Zitto: ACT Hatutaki Anasa, Usafiri Wetu Treni!

Zitto: ACT Hatutaki Anasa, Usafiri Wetu Treni!

Boot leeking sioni habari hapo


Wana Ukumbi,

Kama Watanzania tunataka chama cha siasa chenye nidhamu ya matumizi ya pesa, basi ACT ndio chama sahihi!

Zitto ameendelea kuonyesha tabia yake ya kujali raslimali kwa kuzitumia kwa uangalifu mkubwa huku akifikiria wanyonge wa nchi hii ambao wengi wao wako kijijini.

Katika kutekeleza hilo, Zitto ameamua kufanya ziara za chama hicho (kwa awamu ya pili) kwa kutumia treni kwa kuwa itapita maeneo ambayo ACT imeyakusudia kwa awamu ya pili!

Watanzania, matukio haya ambayo tunayoyaona ndani ya ACT ni ukumbusho wa ujamaa wa Mwalimu wakati wa CCM ile ya enzi za azimio la Arusha.


View attachment 246214
 
Join Date : 20th April 2015
Posts : 43
Rep Power : 309
Likes Received46
Likes Given0


Kikosi kazi April brigade
 
Upuuzi mtupu!

Kama mtu ana utajiri wa milioni 600 halafu akasafiri kwa baiskeli au kwa mguu, anafanya hivyo au kwa unafiki au kwa nia ya kuwalaghai wale wasio na uwezo wa kupanda ndege au kutumia magari binafsi ili wajione kama wanafanana naye lakini ukweli hautabadilika kuwa hawa walio wengi hawana kitu, na huyu mmoja ni utajiri wa milioni 600 ambao hataki kuupunguza kuwasaidia hawa wasio nacho. Ambaye ana milioni 600 halafu akazitumia hizo pesa kuwasaidia maskini kiasi cha kumfanya yeye alazimike kusafiri kwa basi kwa sababu hana uwezo tena wa kusafiri kwa ndege, huyo anaweza kuitwa ni mjamaa mzalendo aliyepindukia.

Zito ni muigizaji, mlaghai na mnafiki. Anapanda treni kama maigizo na ghiliba, hapandi treni kwa sababu hana fedha ya kupanda ndege au kutumia gari binafsi. Hapendi treni kwa sababu mali zake zote amezitumia kwaajili ya watu waskini. Ni sawa na EL anapoamua kutembea kwa miguu umbali wa kilometa 4.
 
Hahaha Hujui sanaa ni ngumu kufanya siasa tz ndo maana Wasanii wakijiunga na siasa wanafanikiwa haraka ila zito kuwa makini ACT isije kufilisi
 
Hata delila alimwendea samson kwa maneno matamu lakini siku ya siku samson alilegeza masharti.
 
Unafiki mtupu. Bado tunsmtaka aueleze Imma wa watanzania, ni nani anafadhili hiyo mikutano ya chama chake

chama tunafadhili wenyewe tunachangishana usiku na mchana kama unalingine sema .....!wakati mnasema tunafadhiliwa na ccm wakatu ruzuku wanatoa ccm kwenu sisi tuko kimya ela za ccm ni HARAMU kwa ACT ila ni HALALI KWA CHADEMA SASA HIVI TUMEIJUA JANJA YENU.
 
Zito ni kama Jose Mujica rais wa Uruguay ni mjamaa kwelikweli ni raisi lakini anaishi kijijini kwake na sio ikulu,anatumia public bus kwenda ofisini na train kwenda mikoani so as to minimize cost.Type ya viongozi kama Zito wakiwepo nchini unneccessry expenses kwa govt zitapungua sana,Go Zito go ACT wazalendo tuirudishe nchi kwenye misingi iliyoasisi
 
Picha ya uongo hiyo na alieweka hiyo picha na kwa mapenzi yake na Zitto picha hiyo ni ya kitombo hapo wapo kwenye kiberenge na kamati ya PAC japange upya
 
Picha ya uongo hiyo na alieweka hiyo picha na kwa mapenzi yake na Zitto picha hiyo ni ya kitombo hapo wapo kwenye kiberenge na kamati ya PAC japange upya

MODS yaani mkuu wa chama anadhalilika hivi mko kimya..huyu kasema hii picha ni ya KiTOMBO mnamuangalia tu..piga ban huyuuu
 
Wana Ukumbi,

Kama Watanzania tunataka chama cha siasa chenye nidhamu ya matumizi ya pesa, basi ACT ndio chama sahihi!

Zitto ameendelea kuonyesha tabia yake ya kujali raslimali kwa kuzitumia kwa uangalifu mkubwa huku akifikiria wanyonge wa nchi hii ambao wengi wao wako kijijini.

Katika kutekeleza hilo, Zitto ameamua kufanya ziara za chama hicho (kwa awamu ya pili) kwa kutumia treni kwa kuwa itapita maeneo ambayo ACT imeyakusudia kwa awamu ya pili!

Watanzania, matukio haya ambayo tunayoyaona ndani ya ACT ni ukumbusho wa ujamaa wa Mwalimu wakati wa CCM ile ya enzi za azimio la Arusha.


View attachment 246214

Ulitusaidia nini zaidi ya kutufanya tuwe masikini wa mwisho duniani?
 
Hata angepanda UNGO...bado chadema ni baba lao...na adui yetu namba moja ni CCM na mawakala wake ACT...Wachumia Tumbo...
 
Kuna wenzako walikuwa wakisubiri hivyo hivyo Zitto apokee posho baada ya kutangaza kuwa hatopokea posho za bungeni....hadi leo hii wanaendelea kusubiri na wengine wameona wamuache tu!

Zitto hana tamaa za kipuuzi mkuu. Ni mwanasiasa adimu kuwahi kutokea nchini. Na Watanzania wameliona hilo na ndio maana anaungwa mkono pamoja na majungu yote yanayopigwa na maadui zake ( maana wengine wanatangazq hadharani kabisa)!

Nadhani utakuwa hujanielewa vizuri, sentensi yangu iko very clear! haijajificha jificha! isome vizuri tena kwa mtindo wa kama unatafakari moja ya picha zilizochorwa kwa rangi nyingi! ishu hapa ni muendelezo wa vitendo ama kitendo kilicho/kinacho mfanya mtu au bidhaa ikae sokoni kwa muda na ipendwe/kupendwa na watu. mfano utasikia watu wanasema hivi, "ZAMANI NIDHAMU ILIKUWA NIDHAMU KWELI KWELI SIO SASA" simsemi Zitto ila nahofia kama mtindo wa upigaji drums utabadilika baada ya kuuza albamu kadhaa huenda ukapoteza soko a.k.a Imani kwa wateja. CCM nao wamerudi na mtindo aliokuwa anautumia Baba wa taifa (ila huyu alikuwa haigizi alikuwa anamaanisha) kinana amepanda treni sana tumeona, kinana ambeba hadi ndoo ya maji kichwani tumeona na mengineyo, ila uhalisia wa vitendo hivyo maana yake ni matusi na hadaa kwa wananchi!!?? unapofundisha kwa mifano ni unamaanisha hivyo ndivyo maisha yanavyotakiwa kwenda na watu walielewe somo vizuri, sasa leo umeboba ndoo kichwani kesho wewe unatumia bomba hadi chooni lazima uliye mfundisha kubeba ndoo kichwani atakuona wewe ni mnyonyaji na muongo. hili ni kwa vyama vyote tanzania,hebu kuweni makini na silabasi zenu za kufundishia mnapokutana na sisi wananchi katika madarasa (mikutanoni) ziwe zinaendana na maisha yenu ili tubadilike kwa pamoja.
 
mimi siko mbali na wewe lakini,sioni mahali walipokosea kwani hakuna ubishi kuwa si kweli kuwa watumishi wa serekali hawatembelei magari ya serekali.

Alichokisema dr silaa na mbowe ni kweli kabisa,sasa suala la kuacha kuvitumia ili waendane na kile wanachokisema wanaweza kuachaje wakati serekali iliyopo madarakani ndio inayowataka watumie vitu kama hivyo na serekali yenyewe ndiyo iliyovinunua ili wavitumie kulingana na nafasi zao na hakuna sehemu yoyote ambayo serekali imebainisha wazi kuwa kama hutaki kutumia shangingi basi utumie gari la kiwango fulani.

Na akisha kataa kutumia shangingi lililonunuliwa na serekali kitakachofuata ni kitu gani,kwamba achukue hela zake za mfukoni akanunulie gari analo litaka yeye,na baada ya kununua gari hilo kwa fedha yake serekali italipokea na kuruhusu litumike wakati wadhifa alionao ana takiwa atumie shangingi tena mali ya serekali.

Chadema walichokuwa wanajaribu kukifanya hapa ni kuishauri serekali iachane na maisha ya anasa ili fedha ambazo zinatumika kununulia mashangingi ziweze kutumika kwenye huduma za kijamii na hakuna mahali popote walipojifunga kuishi tofauti na maisha ya serekali iliyopo madarakani.

Kama serekali ingekubali ushauri wao ina maana kuwa isingeweza kununua mashangingi yanayotumika hivi sasa hivyo mwenyekiti wa kambi rasimi ya upinzani angejikuta moja kwa moja ana tumia gari tofauti na shangingi kwa kuwa ndilo lililokuwepo.

Kumtaka mwenyekiti wa kambi rasimi kuacha kutumia shangingi kwa kuwa ana amini kuwa ni gari ya anasa ni sawa na kusema kuwa asilipe ada ya shule kwani yeye na chama chake wanaamini kuwa elimu ya bure inawezakana wakati serekali iliyopo madarakani inataka walipe ada.

Mlagai na muongo ni yule ambaye ametangaza waziwazi kuwa ameamuwa kufuata siasa za ujamaa lakini haishi katika maisha kama hayo.

Aliye sema kuwa kuna wakubwa wameficha fedha uswiss walipomtaka athibitishe akashindwa kuthibitisha,wakamwambia kuwa kwa kuwa umeshindwa kuthibitisha basi wewe ni muongo,chukukua karatasi uandike kuwa mimi ni muongo na uweke sahihi yako na yeye akakubali kuandika na kuweka sahihi kuthibitisha kuwa yeye ni muongo.

Mtu wa aina hii ndiye muongo na mlaghai asiyefaa katika jamii na sioni adhabu itakayomfaa hapa duniani labda kwa mungu ndiko anako weza kupata adhabu yake sitahiki.

hakika umenena vyema.
 
Siku chache zijazo huyu mtu ataokota makopo,ZZK hayuko sawa kisaikolojia hata ukimwangalia tu jukwaani
 
Wana Ukumbi,

Kama Watanzania tunataka chama cha siasa chenye nidhamu ya matumizi ya pesa, basi ACT ndio chama sahihi!

Zitto ameendelea kuonyesha tabia yake ya kujali raslimali kwa kuzitumia kwa uangalifu mkubwa huku akifikiria wanyonge wa nchi hii ambao wengi wao wako kijijini.

Katika kutekeleza hilo, Zitto ameamua kufanya ziara za chama hicho (kwa awamu ya pili) kwa kutumia treni kwa kuwa itapita maeneo ambayo ACT imeyakusudia kwa awamu ya pili!

Watanzania, matukio haya ambayo tunayoyaona ndani ya ACT ni ukumbusho wa ujamaa wa Mwalimu wakati wa CCM ile ya enzi za azimio la Arusha.


View attachment 246214

Ni kawaida na dalili ya wapenda madaraka kiongozi anaweza hata kusafiria gubi la kuti la mnazi ili ajifanye anapenda wanyonge lakini akiishika dola ndo kwanza atasema lazima Rais awe na ndege yake
 
Back
Top Bottom