Haya yote unayosifia kufanyqa na kikwete 80% ni pressure ya wabunge na nje ya bunge ni pressure ya upinzani na wanaharakati. Ila ukitaka kuoka ana kigugumizi ona alivyoshughulikia issue za epa,richmond,escrow n.k ndo utagundua kikwete alikuwa hawezi maamuzi magumu yote aliyafanya kwa pressure ya upinzani. Hta mawaziri wengi kutimuliwa ni baada ya ripoti za PAC kusomwa bungeni na kutishia kumng'oa waziri mkuu ndo kikwete anakuja mwishoni anasimamisha mawaziri tena kwa kigugumizi kma siku ile alipomsimamisha tibaijuka akasema eti "uwapishe kidogo maana maneno mengi" sasa hapo huoni alikuwa ana-act kwa pressure ila alikuwa hana nia ya dhati moyoni ya kushughulikia ufisadi.
Wewe hujui Siasa zinaendeshwaje!!
Zitto alipewa PAC na Kikwete na hata taarifa Nyeti za kifisadi alikuwa akipewa na Kikwete ili kuwachomoa wasiohitajika!
Unajua kwanini Jk alimuacha Prof Issa Shivji aliekuwa akitajwa sana kwny Tume ya Katiba na kuwapa Maadui zake kina Warioba na Mzee Butiku waliokuwa wanamshambulia daily kwny Kigoda cha Mwalimu Nyerere?
Siasa ni mbinu na Jakaya alitumia Bunge na Vyama vya Upinzani kutimiza Malengo yake ya Kisiasa.
Mpaka Leo Lowassa kupoteza Uwaziri Mkuu wale analia na Jk sio Bunge wala Mwakyembe.
Leo hii Mbowe na Chadema wakikumbuka walivyowezeshwa bila ya kujijua kutangaza Ufisadi wa Richmond na wa Lowassa kwa Miaka nane wanabaki kuhuzunika jinsi walivyoshindwa kung'amua Michezo ya Kisiasa.
Wewe unamjua aliempa Report ya Buzwagi Zitto Kabwe ili kumyofoa Nazir Karamagi?
Unajua kwanini Taarifa za Epa na Kagoda Agrilcuture ya Rostam Azizi alikabidhiwa Dr. Slaa na Saed Kubenea ili kummaliza Tycoon wa Siasa za Kimafia Rostam Azizi na kweli akapotea na Akina Kubenea enzi hizo wanajua Jk kapoteza Mtu muhimu Kumbe yeye ndo Architecture wa Kaburi la Kisiasa la Wanamtandao wenzake
Unajua ili kumchomoa Andrew Chenge kwny Uwaziri wa Miundombinu ilitokana na habari tu iliyoandikwa kwny Guardian la Uingereza kuhusu kuhifadhi only 1.2 Billion kwny Account za Nje unafahamu kina Nani walizisambaza hizo habari na kushadadiwa bila ya kujua Msusi wa hiyo Michezo ni Nani?
Jakaya Kikwete alikuwa akitumia mbinu ya kujifanya Dhaifu ili watu wambeze nae akawa anawatumia bila ya kujijua.
Yule Jakaya inawezekana akawa hakuwa Kiongozi Mzuri kwa maana ya Matarajio ya baadhi ya watu Ila atakaekwambia alikuwa Mwanasiasa Dhaifu huyo hajui Siasa ni nini !
May 4, 2005 Mzee Mkapa akitokea Kwny Mei Mosi Songea aliweka Kambi sehemu Kule Chamwino na kuanza kupitia Majina ya Wagombea Urais akiwa na Wazee wa System Kumbe wote walimzunguka Mzee walikuwa Vijakazi wa Jakaya na kila Mkapa akifurukuta alikuwa anapewa Vitisho hewa kuwa akimkata Jk Chama kingepasuka Kumbe ulikuwa Mkwara Mbuzi.
Sifukui Makaburi Ila hata Waliohesabu kura za Mwandosya na Dr. Salim Ahmed Salim kwny Tatu bora ya 2005 walikuwa Wanamtandao [emoji3][emoji3][emoji3] kindaki ndaki, Meneja wa Kampeni za Mwandosya alikuwa Msiri wa Jk na mpaka Leo ni Mh. Waziri kwa ushawishi wa jk.