Hayati Magufuli aliwatumia sana TISS. Pangua ya Rais Samia anataka nini?

Mtanke

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
715
1,774
Mambo mengi aliyofanya Magufuli pamoja na viongozi wengi aliowateua walitokana na TISS. Hata Bunge lenyewe limejaa TISS. Mama kashaondoa wakuu wawili wa TISS ikimaanisha hawafanyi anavyotaka.

Swali langu ni Je mama anataka nini? Kupangua mambo ya TISS hao hao waliyoyatekeleza wakati wa Magufuli au?

Trump aliwahi kumuuliza Comey can I have your loyalty?. Comey alishituka sana na akaandika hilo swali kwenye notebook yake.

Huenda Mama nae anatafuta loyalty ya hawa TISS ndio maana anawapangua pangua. TISS ni kama buibui Rais ukijifanya inzi wanakutanda tu.
 
Hivi mama huwa anajua TISS ni chombo kilichojengwa na watu wenye undugu na kujuana sio uwezo wa kufanya kazi. TISS kama wapo serious wawatafute staff wao toka utumishi wa umma ambao tayari wana ajira zao kwenye nafasi za juu kuanzia mikoani sio hao watoto wa viongozi wa TISS waliopo sasa. Kuna siku hawa watoto wakiunda syndicate yao watasumbua hili taifa maana hawana maadili
 
Kesho uje uwaponde tiss maana nyie watu wa JF hamueleweki.
Leo mtasifiia kesho mtaponda kile kile mlichokisifia jana.

Kama Nay wa Mitego, kipindi alimkashifu kipind hiki anasema kam-miss. Acha nicheke mie.
 
Hivi mama huwa anajua TISS ni chombo kilichojengwa na watu wenye undugu na kujuana sio uwezo wa kufanya kazi. TISS kama wapo serious wawatafute staff wao toka utumishi wa umma ambao tayari wana ajira zao kwenye nafasi za juu kuanzia mikoani sio hao watoto wa viongozi wa TISS waliopo sasa. Kuna siku hawa watoto wakiunda syndicate yao watasumbua hili taifa maana hawana maadili
Watoto gani mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom