Zitto aitaka serikali kutangaza njaa nchini

K M S

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
524
424
Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameitaka Serikali itangaze hali ya hatari kwa upande wa chakula kwani hali ni mbaya kulingana na upungufu wa wa chakula uliopo nchini.

Kama ni kweli je ni sahihi kwa serikali mpaka isukumwe na wanasiasa katika mambo muhimu kama chakula? Kwanini kama chakula hakuna nchini tusiambiwe ili tujiandae?
 
"Serikali haina chakula cha msaada, nchi ni ya kijani." - JPM

Hivi mbona nyie Watanzania ni wagumu sana kuelewa?! Mshaambiwa hakuna chakula cha bure bali mfanye kazi, bado mnataka serikali iwatangazie!? Iwatangazie nini?!
 
nakumbuka mkuu alisemaga kuwa mkuu wa wilaya atakaelalamika kuwa kuna njaa ndani ya wilaya yake hatoshi kwenye hiyo nafasi sasa leo hii akitangaza kwenye level ya nchi maana yake ni kuwa yeye mwenyewe............kwenye hiyo nafasi hivyo msitegemee kama mtatangaziwa zaidi kila mtu ajipange tu.
 
Inawezekana kuna njaa au ama hakuna kwa sass.....ila huko tuendako lazima hali tete ya chakula itaikumba hii Nchi.....rejea kauli ya Waziri wa fedha khs kushuka kwa sekta ya kilimo Nchini.
 
Kwa sisi wa Nyanda za juu kusini ambao ndio kwanza tunajiandaa na palizi ya kwanza ni mapema mno kutangaza njaa, labda kwa wale waliouza akiba zao za chakula kwa tamaa ya bei nzuri zilizopo sasa. Debe la Mahindi 20,000- haijawahi kutokea

Pia tunakodoa kodo kuona mkuu wa wilaya wa kwanza kutangaza njaa wilayani mwake atumbuliwe pwaaaaaa. Hapa Kazi Tu, je tutafanya kazi na njaa?
 
Optimists na Pesimists hizi n pande mbili zinazokuwapo katika mjadala wowote unaoendelea nchini ngoja tuone upande gani utakuwa sahihi....mimi niko upande wa ma-Optimists wewe mtoa maada uko upande gani?....yan siamini kama kutakuwa na upungufu wa chakula
 
Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameitaka Serikali itangaze hali ya hatari kwa upande wa chakula kwani hali ni mbaya kulingana na upungufu wa wa chakula uliopo nchini.

Kama ni kweli je ni sahihi kwa serikali mpaka isukumwe na wanasiasa katika mambo muhimu kama chakula? Kwanini kama chakula hakuna nchini tusiambiwe ili tujiandae?
Njaa gani?
 
Back
Top Bottom