Zitto achukua fomu Kigoma mjini

Zitto achukua fomu Kigoma mjini

binafsi nampongeza kwa kwenda kwenye jimbo linaloongozwa na ccm. lakini najiuliza je ni kweli kigoma kaskazini hakuna matatizo? ni swali linalopaswa kujibiwa na zitto pamoja na wana kigoma kaskazini wenyewe.
 
Aaaaa nashangaaa sana kwa wanaomfananisha Zitto na mnyika,mnyika ni Wa kawaida sana kwa Zitto,Zitto ni zaidi hata ya chairman
 
Zitto kaenda kupambana kwenye jimbo la CCM angeenda kugombea kwenye jimbo la upinzani tungesikia lawama nyingi tu Zitto anauwa upinzani.

Dollar imewashika mmeshindwa kuikwamua,mlipochukua nchi kwa chinga deni lilikuwa dogo leo Trillion 39,000/- ccm hovyo
 
Aaaaa nashangaaa sana kwa wanaomfananisha Zitto na mnyika,mnyika ni Wa kawaida sana kwa Zitto,Zitto ni zaidi hata ya chairman
Mbona kakimbia Ubungo?

Alijidai wanaUbungo wanamtaka?
 
zitto.jpg

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT, Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Picha ya Maktaba.

Kigoma. Safari ya mbunge wa zamani wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe kurejea bungeni imeanza rasmi baada ya kiongozi huyo wa chama kipya cha ACT-Wazalendo kuchukua fomu za kuwania kuongoza jimbo la Kigoma Mjini.

Uamuzi huo wa kulitaka jimbo hilo unathibitisha kauli zake ambazo amekuwa akizitoa kwa muda mrefu kuwa hatarudi tena Kigoma Kaskazini kwa kuwa alishawatimizia kila kitu na haoni sababu za kuwawakilisha tena wananchi wa eneo hilo.

Kauli yake iliibua ubashiri kuwa Zitto anataka kubadilishana jimbo na mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba, uvumi ambao aliukanusha akisema hadhani kama CCM inaweza kupata jimbo Kigoma.

Zitto, ambaye alijiondoa Chadema baada ya kukiuka katiba kwa kufungua mashtaka dhidi ya chama hicho, hakufanya mbwembwe wakati akienda kuchukua fomu kwenye ofisi za ACT Ujiji jana, badala yake aliita viongozi wa kata na matawi bila ya kutaarifu vyombo vya habari.

“Nimeamua kugombea ubunge wa Kigoma Mjini ili niwatumikie ndugu zangu ambao wamekuwa wakipata tabu katika kupigania haki zao za msingi ambazo walistahili kuzipata kama ilivyo katika mikoa mingine,” alisema Zitto alipoongea na mwandishi wa Mwananchi kwa simu.

“Nitakapokuwa mbunge wa Kigoma Mjini nitahakikisha barabara za mitaani zinapitika katika kipindi chote cha mwaka, nitahakikisha watu wanaacha tabia ya kulima mashamba katikati ya mitaa na makazi, lakini nitahakikisha kila mmoja anajiunga na mifuko ya kijamii ili kujiwekea akiba ya uzeeni pamoja na kupata huduma ya matibabu, elimu na nyinginezo zinazopatikana kwa kutumia mifuko hiyo.”

Mwenyekiti huyo wa zamani wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema bonde la Mto Luiche bado halijatumika ipasavyo kuzalisha chakula kwa wingi.

“Nakusudia kuibana Serikali ijenge skimu ya umwagiliaji maji ili wakulima walime kilimo cha mpunga kwa mwaka mzima bila kupumzika, jambo ambalo litainua uchumi wa wakulima na kuongeza chakula hapa Kigoma,” alisema.

Kuhusu umeme wa gridi ya Taifa, Zitto alisema lazima upatikane ili kusaidia jitihada ya ujenzi wa viwanda vya kusindika mazao ya uvuvi na kilimo kwa kuwa hivi sasa mji wa Kigoma Ujiji unategemea umeme wa jenereta ambao hauwezi kuendesha shughuli za viwanda, hali inayochangia mkoa kuendelea kuwa masikini licha ya kuzungukwa na rasilimali nyingi.

Katibu wa ACT wa Jimbo la Kigoma Mjini, Azizi Ally alisema Zitto alichukua fomu hiyo jana kwa malipo ya Sh100,000 mbele ya viongozi 72 wa kata na matawi kutoka jimboni humo.

“Kwa hali ya sasa Kigoma Mjini inahitaji kupata mbunge anayeweza kufuatilia mambo kwa kina ili kuleta maendeleo ya wananchi baadala ya yule anayekwenda bungeni kujifunza,” alisema Ally.

“Watu wanakabiliwa na kero mbalimbali kama ubovu wa barabara za mitaani, uhaba wa umeme wa uhakika unaoweza kuendesha viwanda vikubwa na vidogo, pamoja na wengi kufanya kilimo cha kujikimu zaidi.“ Zitto alitofautiana na uongozi wa juu wa Chadema uliomtuhumu kuwa alikuwa amefanya uasi na kwamba alishaanzisha chama kingine akiwa ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani na kusababisha avuliwe nyadhifa zote, ikiwamo ya unaibu katibu mkuu.
Hata hivyo, wakati Chadema ikijiandaa kumjadili na pengine kumvua uanachama, Zitto alifungua kesi akitaka mahakama imuamuru katibu mkuu wa Chadema ampe nyaraka za mwenendo wa vikao vilivyomvua madaraka na kuomba amri ya kuzuia vikao hivyo visimjadili.

Katika hukumu ya kesi hiyo, mahakama ilitupilia mbali hoja zake, uamuzi uliotafsiriwa kuwa umefungua njia ya kutimuliwa kwake kwa kitendo cha kufungua kesi mahakamani kinyume cha katiba.

Mkazi wa Gungu mjini Kigoma, Zuberi Mrisho alisema ujio za Zitto kugombea Ubunge wa jimbo hilo utaamsha ari ya wananchi kujiandikisha kwa wingi katika Daftari la Wapigakura na kujitokeza kupiga kura tofauti na chaguzi zilizopita.

“Mwaka 2010 Vijana wengi hatukupiga kura hapa kwa sababu tulikosa imani na baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali, lakini kwa ujio wa Zitto sasa nina hakika wengi tutajitokeza kupiga kura ili tupate viongozi makini kwa maslahi ya mji wetu,’ alisema Mrisho.chanzo.Zitto apiga tambo kuelekea bungeni - Kitaifa

Zitto bungeni kama nyumbani vile. kama anagombea kgm mjini bas biashara imeisha.
 
Msaka tonge tu huyo anasemaje ametimiza kila kitu kinachohitajika na wananchi wa jimbo la kigoma kaskazini ili hali wananchi wengi bado wanashida ya kiuchumi na matatizo kibao, atueleze ni kitu gani anatafuta maana sisi tulimkataa kwa kutukimbia na kujionyesha siku hizi za uchaguzi na vimisaada vya ajabu ajabu tu. Tutaondoka wananchi wote wa kigoma kaskazini tukawwambie wa mjini jinsi gani huyu jamaa alivyo na mdomo mtamu ila vitendo ni poor. Asitudanganye
 
Kumbe Kigoma kaskazini hawahitaji tena Mbunge, yaani walishatimiziwa kila kitu!

Tanzania is the greatest nation in the world!
 
Napenda kumnukuu Ben Saanane "Ikifika wakati wabunge wanabadilishana majimbo basi ni disaster".Zito Kabwe ametajwa kubadilishana jimbo na mbunge wa Kigoma mjini Mh.Peter Serukamba.Hata hivi juzi kati iliripotiwa kuwa Zito amechukua form ACT ili awe mgombea ubunge.Hivi wakuu ni lini "mpinzani" huyu amewahi kueleza sababu ya kubadili7hana majimbo?huu sio usaliti kwa wana Kigoma Kaskazini?Zitto ona aibu mkuu,tamaa hizo
 
Last edited by a moderator:
Una Ushahidi wa hayo unayonena?...au na wewe unaanzisha mada ili ionekane na wewe umeanzisha mada?
 
ana take chance ya kuwa maarufu anashindwa kutumia opportunity labda hana washauri wazuri au ni mjeuri na mbishi akishauriwa hataki,kujijenga kisiasa inachukua miaka kujimaliza inachukua siku chache sana
 
KAHAMA hatutaki MAMLUKI bora aende hukohuko kwao.
Hawa uwa wanachekesha sana kwao Zitto ana jema, angeenda kugombea Kahama wangesema kakimbia kwao mwingine anasema kamkimbia Mnyika Ubungo wakati Mnyika mwenyewe kurudi bungeni miujiza.
 
Last edited by a moderator:
.... Kwa Anayejua Au Zzk Mwenyewe Naomba Atufahamishe Kwanin Ameamua Kuchepukia Kigoma Mjini..
 
Kasoma alama za nyakati kule angepigwa chini maana hajafanya lolote kule.
 
Zitto ni mdini kama wadini wengine, kilichomkimbiza Kigoma Kaskazini ni udini tu, anashinda misikitini kwa wazee wa ujiji, gungu na buzebazeba ili wamsaidie kumpigia kampeni.
tena wamebadilishana na Serukamba kwa miadi kua CCM italeta mgombea dhaifu Kigoma Mjini ili ZZK apite kirahisi.
 
Back
Top Bottom