Zitto: ACT Hatutaki Anasa, Usafiri Wetu Treni!

Zitto: ACT Hatutaki Anasa, Usafiri Wetu Treni!

Waswahili walisema, Kazi ni kazi, mradi mkono uende kinywani!

Facts za mleta mada!



  • Join Date : 20th April 2015
    Posts : 55
    Rep Power : 312
    Likes Received52
    Likes Given0


 
mwitkio n mdogo sana mh,ndo maana anapopga mkutano akiondoka anaondoka na kachama kake,ila kuna usanii unaofanyka magamba wanampa watu wa kumshanglia kla atakapopga mkutano sasa watu ambao hawajui wakiona amejaza watu anashangliwa wanajua anakubalika.alafu kitu kngne n hiv jamaa anapoitsha mkutano wanachama wa ukawa wanaenda kwa wing pamoja na wanachama wa ccm ambao wao huwa wameenda kimkakat kwa ajl ya kumshabkia tu.ila wale wa ukawa huwa wanaenda kwa ajl ya kumshangaa na kumckilza amekuja na lip.UKAWA bado tuko imara
 
Kuna wenzako walikuwa wakisubiri hivyo hivyo Zitto apokee posho baada ya kutangaza kuwa hatopokea posho za bungeni....hadi leo hii wanaendelea kusubiri na wengine wameona wamuache tu!

Zitto hana tamaa za kipuuzi mkuu. Ni mwanasiasa adimu kuwahi kutokea nchini. Na Watanzania wameliona hilo na ndio maana anaungwa mkono pamoja na majungu yote yanayopigwa na maadui zake ( maana wengine wanatangazq hadharani kabisa)!

Kutokupomea posho nao ni ujamaa?Kwangu mimi naona ni Upumbavu wa Kupindukia.Atueleze faida iliyopatikana kwa yeye kutokupokea hizo posho!Upumbavu at the Best level.
Hizo Posho angewasomeshea watoto wa Kigoma Kaskazini wanaokosa Ada shuleni,Angeboresha vituo vya Afya jimboni kwake,ama lah!angepeleka ikawe sadaka msikitini na Mungu angemzidishia zaidi na zaidi! Mtuambie sasa ninyi wenye akili za Kiroboto,Posho alizozikataa Zitto zilifanyiwa nini?Au zilikuwa allocated wapi?Je!Alikataa na mshahara wa Ubunge?kama hapana ni kwa nini hakufanya hivyo?
Mbona hakuwahi kukataa Posho za Mifuko ya Jamii kila alipoattend mikutano yao?
Mbona hakuwahi kukataa hela za TISS? Mbona hakuwahi kuzikataa hela walizojigeizia ni za Kwao yeye na Wenzake,fedha za IPTL kila mwezi kabla ya Muhongo kukata hiyo pipe? Watu wana mafile ya Zitto ila kwa kuwa hamumfahamu,endeleeni kumwita Mjamaa,ingawa hamjatueleza huu Ujamaa ni wa Tangu Kitambo au Kaununua juzi baada ya kutoka cdm?
 
Zitto danganya toto, hatakama amelelewa na Chadema hana tofauti na kinyonga.
 
chama tunafadhili wenyewe tunachangishana usiku na mchana kama unalingine sema .....!wakati mnasema tunafadhiliwa na ccm wakatu ruzuku wanatoa ccm kwenu sisi tuko kimya ela za ccm ni HARAMU kwa ACT ila ni HALALI KWA CHADEMA SASA HIVI TUMEIJUA JANJA YENU.

Ruzuku haijawahi kuwa Fedha ya ccm.Ni juha peke yake ndiye atakayedhani ruzuku ni fedha toka ccm,haiwezekani na wao wawe wanapokea ruzuku ilihali wanatoa,wana fursa ya kufanya moja tu. Sasa act wanapokea ruzuku toka wapi?kwa misingi gani?hiyo fedha mnayochangishana mbona hatuoni mkichangishana?au mnachangishania KUZIMU? Anyway,mnachangishana ndani ya ofisi za Lumumba!
 
ACT ni jeshi la mtu mmoja. Haina tofauti na NCCR ya Mrema. Hiki ni chama ambacho kimeshindwa kujenga base, na kubaki kujiuza kwa kupitia jina la Zitto tu. Hakuna namna unaweza kwenda kumshawishi mtu ahudhurie mkutano wa ACT pasipo kumtaja Zitto. Na yumkini walio wengi wanakuja kwenye mikutano kwa nia tu ya kutaka kumfahamu Zitto na si lingine.

Ninaogopa kuwashauri mashabiki wa Zitto msije mkanirushia mawe. But kwa uhakika kabisa, sioni cha maana ambacho anakifanya Zitto kinachomtofautisha na wapinzani wengine. Zaidi sana, ni ukweli kuwa ACT inabebwa na jina la kiongozi wake na si sera zake. Hakuna mtu yeyote atakayevutiwa na hadithi ya sera za ujamaa hii leo, itikadi ambazo zilishindwa kufanya kazi mahali pote duniani. Kusema ukweli sioni lolote la maana zaidi ya blabla tu.

Kwa hiyo zitto kama zitto anakubalika? Waliosema hana madhara?mezeni tu japo ya moto
 
Kama ujamaa unapimwa kwa aina ya usafiri,basi mheshimiwa Prof Lipumba ni mjamaa&mzalendo haswaa!
Kwani yeye amekuwa akitumia tela la punda mara kadhaa hasa ktk kampeni za uchaguzi mdogo-Igunga.
Jipange upya we mnafiki wa ACT.

😂😂😂😂😂 ajhahahahahahahahahagagagagaga
 
kumbe kutumia usafiri wa treni ndo uzalendo mwaka huu tutashuhidia mengi sana . 481.jpg
 
Wana Ukumbi,

Kama Watanzania tunataka chama cha siasa chenye nidhamu ya matumizi ya pesa, basi ACT ndio chama sahihi!

Zitto ameendelea kuonyesha tabia yake ya kujali raslimali kwa kuzitumia kwa uangalifu mkubwa huku akifikiria wanyonge wa nchi hii ambao wengi wao wako kijijini.

Katika kutekeleza hilo, Zitto ameamua kufanya ziara za chama hicho (kwa awamu ya pili) kwa kutumia treni kwa kuwa itapita maeneo ambayo ACT imeyakusudia kwa awamu ya pili!

Watanzania, matukio haya ambayo tunayoyaona ndani ya ACT ni ukumbusho wa ujamaa wa Mwalimu wakati wa CCM ile ya enzi za azimio la Arusha.


View attachment 246214
mbona alipokuwa chadema hakuwahi kufanya hivyo hizi mbwebwe tuu zina mwisho wake
 
Kutoka kupanda ndege za TANAPA yeye na kimada wake hadi kupanda treni sio kazi ndogo ..........na ataanza kulala guest na sio hotelini .........usitukane mamba kabla ya kuvuka mto , unawasaliti watanzania unafikiri utaendelea kuwasalama kweli?
 
Kwa hiyo zitto kama zitto anakubalika? Waliosema hana madhara?mezeni tu japo ya moto
Hakuna anayebeza ukweli kwamba Zitto ana popularity kubwa, na hata attention aliyokuwa anaitengeneza ndani ya CHADEMA ilikuwa ni kwaajili ya kutafuta hiyo popularity. Ni ukweli usiopingika kwamba tangu baada ya tukio la Buzwagi Zitto aligain umaarufu mkubwa, na umaarufu huo ulimpa kiburi kiasi cha kujiona yeye ni kila kitu ndani ya CHADEMA, na kwamba bila yeye CHADEMA haiwezi kusimama. Kwa kiburi hicho, akajiona anafaa kuwa Rais, akajiona anafaa kuwa mwenyekiti wa chama, akatamani kila cheo kilicho kikubwa zaidi hapa duniani, naamini atakuwa alitamani pia kuwa Rais wa dunia.
Hata CHADEMA wanajua wazi kwamba Zitto ni popular, japo sina uhakika kama anakubalika. Lakini upopular wake kama ungebaki ndani ya CHADEMA kwa kiburi kile alichokuwa nacho kiasi cha kuanzisha kikundi cha akina Mchange, Mwamtela etc kwa ajili ya kuwachafua viongozi wa CHADEMA mitandaoni ili tu yeye akubalike katika nafasi ya uenyekiti, kwa hakika chama kingekufa. Hao watu wasio na msimamo ambao watatoka ndani ya CHADEMA kumfuata Zitto hivi sasa, hawana madhara makubwa kwa chama kama ambavyo Zitto angebaki ndani ya CHADEMA.
 
Wana Ukumbi,

Kama Watanzania tunataka chama cha siasa chenye nidhamu ya matumizi ya pesa, basi ACT ndio chama sahihi!

Zitto ameendelea kuonyesha tabia yake ya kujali raslimali kwa kuzitumia kwa uangalifu mkubwa huku akifikiria wanyonge wa nchi hii ambao wengi wao wako kijijini.

Katika kutekeleza hilo, Zitto ameamua kufanya ziara za chama hicho (kwa awamu ya pili) kwa kutumia treni kwa kuwa itapita maeneo ambayo ACT imeyakusudia kwa awamu ya pili!

Watanzania, matukio haya ambayo tunayoyaona ndani ya ACT ni ukumbusho wa ujamaa wa Mwalimu wakati wa CCM ile ya enzi za azimio la Arusha.


View attachment 246214
Angalieni profile ya mleta mada ya kupromote ACT na supreme leader wao

attachment.php


Eti hawa wanaunga mkono harakati za Zitto za kuitoa CCM madarakani!!!???

Ulaghai, uongo wa wazi!!!
 

Attachments

  • hamy.PNG
    hamy.PNG
    29.8 KB · Views: 116
Back
Top Bottom