Zitto aamua liwalo na liwe juu ya mabilioni yaliyofichwa nje ya nchi

Status
Not open for further replies.
Zitto bwana akihishiwa hela tu anaanza ngonjera zake ili ale rushwa hana lolote........kama majina unayo kwanini usiweke? Mpe Lema basi kama unaogopa!!
 
Alishaahidi kitambo saana kuwataja, nadhani muda ulikuwa bado. Pia imeytusaidia kutambua jinsi ambavyo watu wanaweza kuungana na adui yao kisa chuki tu. Miaka yote Chadema imekuwa iko pamoja kwenye suala la fedha zilizofichwa nje ya nchi, ila baada ya hili, tumejikuta njia moja na CCM!!

Hapo kwenye BLUE una ushahidi na andiko lako au umejiaminisha bila kuushirikisha vizuri Ubongo wako?
 
Kwani anayetuhumiwa ni Zitto au Chadema??? nani katika Chadema anaemuzwa na hili?? Nani kasimama naye hata pale alipotuhumiwa wazi wazi Bungeni?? Nimewaona akina Msigwa wakisherehekea kwa Zitto kusemwa vibaya na AG!! Ndio hao unaowataka ashirikiane nao?? Kuwa mkeli kaka, wengine wote ni wanasiasa wa matukio. Bora asimame pekee hata kufa kwenye ukweli. Si lazima uungwe mkono na wasiopenda kweli!!

Siasa ni kutafuta uungwaji mkono, hakuna mwanasiasa duniani aliyewahi kufanikiwa pasipo kushawishi na kuungwa mkono. Kama Zitto hana uwezo wa kuwafanya maadui kuwa marafiki au kushawishi majority kumuunga mkono then hafai kuwa mwanasiasa. Hiyo ya yeye kubaki peke yake ni kazi bure, hata kama idea zake ni kweli. na bytheway haiwezekani ideas zake kama ni za kweli zisionekane kwa wooote hasa wa chama chake, haiwezekani eti yy Zitto is exceptional, that he sees what others can not see, a Prophet.
 
Anaenda kuzungumzia bungeni ili awe na kinga ...azungumze hadharani kama wenzie walivyotaja list of shame pale Mwembe yanga . Zitto acha Comedy

pole sana mkuu, kumbe shida yako ni ataje hadharani kama slaa na wala sio washughulikiwe??

hivi shida yetu ni kujua walioficha pesa na washughulikiwe auu ni kuwataja kwenye kadamnasi then tushangilie alafu basi.....

tuache unazi siasa bongo hatuziwezi
 
Hivi waswahili mnajua maana ya kiapo cha kisheria?


Acheni kubebewa akili, nawahakikishia kwamjibu wa kiapo cha Zitto kilichopo kisheria, hata leo hii akaamua kutaja kinachoitwa majina na akaunti za watanzania waliohifadhi fedha Uswisi na kwingineko, serikali haitashugulikia majina hayo, zaidi atakuwa anajifurahisha tu Zitto,

Kibaya zaidi nikuwa sasa Zitto atafikishwa mahakamani kwa yeye kumtaja binadamu yeyote katika jamhuri ya Wadanganyika,

Zitto anahitaji mshauri makini, hawa vichwa maji akina Msando watasababishwa apotee kabisa kisia na kimaisha,
Ngoja tuone kwa maelezo ya makala hii si zitto anasema AG ni muongo, labda na hicho kiapo ni feki
 
Ngoja tuone kwa maelezo ya makala hii si zitto anasema AG ni muongo, labda na hicho kiapo ni feki

mhhhhh adui muombee njaaa...
yericko leo unajifanya kumuombea mema adui yako zitto? eti atafutiwe mshauri....

mnakutia aibu chama viongozi kuchambana mitandaoni...
 
safi kaka wataje bana maana yawezekana na huyo mwanasheria mkuu ni mmoja wao au kuna marafiki zake anataka kuwaficha
 
ngoja nimsubili hapahapa sitoki maana mziki wenyewe naona unafifia labda betree
 
teh teh, wewe kweli mipango mingi, kwa hiyo kila kinachosemwa na werema ni uwongo? Acheni huo upuuzi, sio kila kinachofanywa na ccm ni uwongo.

Ndiyo maana nimewauliza kwa sababu hao jamaa kila kinachosemwa au kufanywa na serikali wao kwao ni kubeza tu. Kuna new developments katika maeneo mbalimbali wao wanabeza tu. Huyo Werema wamesham-blacklist mara nyingi na muda mrefu. Hii ya "kutengua" uamuzi wao ni aina ya mfano wa kuonesha kucha zao walizoficha ambazo tunaanza kuziona kwa kuendesha siasa za chuki, visasi, na uadui. Hali ya kuwa siasa si uadui bali mashindano ya hoja yenye lengo la kuwaletea maendeleo wananchi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom