaliyopita nadhani ingekuwa sahihi Zitto angeshauri utangazwe Ukame sio Njaa kwa sasa Kama Msingi wake ni ukosefu wa Mvua za Mwisho wa Mwaka!
 
Sawa lkn serikali hii ispokuwa alerted mapema itakumbuka shuka kumechuka na unajua madhara ya njaa ikiwa hata ghala zako hazina akiba yakutosha
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tupime:

Ulipo, mchele wa bei ya chini kilo shillingi ngapi?

(Kwa mimi, wali ni chakula. Ugali ni rizki).
 
Sawa lkn serikali hii ispokuwa alerted mapema itakumbuka shuka kumechuka na unajua madhara ya njaa ikiwa hata ghala zako hazina akiba yakutosha

Hoja hapa ni Zitto kui alert Serikali au kuitaka Serikali itangaze Baa la Njaa kitaifa?

Zitto ni Mwanasiasa Mjanja mjanja hapo anajaribu kuingiza Mkenge Serikali itangaze Njaa kitaifa na Matokeo yake itokee Inflation kutokana na Public speculation kuwa Vitu vitaadimika hivyo wataficha bidhaa na Matokeo yake itokee uhaba Kama wa Sukari , usipokuwa Makini na Wanasiasa Kama Zitto unaweza ukaingia Mkenge.

Zitto ni Propagandist Mzuri sana japo si mhamasishaji mzuri na Chadema ni wahamishaji sana wa Propaganda japo si wazuri wa Propaganda hivyo kutengana kwao ni Jambo zuri kwa Mustakbali wa Nchi yetu na Siasa zetu
 
Mungu atuepushe na njaa, yaliopo yanatosha.
 
Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameitaka Serikali itangaze hali ya hatari kwa upande wa chakula kwani hali ni mbaya kulingana na upungufu wa wa chakula uliopo nchini.

Kama ni kweli je ni sahihi kwa serikali mpaka isukumwe na wanasiasa katika mambo muhimu kama chakula? Kwanini kama chakula hakuna nchini tusiambiwe ili tujiandae?
Kiongozi wa ACT wazalendo......Mwenyekiti ni Anna Mghwira
 
Back
Top Bottom