Zitto aamua liwalo na liwe juu ya mabilioni yaliyofichwa nje ya nchi

Status
Not open for further replies.
Mh Zitto mbunge kigoma kaskazini NITAJIBU MAPIGO YA WEREMA. Mbunge wa Kigoma kaskazini Zitto (chadema) amesema atamjibu mwanasheria mkuu wa serikali, Jaji Fredrick Werema juu ya kauli aliyoisema bungeni kwamba mbunge huyo hana majina ya watanzania waliyoficha mabilioni Uswis.

Zitto alisema kwa kuwa Jaji Werema alimshambulia kupitia bunge naye atatoa majibu bungeni ili ukweli uweze kubainika. Nilimsikia mwanasheria mkuu wa serikali akinishambulia! Nitakachokifanya ni kwamba wiki ijayo nitamjibu hapa bungeni baada ya kumuomba spika anipe nafasi ya kuwasilisha maelezo binafsi alisema Zitto.

Mwanasheria mkuu ni muongo nasema totally ni muongo kwa sababu nimehudhuria maranne na nikawakabidhi majina ya watuhumiwa. Tena kibaya zaidi niliwakabidhi hadi jina la Mchungaji wa kimataifa ambaye angeweza kuwasaidia ktk uchunguzi wao alisema zitto.

SEHEMU NYINGINE KANUKULIWA AKISEMA;

"Nimeamua suala hili nilizungumzie ndani ya bunge, kwahiyo tayari nimewasilisha maelezo yangu kwenye ofisi ya bunge, na wameniambia kuwa nitapangiwa kuwasilisha maelezo hayo wiki ijayo, kila kitu nitabainisha siku hiyo. sina zaidi"

Chanzo ni gazeti la rai

WADAU TUSUBIRI SUALA HILI ILI TUZIJUE MBIVU NA MBICHI.

Hayo majina tutayasubiri hadi karne ziishe....yetu mackio na macho
 
...agenda za zito siku zote its about me,me,me and i,i only. singo hii anakuja nayo iliwamuokoe kwenye wimbi la kutoswa na chama aonekane mzalendo na chama kimemuonea, anapigwa chini tu,...!
 
Hivi kaka umeisoma post yote?? Maana hilo la kukiri lilifanyika kitambo saana hata bado hajaenda Uswis. Je, mpaka sasa hana hayo majina!!! Pia kumbuka kuwa nayo ni suala moja na kuwa na vithibitisho ni suala lingine.
Sasa kama alikiri chini ya kiapo kabla na baadae akayapata si angewasiliana na wenyewe...
 
Nilidhani ataongelea Serena Hotel kama kawaida yake, au UVCCM wamemtema nao maana ndio wanaomuandalia mikutano pale Serena.

Sisi hapa Mwanza tunaelekea viwanja vya Furahisha kumsikiliza mwenyekiti...

mtanange utaanza saa ngapi?
 
Hivi waswahili mnajua maana ya kiapo cha kisheria?


Acheni kubebewa akili, nawahakikishia kwamjibu wa kiapo cha Zitto kilichopo kisheria, hata leo hii akaamua kutaja kinachoitwa majina na akaunti za watanzania waliohifadhi fedha Uswisi na kwingineko, serikali haitashugulikia majina hayo, zaidi atakuwa anajifurahisha tu Zitto,

Kibaya zaidi nikuwa sasa Zitto atafikishwa mahakamani kwa yeye kumtaja binadamu yeyote katika jamhuri ya Wadanganyika,

Zitto anahitaji mshauri makini, hawa vichwa maji akina Msando watasababishwa apotee kabisa kisia na kimaisha,
 
Mh. ZZK wewe ni mkomavu katika siasa na mwenye uwezo mkubwa kujenga hoja na usiyekurupuka kutoa mbambo yasiyo ya kweli, Watanzania tunasubiri kwa hamu majibu yako na ukweli utaubainisha bila shida.

ZZK hana uwezo wa kujenga hoja kama unavyofikiria, magamba walikuwa wanampa support kwenye hoja zake, ngoja wamgeuke uone alivyo mweupe. Na nnaona wameanza kumgeuka, huyu jamaa lazima aonekane kituko tu, just wait and see.
 
Kimsingi sijaona sehemu ametamka kuwa atataja majina, instead amesema atamjibu AG, kwenye kumjibu AG sidhani kama atataja hata jina moja la mwenye A/C Uswisi!

zaidi atajibu kuwa hajawahi kula kiapo ambacho AG amelieleza bunge then hoja mama itazimwa itabaki hoja ya AG kalidanganya Bunge na game itakuwa ishageuzwa kwa mtindo huo.

Na hicho ndicho kitakuwa kiitanzi chake!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom