Zitto adai ripoti ya TISS yaonyesha Rais Magufuli hawezi kushinda 2020

Ni kweli sio sawa kusema kwamba hana vya kuonyesha maana hivyo anavyo. Ila hata makuburu wa Afrika kusini walikuwa na maendeleo ya kuonyesha ambayo hata Magufuli awe rais wa maisha hatayafikia, lakini akina Mandela na wenzake waliwakataa.
Vijana wanaohisi kwa kupiga debe tumbo litashiba hawaelewi mambo kama haya! Wengi hawana uwezo wa kupambanua mawazo makubwa kama haya
 
Aisee!!
Nauliza tu!? Tiss wanaitumikia Tanzania "umma" au CCM?
Tunaomba hii Taasisi iwe huru kama Mossad, CIA..... Wasiendelee kuwa kitengo ndani ya ccm!! Hatuwatendei haki watanzania na watumishi wenye weledi ndani ya TISS!!
hapo umenena mkuu
 
Uchaguzi gani ulishashindwa au kushinda kabla ya kura kupigwa. Zitto una matatizo siyo bure. Nilikuwaga nakuona wa maana enzi zile tunawaona kwenye ITV mligomaga ili muongezewe bumu some one Mkili akakamatwa. Nakumbuka niliona kwenye TV na Omary na mkaka mmoja mweusi anavaa miwani mnasema Mkili must be free na kweli alitoka celo. Sasa naona umegauka na kuwa vuvuzela tu.
Iko wapi hiyo ripoti yenyewe watanzania waione?
Au ni kwaajili ya zito pekee?
 
Ofcourse TISS kabla ya uchaguzi huwa wanafanya utafiti wao kujua nani anakubalika mbele ya wananchi.

Kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015, ilikuwa around 2013/2014 na kabla ya Lowasa kuhamia Chadema Ripoti ya "KITENGO" ilionyesha kuwa miongoni mwa possible candidates nchini, Magufuli anakubalika sana kwa wananchi

Sasa sishangai tena ripoti kama hiyo ya TISS kuonyesha kuwa hakubaliki, Huwa wanafanya utafiti kujua hali ya kinchi inakwendaje.

Kinachomkwamisha JPM ni Uchumi uchumi uchumi uchumi uchumi na Demokrasia na haki za binadamu
Maisha ya watu yako duni, biashara zinakufa, Kilimo ambacho kinagusa watu wengi hajakipa kipaumbele, Hali ya usalama wa raia (mambo ya utekaji) ni ya mashaka, uonevu kwa wapinzani, wananchi hawapendi mambo ya maguvumaguvu kwenye siasa, ajira kwa vijana, Maslahi ya wafanyakazi, Stahiki za wastaafu etc

Amebaki kuonyesha SGR, Stieglers, Flyover, Uwanja wa Ndege Chato, Daraja la Kigamboni etc
URAIS NI ZAIDI YA UJENZI
Hiyo ripoti inapatikana wapi?
Kama una access hebu iweke hapa hata link tuisome uzuri....
 
Zitto anaelekea kupata kichaa
Yaani Magufuli ashindwe kutuonesha
SGR
STIEGLERS GORGE
AMEJENGA HOSPITALI 60 kwa miaka.mitatu,wakati toka huru zaidi 50 yrs tuna hosputali.60 tu
Amekarabati shule kongwe zaidi ya 20,ikiwemo kigoma sekondari
Viwanda zaidi 2,000 vimeanzishwa
Amefuta kodi kandamizi zaidi 50
Elimu bure kuanzia msingi mpaka upili
Mikopo elimu ya.juu imeboreshwa
Ameanzisha vituo vya kuuza madini nchi nzima
Kwa hayo machache tu.mie sipotezi kura yangu,ni Magufuli tu
 
Mimi Victoire wa Tanzania. Victoire ni role modal wangu alinishangaza alivyoacha mme na watoto kurudi Rwanda kupambana na Simba ana kwa ana. Hapo tu ndo simuungi mkono.
Ndio ushujaa wenyewe huo, history will vindicate her sometime! cheers.
 
Aisee!!
Nauliza tu!? Tiss wanaitumikia Tanzania "umma" au CCM?
Tunaomba hii Taasisi iwe huru kama Mossad, CIA..... Wasiendelee kuwa kitengo ndani ya ccm!! Hatuwatendei haki watanzania na watumishi wenye weledi ndani ya TISS!!
umewapima vipi hao Mossad,CIA watanganyika bhana
 
Zitto anaelekea kupata kichaa
Yaani Magufuli ashindwe kutuonesha
SGR
STIEGLERS GORGE
AMEJENGA HOSPITALI 60 kwa miaka.mitatu,qakati toka huru zaidi 50 yrs tuna hosputali.60 tu
Amekarabati shule kongwe zaidi ya 20,ikiwemo kigoma sekondari
Viwanda zaidi 2,000 vimeanzishwa
Amefuta kodi kandamizi zaidi 50
Elimu bure kuanzia msingi mpaka upili
Mikopo elimu ya.juu imeboreshwa
Ameanzisha vituo vya kuuza madini nchi nzima
Kwa hayo machache tu.mie siporezi kura yangu,ni Magufuli tu
Nikusahihishe hapo kwenye viwanda mkuu. Ni viwanda elfu nne (4,000).

Asante!
 
Back
Top Bottom