Zitto aamua liwalo na liwe juu ya mabilioni yaliyofichwa nje ya nchi

Status
Not open for further replies.

talentbrain

JF-Expert Member
Oct 5, 2009
1,188
759
Mh Zitto mbunge kigoma kaskazini NITAJIBU MAPIGO YA WEREMA. Mbunge wa Kigoma kaskazini Zitto (chadema) amesema atamjibu mwanasheria mkuu wa serikali, Jaji Fredrick Werema juu ya kauli aliyoisema bungeni kwamba mbunge huyo hana majina ya watanzania waliyoficha mabilioni Uswis.

Zitto alisema kwa kuwa Jaji Werema alimshambulia kupitia bunge naye atatoa majibu bungeni ili ukweli uweze kubainika. Nilimsikia mwanasheria mkuu wa serikali akinishambulia! Nitakachokifanya ni kwamba wiki ijayo nitamjibu hapa bungeni baada ya kumuomba spika anipe nafasi ya kuwasilisha maelezo binafsi alisema Zitto.

Mwanasheria mkuu ni muongo nasema totally ni muongo kwa sababu nimehudhuria maranne na nikawakabidhi majina ya watuhumiwa. Tena kibaya zaidi niliwakabidhi hadi jina la Mchungaji wa kimataifa ambaye angeweza kuwasaidia ktk uchunguzi wao alisema zitto.

SEHEMU NYINGINE KANUKULIWA AKISEMA;

"Nimeamua suala hili nilizungumzie ndani ya bunge, kwahiyo tayari nimewasilisha maelezo yangu kwenye ofisi ya bunge, na wameniambia kuwa nitapangiwa kuwasilisha maelezo hayo wiki ijayo, kila kitu nitabainisha siku hiyo. sina zaidi"

Chanzo ni gazeti la rai

WADAU TUSUBIRI SUALA HILI ILI TUZIJUE MBIVU NA MBICHI.

#########
Zitto-Kabwe.jpg
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, amesema anatarajia kuwasilisha maelezo binafsi kuhusu, kauli ya Mwanasheria Mkuu aliyoitoa juzi bungeni dhidi yake na kumuita muongo kuhusu suala la kuwa na orodha ya watu wanaodaiwa kuficha fedha nje ya nchi.

Zitto, aliyasema hayo bungeni juzi, ikiwa ni siku moja tu baada ya Mwanasheria Mkuu (AG), Jaji Frederick Werema, kudai mbele ya Bunge kuwa Serikali inashughulikia kisheria suala la Zitto kudanganya Bunge na Kamati kuhusu majina ya watu walioficha mabilioni ya fedha Uswisi.

Akizungumzia sakata hilo, Zitto alisema kwa sasa hataki kuzungumzia suala hilo, ila ukweli wote ataubainisha kwenye maelezo yake binafsi ambayo atayawasilisha wiki ijayo kwenye mkutano wa 14 wa Bunge unaoendelea.

"Nimeamua hili suala nilizungumzie ndani ya Bunge, kwa hiyo tayari nimewasilisha maelezo yangu kwenye Ofisi ya Bunge, na wameniambia kuwa nitapangiwa kuwasilisha maelezo hayo wiki ijayo, kila kitu nitakibainisha siku hiyo, sina zaidi," alisisitiza Zitto.

Wakati akitoa majumuisho ya mjadala wa taarifa zilizowasilishwa bungeni juzi, ambazo ni taarifa ya Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Werema alisema katika suala hilo, Zitto amezidi kuwa mzito.

AG huyo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kuchunguza madai ya mabilioni hayo amesema ili kumalizia uchunguzi wa fedha hizo ameomba Spika wa Bunge kuongezea kamati hiyo miezi sita.

Werema alisema alishangaa kitendo cha Zitto kutaka suala hilo liangalie mfumo na siyo majina ya watu walioficha mabilioni hayo. Alisema awali yeye alishauri kuangalia mfumo wa uwekaji wa fedha hizo, lakini Zitto alikataa na kusema anataka kutoa dukuduku kwa kutaja majina ya watu walioficha fedha hizo.

Alisema mwezi Februari Kamati ilikutana na Zitto na kuwaeleza kuwa ana taarifa na nyaraka na kutoa masharti lakini aliondoka kwenda katika kambi ya Jeshi ambako Kamati ilimfuata lakini bado aliwataka kukutana Dar es Salaam.

Alisema Mei mwaka huu hadi aliposema hakuwa na jina wala akaunti ya mtu yeyote ambaye ana akaunti nje ya nchi kwa kiapo maalumu.

"Jambo la kushangaza ni leo kudai Serikali haina dhamira na suala la walioficha fedha Uswisi? Kwa kweli Zitto Kabwe ni mzigo na sasa tunaingia kufanya kazi hiyo ya uchunguzi kama Serikali kwa kutafuta taarifa bila kumuonea mtu," alisema Werema.


--Habari Leo
 
Nilidhani ataongelea Serena Hotel kama kawaida yake, au UVCCM wamemtema nao maana ndio wanaomuandalia mikutano pale Serena.

Sisi hapa Mwanza tunaelekea viwanja vya Furahisha kumsikiliza mwenyekiti...
 
Wenye Akili Tumeshamwelewa Zitto! Reality: Hana majina ya account holders. Ana majina na njia zinazoweza kupata wahalifu kama wapo. Ni vyema pia mkaelewa yawezekana wahalifu wasiwepo kabisa! BoT ilishasema hakuna fisadi mwenye akili anatumia mfumo wa Ki-benki.

Kwa nini hapendi kusemea nje ya Bunge!Hii ni strategy ya kupata Kinga ya Bunge ya Kikatiba that is it!

Subirini mtaona!
 
PHP:
[CODE][/CODE]

Kaka.... Zitto ameshakiri mwenyewe ofisini chini ya KIAPO..

Hivi kaka umeisoma post yote?? Maana hilo la kukiri lilifanyika kitambo saana hata bado hajaenda Uswis. Je, mpaka sasa hana hayo majina!!! Pia kumbuka kuwa nayo ni suala moja na kuwa na vithibitisho ni suala lingine.
 
Wenye Akili Tumeshamwelewa Zitto! Reality: Hana majina ya account holders. Any names and ways that can help to the culprit!
Kwa nini hapendi kusemea nje ya Bunge!Hii ni strategy ya kupata Kinga ya Bunge ya Kikatiba that is it!

Subirini mtaona!


Kupata taarifa za binafsi za kibenki ni kazi ngumu na inambana mtu kisheria. Si rahisi kwake kutaja namba za Account ila huenda walioweka pesa anawafahamu. Cha msingi ni je, hakuna fedha zilizofichwa nje ya nchi?? Kama zipo ni akina nani wanastahili kuja na taarifa za kina??
 
Kwahiyo alihitaji push ya Werema ndio ayataje hayo majina publically? Au alikuwa ananegotiate na wahusika kwanza.

Alishaahidi kitambo saana kuwataja, nadhani muda ulikuwa bado. Pia imeytusaidia kutambua jinsi ambavyo watu wanaweza kuungana na adui yao kisa chuki tu. Miaka yote Chadema imekuwa iko pamoja kwenye suala la fedha zilizofichwa nje ya nchi, ila baada ya hili, tumejikuta njia moja na CCM!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom