Zitto: ACT Hatutaki Anasa, Usafiri Wetu Treni!

Zitto: ACT Hatutaki Anasa, Usafiri Wetu Treni!

Nakubaliana na wewe, ukiangalia historia ya dunia ni kwamba
watu hufanya mabadiliko ktk maisha na mazingira wanayoishi kuangalia the past! Yaani kwa kimombo wanasema"The past predict the Future " Ktk historia ya Tanzania, ujamaa ni the Past ambayo ilifeli kuwakomboa wananchi Kiuchumi, elimu na kisayansi. Nakumbuka miaka ya 1980,1981,82 mpaka Kuritire kwa Mwalimu JK, Wananchi tulijipanga kupigiania mahindi ya njano, sukari ilikuwa kama dhahabu, tulifua nguo na maji ya mipapai. Huduma zilipatikana kwa shida ktk mashirika ya umma. Vitu kama TV, gari, friji na vitu kama hivyo, tuliambiwa ni Anasa! Kweli friji au TV au gari ni anasa? Ktk nchi zilizoendelea hivi ni vitu ambavyo ni lazima uwe navyo kukurahisishia maisha. Leo 2015 mtu anakuja anasema kwa akili yake kwamba mimi nataka kuwarudisha ktk siasa ya Ujamaa. Hivi kweli hii inaingia akilini? Sijuhi Zito alikuwa na umri gani kwenye miaka hiyo ya early 1980's but anatakiwa kutambua kuwa watanzania tumesafa chini ya Ujamaa mpaka hata Baba wa Taifa alikubali hilo katika moja ya interview na redio moja ya nje. Mimi kama Mtanzania ningependa kuona wana siasa wanakuwa wakweli kulikoni kuhubiri kitu ambacho tulijaribu na tukashindwa vibaya. Namtakia bwana Zito kila laheri but Ujamaa sio Gia ya kutuambia ktk hii karne ya 21.

Zito ni fisadi mkubwa mjaamaa ana fadhiliwa na mafisadi!!maajabu
 
Wana Ukumbi,

Kama Watanzania tunataka chama cha siasa chenye nidhamu ya matumizi ya pesa, basi ACT ndio chama sahihi!

Zitto ameendelea kuonyesha tabia yake ya kujali raslimali kwa kuzitumia kwa uangalifu mkubwa huku akifikiria wanyonge wa nchi hii ambao wengi wao wako kijijini.

Katika kutekeleza hilo, Zitto ameamua kufanya ziara za chama hicho (kwa awamu ya pili) kwa kutumia treni kwa kuwa itapita maeneo ambayo ACT imeyakusudia kwa awamu ya pili!

Watanzania, matukio haya ambayo tunayoyaona ndani ya ACT ni ukumbusho wa ujamaa wa Mwalimu wakati wa CCM ile ya enzi za azimio la Arusha.

Zile Million 700 zimeshaingia?
 
Kaazi kweli kweli, ina maana siku ya kupiga kura ikifika mpiga kura akifika kwenye ballot box ni sababu gani za msingi atumie kuichagua kati ya CDM na ACT.

Maana kikubwa kwenye maswala ya ushaiwshi kwa wenzetu ni kuchagua kati ya chama cha Zitto na mgombea wa CDM bila ya reason muhimu zinazoeleweka as alternative to the ruling party. Na kuna watu watapiga kura kwa sababu hizo ujue: haya mambo yanawezekana third world only imagine siasa zetu zingekuwa na misingi ya ukabila maana sioni jitihada za ahadi kabisa kwenye chaguzi hizi za kuwafanyia nini wapiga kura.

Siasa za Tanzania conundrum.
 
Hapa baba rizy alipanda ya tazara ila inakufa kuwafuata walioijenga
 
Zitto sijui anamdamganya nani na siasa zakuigiza hizi
 
Mbalinga hebu jiangalie kwenye kioo halafu ujicheke mwenyewe.!!maana kwa chuki hiyo lazima uwe mwendawazimu. Sio watz wanaotaka kujua wafadhili wa mikutano watz wameelewa labda wewe binfsi
 
Ndiyo maana hatumtaki kwavile upeo wake wa kufikiria ndiyo umeishia hapo. Wakati watu wanagundua vifaa vya kwenda mwezini yeye bado ameng'ang'ania treni ya kigoma.
 
Alishawahi kuwa na range alipoona ni shida akahamia kwenye caldina zile ndefu kupoteza ushahidi,kwahiyo hilo sio geni anaweza.usishangae akatumia toyo kupita mtaani,
 
Zitto hana jipya zaidi ya kufanya siasa za maigizo,siasa ambazo haendani nazo na haziendani na wakati tuliopo.

Kama ana vyoleta hadithi za kutembea kwa train wakati yeye mwenyewe ana miliki na kutembelea magari ya kifahari.

Wakati mjamaa Nyerere anae jaribu kumuiga aliishi maisha yanayofanana na viongozi wenzake wote pamoja na watanzania wote kwa ujumla wao.

Akisema kuwa wananchi wote watatumia magari aina ya Land rover na itakuwa hivyo kuanzia kwake mwenyewe kwanza na kwa viongozi wenzake wote na kushuka mpaka kwa wananchi wa kawaida.
 
Shangingi moja sawa na zahanati nne, maneno ya ya slaa kwenye kampeni 2010,
Baada ya kuingia bungeni kiongozi wa kambi rasimi ya upinzani anatembelea zahanati nne.

Sawapendi chadema ni walaghai, wanafiki, wazandiki, mafisadi, na matapeli wa kisiasa wanasema kile wasichoweza kuishi. Tuwaogope kama ukoma.
Mkombozi wa kweli ni ACT wazalendo wa kweli walioamua kuirudisha nchi yetu kwenye misingi ya mwasisi. Ili kila mwannchi aweze tuweze kugawana kwa usawa keki ya taifa.
 
Hivyo ndivyo inavyotakiwa kiongozi uwe mfano kwa wengine, team wazalendo
 
At least this is not coming from the horse's mouth, maana isije siku akaonekana ana shuka ndani ya ndege hapo Kigoma airport wakati asilimia kubwa ni kwa mtindo wa mabasi na train kuitafuta dar, worse still aonekane akisafiri na gari binafsi lenye engine ya zaidi ya four little ambapo gharama ya kwenda na kurudi ni zaidi ya mshahara wa wafanyakazi wengi wa umma.

Usijipe thamani ambayo unajua uwezi kuishi nayo baada ya political campaigns we sema tu una nia gani atakama mbinu zenyewe azina maelezo so far bora ahadi za aina hiyo.
 
Shangingi moja sawa na zahanati nne, maneno ya ya slaa kwenye kampeni 2010,
Baada ya kuingia bungeni kiongozi wa kambi rasimi ya upinzani anatembelea zahanati nne.

Sawapendi chadema ni walaghai, wanafiki, wazandiki, mafisadi, na matapeli wa kisiasa wanasema kile wasichoweza kuishi. Tuwaogope kama ukoma.
Mkombozi wa kweli ni ACT wazalendo wa kweli walioamua kuirudisha nchi yetu kwenye misingi ya mwasisi. Ili kila mwannchi aweze tuweze kugawana kwa usawa keki ya taifa.

Kwani alichosema Slaa ni uwongo?kwani hilo shangingi lilinunuliwa na kiongozi wa kambi rasimi ya upinzani yeye si alilikuta tu, na ataliacha hapohapo ili Zitto aje atembelee siku atakapo kuwa mwenyekiti wa kambi rasimi ya upinzani.

CHADEMA ni wa laghai katika lipi,kwani wao wamekwambia kuwa wanaamini katika siasa za ujamaa mpaka uwachukie kwa kuwa wanatumia mashangingi ambayo ni sawa na hosptali 4.

Mimi naona utakuwa umepotea njia,mtu wa kumchukia ulitakiwa umchukie yule anae hubiri siasa za ya ujamaa lakini mwenyewe ana miliki magari ya kifahari na mali kadhaa za mabilioni halafu ana taka wenzake waendelee kutembea kwa train ya mjerumani.
 
Zitto vijana wana bet ili kutoka kimaisha wewe unahubiri Ujamaa? Mafisadi wanaitwa wajanja wewe unahubiri Ujamaa? Umeshiba mema ya nchi kwanza halafu unajificha nyuma ya Ujamaa? Hivi mjamaa unamjua au unawaona watanzania hamnazo nini?
Very nyc comment
 
Back
Top Bottom