Jamani wote tupo mtaani tunaona hali halisi. Wakulima wanaona utofauti msimu uliopita na huu
Faru j ashasema serikali haina shamba. So tusubiri msaada wa chakula kutoka china
Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameitaka Serikali itangaze hali ya hatari kwa upande wa chakula kwani hali ni mbaya kulingana na upungufu wa wa chakula uliopo nchini.
Kama ni kweli je ni sahihi kwa serikali mpaka isukumwe na wanasiasa katika mambo muhimu kama chakula? Kwanini kama chakula hakuna nchini tusiambiwe ili tujiandae?
Hata Mimi nakuunga mkono ila tofauti kidogo tu..kuongea kile ambacho kipo kwa takwimu za uhakika. Mfano hiyo hali ya chakula ni taarifa ya Uchumi ya BOT kwa robo iliyopita. Ila uhalisia njaa ipo sana tu tujihadhari.
NILAANA ZA KUWANYANYASA WANYONGE. WAO WANAKULA NA KUNYA HAWANA HABAR NA WENGINE.
KESHASEMA PHARAOH KILA MTU ATABEBA MSALABA WAKE. Wasitangaze wakae kimya tu
Hata Mimi nakuunga mkono ila tofauti kidogo tu..kuongea kile ambacho kipo kwa takwimu za uhakika. Mfano hiyo hali ya chakula ni taarifa ya Uchumi ya BOT kwa robo iliyopita. Ila uhalisia njaa ipo sana tu tujihadhari.
Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameitaka Serikali itangaze hali ya hatari kwa upande wa chakula kwani hali ni mbaya kulingana na upungufu wa wa chakula uliopo nchini.
Kama ni kweli je ni sahihi kwa serikali mpaka isukumwe na wanasiasa katika mambo muhimu kama chakula? Kwanini kama chakula hakuna nchini tusiambiwe ili tujiandae?
Wakinanani hao??? Majanga hupangwa na Mungu sawa ila hatua zinazochukuliwa baada ya hapo ni mipango ya Mungu???
Kikwete hatukumsakama kwa sababu kulikuwa na ufisadi la hasha tulimkosoa kwa hatua alizochukua baada ya JANGA la ufisadi kutokea kwenye taasisi tofauti.
Kwa mwendo huohuo ndio huwa tunakosoa tukiona hatua zinazochukuliwa baada ya janga kuwa hazina ufanisi wowote.
Kwa hyo watakaomkosoa magu kuhusu mada hii ya njaa watamkosoa kwa hatua anazochukua baada ya kugundua JANGA hili ila sitegemei kuna atakayemlaumu kwa JANGA hili kma ulivyosema ni mpango wa Mungu kukosekana mvua.
KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameitaka Serikali itangaze rasmi baa la njaa kwa mujibu wa sheria.
Zitto alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Nkome mkoani Geita kupitia ACT-Wazalendo.
“Hali ya chakula nchini si nzuri. Wananchi mmeshuhudia namna bei za vyakula zinavyopanda kila siku. Bei ya sembe sasa kilo moja imefikia shilingi 1,600 pale Morogoro, kilo moja ya mchele ni shilingi 1,500, maana yake leo ugali na wali imekuwa bei inafanana. Gharama za maisha zitaendelea kupanda kutokana na uhaba wa chakula kuwa mkubwa.
“Kwanini hali ya chakula inazidi kuwa mbaya? Ni kwa sababu ya uamuzi mbovu wa Serikali kuhusu hifadhi ya chakula. Serikali zote zilizopita huko nyuma zilikuwa zinanunua chakula cha akiba ili wakati wa ukame kama sasa chakula hicho kiingie sokoni na hivyo kushusha bei na kuwezesha wananchi kumudu gharama za chakula.
“Rais wetu kawaambia wananchi wa Kagera kwamba Serikali haina shamba hivyo hakuna chakula cha njaa. Hii kauli si ya uongozi. Ni kauli ya kuficha uamuzi wa Serikali uliotusababisha kukosa akiba ya chakula,” alisema.
Zitto alisema Ghala la Taifa la Chakula (NFRA) lina tani 90,000 tu za chakula wakati kwa kipindi kama hiki mwaka juzi lilikuwa na tani 450,000.
Kwa mantiki hiyo, alisema chakula kilichopo kwa sasa ndani ya ghala hilo kinatosha kwa wiki moja kwa mujibu wa takwimu katika taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa mapitio ya uchumi ya Novemba, mwaka jana.
“Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba, alijibu hoja hizi kwa wepesi kabisa na kusema kwamba Tanzania ina chakula cha kutosha. Alipoulizwa ataje kiasi kilichopo NFRA, alijibu kwa sababu za kiusalama hawezi kutaja,” alisema.
Zitto alikwenda mbali kwa kumpongeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kwa kuamua yeye mwenyewe kutembelea NFRA na kujionea hali halisi.
Alisema alichokifanya Majaliwa ndio uongozi na si viongozi kukanusha habari ambazo ni za kweli na zilishathibitishwa na taasisi za Serikali kama BoT na alimtaka kuwachukulia hatua viongozi wa Serikali wanaoficha ukweli kuhusu baa la njaa.
“Waziri wa Kilimo anasema kama wananchi wanaona ugali ni ghali wale wali. Anasema kuna mchele mwingi nchini, lakini umeshikwa na watu binafsi. Waziri anataka kuwaambia Watanzania kuwa hivi sasa Serikali inategemea chakula cha watu binafsi ambao haijui idadi ya tani zilizopo kushughulika na suala la njaa.
“Hii ni ajabu kubwa sana, nchini Ufaransa alitokea mke wa mfalme mmoja. Wananchi walikuwa wanalalamika kuwa hakuna mikate. Malkia yule akiitwa Marie Antonnoite, alimwambia mumewe, hawa watu wako kama hawana mikate si wale keki? Hii ndio hali ya sasa nchini. Waziri anasema kama sembe imekuwa ghali, wananchi wale wali. Anasahau kuwa hata mchele umepanda bei. Maharage yamepanda bei na mafuta ya kupikia yamepanda bei,” alisema.
Kauli ya Majaliwa
Katikati ya wiki hii, Majaliwa, akiwa mkoani Ruvuma alitoa agizo la kusisitiza kutunza chakula kwa kusema akiba ya mahindi iliyopo iendelee kutunzwa hadi msimu ujao wa mavuno.
Alitoa agizo hilo baada ya kukagua maghala ya nafaka yanayomilikiwa na NFRA Kanda ya Songea.
Alisema kawaida mwezi huu mvua za kutosha huwa zinanyesha na huwa kuna baridi lakini mwaka huu imekuwa tofauti kwa sababu kunashuhudia kuwapo joto kali.
“Kama mvua haijanyesha hadi leo ni lazima tuchukue tahadhari, hata mvua ikija hatujui itaendelea kunyesha hadi lini na kwa kiasi gani,” alisema.
Majaliwa aliwataka wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kutoa elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa akiba ya chakula.
nakumbuka mkuu alisemaga kuwa mkuu wa wilaya atakaelalamika kuwa kuna njaa ndani ya wilaya yake hatoshi kwenye hiyo nafasi sasa leo hii akitangaza kwenye level ya nchi maana yake ni kuwa yeye mwenyewe............kwenye hiyo nafasi hivyo msitegemee kama mtatangaziwa zaidi kila mtu ajipange tu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.