Zitto achukua fomu Kigoma mjini

Zitto achukua fomu Kigoma mjini

Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema anakusudia kuwa mbunge wa Kigoma Mjini kwa kipindi kimoja cha miaka mitano kuanzia 2015 hadi 2020, kabla ya kuomba kazi nyingine ya kufanya kwa Watanzania.

Mbunge wa Jimbo hilokwa sasa ni Peter Serukamba wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza baada ya kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakurakatika Kituo cha OTTU Mwanga Mjini Kigoma juzi, Zitto alisema ana dhamira ya kuhakikisha ACT inashinda majimbo yote manane katika Uchaguzi Mkuu mkoani hapa. "Tumejipanga vizuri kushinda majimbo yote ya Mkoa wa Kigoma, lakini tuna uhakika wa kupata nusu ya majimbo mkoani Tabora na lazima tupate majimbo yote ya Kahama.

Tumejipangavizuri kushinda bila shaka baada ya Oktoba 25 watu watajua hiki tunachokisema leo," alisema Zitto.

Alisema baada ya kuhakikisha Kigoma Mjini inanufaika na miradi ya barabara,Uwanja cha Ndege, ujenzi wa Bandari kavu ya Katosho na Kibirizi wakati huo akiwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kwa sasa anakusudia kupigania upatikanaji wa umeme wa maji kutoka Mto Malagarasi."Kigoma ni mji wa biashara, lazima eneo la Bandari ya Kigoma liwe la kimkakati kwa sababu tunakusudia kuifanya Kigoma kuwa eneo maalumu la biashara kwa ukanda huu wa MaziwaMakuu, mikakati imeandaliwa tayari."Lakini hili litafanikiwa ikiwa tutapata umeme wa uhakika badala ya huu wa kutegemea mafuta ambao ni ghali kuuendesha," alisema.

Kuhusu gharama kubwa ya umeme, Zitto alisema: "Kila mwezi Tanesco wanatumia Sh2 bilioni kuzalisha umeme Kigoma lakini wanakusanya Sh300 milioni kwa mwezi, sawa na roboya gharama halisi za uendeshaji, lazimatupiganie umeme wa Malagarasi utakaozalisha megawati 48 zitakazowezesha kuendesha viwanda vikubwa na vidogo vya kuzalisha na kuchakata mazao mbalimbali."

Hata hivyo, Zitto hakutaka kuzungumzia kwa undani maelezo yakekwamba atakuwa mbunge kwa kipindi kimoja ili itakapofika 2020 aombe kazi nyingine kwa Watanzania.

Zitto huku akicheka alijibu: "Tusubiri kwanza watu wachukue fomu za kugombea urais, haya mengine tutazungumza tu kwani muda bado upo, lakini nitawaomba Watanzania wanipe kazi nyingine niwatumikie."Katibu wa ACT Wilaya ya Kigoma Mjini, Azizi Ally alisema kuna changamoto zinazowakabili hususan ugumu wa baadhi ya watu kuandikishwa kutokana na wingi wao na uchache wa mashine.

Alisema watu wengi wamekata tamaa na wameamua kususia kazi hiyo.

Mkazi wa Kisangani Mwanga, mjini Kigoma, Monica Abel alisema ujio wa Zitto utaongeza ushindani kwa wagombea kutoka vyama vingine na kuwataka watu kujitokeza kujiandikishaili waweze kuchagua viongozi wanaowataka.

Chanzo: Mwananchi
 
Aisee..... Action speaks louder than words Zitto. Ungekaa kimya tu manake kwa haya ya majimbo yote kahama na kigoma na nusu ya Tabora isipotokea hivyo sijui utajisikiaje na hizi tambo. Weka akiba ya maneno and let the actions speak louder than words...
C:C BAK, Molemo Mungi ZeMarcopolo Ritz sweetlady
 
Last edited by a moderator:

kinachompa kiburi ni kuwa hayo majimbo kuna Waha
 
Last edited by a moderator:
Aisee..... Action speaks louder than words Zitto. Ungekaa kimya tu manake kwa haya ya majimbo yote kahama na kigoma na nusu ya Tabora isipotokea hivyo sijui utajisikiaje na hizi tambo. Weka akiba ya maneno and let the actions speak louder than words...
C:C BAK, Molemo Mungi ZeMarcopolo Ritz sweetlady

That is politics mammie.
Confidence wins a day...
 
Last edited by a moderator:
huyu jamaa anawadharau sana wanakigoma. anawageuza kama vitumbua.
 
Dr that is the main problem with this fella. He don't know when to open his mouth wide open or to shut up.

Aisee..... Action speaks louder than words Zitto. Ungekaa kimya tu manake kwa haya ya majimbo yote kahama na kigoma na nusu ya Tabora isipotokea hivyo sijui utajisikiaje na hizi tambo. Weka akiba ya maneno and let the actions speak louder than words...
C:C BAK, Molemo Mungi ZeMarcopolo Ritz sweetlady
 
Zitto na ACT wazalendo yake kumbe yupo? Ziara zake za kuinadi ACT zimeishia wapi???
 
Msaliti kaongea leo.. Mbwembwe kibao

Kuna watu wataondoka ccm baada ya uteuzi wa mgombea urais hawa ndio wamefanya mazungumzo naye kwa ajili ya kuunda ccm b ambayo itakuwa na kazi ya kupambana na UKAWA na wapinzani wao ndani ya ccm
Itatengenezwa colabo moja ya mafisadi ambayo itafanya kila liwezekanalo ipate wabunge wengi. Ni kilinge cha wahuni wezi na wababaishaji ambao wanataka kulinda maslahi yao na walio nyuma yao
Kati yao hao ni wagombea urais ambao wamejiandaa na mapesa mengi lakini wakakosa urais hivyo kupeleka nguvu kwenye ubunge na udiwani....!ndio maana unaona dogo kaja kwa mbwembwe kibao
 
Zitto kawafanya wanakigoma wote ni kama mazuzu na wakimpa ubunge ndiyo atazidi kuwadbarau kabisa pamoja na Serukamba wao.
 
Kuna watu wataondoka ccm baada ya uteuzi wa mgombea urais hawa ndio wamefanya mazungumzo naye kwa ajili ya kuunda ccm b ambayo itakuwa na kazi ya kupambana na UKAWA na wapinzani wao ndani ya ccm
Itatengenezwa colabo moja ya mafisadi ambayo itafanya kila liwezekanalo ipate wabunge wengi. Ni kilinge cha wahuni wezi na wababaishaji ambao wanataka kulinda maslahi yao na walio nyuma yao
Kati yao hao ni wagombea urais ambao wamejiandaa na mapesa mengi lakini wakakosa urais hivyo kupeleka nguvu kwenye ubunge na udiwani....!ndio maana unaona dogo kaja kwa mbwembwe kibao
UKAWA watafanyiwa vurugu sana Kigoma mjini, lakini ni moja ya majimbo wanayopaswa kuweka nguvu kubwa sana na kulinda kura kadri iwezekanavyo. act kuwapokea hawa wezi toka ccm itakuwa jambo jema kwa UKAWA.
 
nitashangaa sana kama wanakigoma watampa jimbo zitto kabwe. maana haeleweki anasimamia nini...
 
Back
Top Bottom