joseeY
Senior Member
- Nov 4, 2010
- 108
- 17
Zitto amewaasa wakazi wa Igunga kuchagua mbunge atakayeweza kuwasemea kero zao ili zifanyiwe kazi.Nianze kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa wagombea wote, wameonyesha namna walivyojiandaa kuwatumikia wananchi, alisema Zito na kuongeza:
Kumbukeni kuwa uchaguzi huu si wa kuamua nani anajua kutukana, nani kavuliwa hijabu ni uchaguzi uliolenga kumpata Mbunge wa Igunga atakayeshughulika na matatizo ya watu.
Uchaguzi huu unaohusu kero za maji, ajira kwa vijana na hatima ya maendeleo ya watu wa Igunga na Chadema tumeshaonyesha mfano bungeni tupatieni mbunge wa 49 ili kutuongezea nguvu, alisema.
Aliwahimiza wakazi wa Igunga kwenda kupiga kura kumchagua mbunge atakayeweza kuwasemea bungeni na si bora kiongozi.Alisema watu wanakumbuka katika Bunge la Tisa ambalo wabunge wa Chadema walikuwa 11, lakini kazi zao zilionekana na sasa wamefikia 48.
Chadema hatuahidi maziwa na asali kwa wakazi wa Igunga, kazi zetu Watanzania mmeziona na mkatuongeza hadi kufikia 48 na sasa tunataka Igunga mtuongezee mtu wa 49 ili kutuongezea nguvu ya kufanya kazi.