Zitto aache upotoshaji

Zitto aache upotoshaji

kwa hiyo ZZK tumwiteje kwa nchi yetu na uchumi wetu?
Nionavyo mimi huyu mheshimiwa anajali maslahi binafsi kuliko ya taifa. Ni kweli alikuwa genuine mtetezi wa raslimali zetu lakini akawa compromized alipoteuliwa na Mh Kikwete kwenye ile tume ya madini. Kwa wenye kumbu kumbu CHADEMA walipinga ZZK kuwekwa kwenye ile tule kwa hofu hiyo hiyo. Na kweli baada ya yeye kuwepo kwenye ile tume mambo yakaanza kubadilika, mawasiliano yake na Rostam Aziz kuhusu mambo ya tume yakawekwa wazi yeye akalalamika sana, Akaja na hoja kuwa ACACIA waruhusiwe kupeleka makanikia nje kwa sababu sio mengi na kununua mitambo ya kuichangua nchini ingekuwa uneconomica kitu ambacho ni tofauti kabisa na msimamo wake kabla kuingia kwenye tume. Kuwa compromised kulimpa uwezo wa kuja kuanza kudai kuwa anafaa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA na ndio ukawa mwanzo wa mgogoro kati yake na viongozi wengine CHADEMA. Ni jeuri ya pesa hiyo. Kwa bahati mbaya sana kwa vile ZZK alikuwa genuine mtetezi wa raslimali za TZ mpaka kufukuzwa kwenye vikao vya Bunge kuna watu wanaamini huyu wa sasa hivi ni yuleyule, very unfortunate. Naamini anachoongea kuhusu kesi kuna ukweli kiasi kikubwa kwa maana yeye na ACACIA sasa hivi ni inseperable.
 
Ogopa sana huo mchezo! Huo mchezo kautumia sana Nimrod Mkono....!!! Hata kwa maamuma kama mimi nilikuwa nafahamu kwamba kesi husika lazima tungepigwa chini lakini pamoja na yote hayo, Nimrodi Mkono alikuwa anawashauri kufungua shauri jipya au kukata rufaa kwa sababu tu anafahamu yeye ataendelea kukunja pesa bila kujali tumeshinda au hapana!!!

GUYS, issue hapa sio nani ana haki bali suala zima la kisheria! Issue ya IPTL ilivurugwa since day one!!

Na serikali ya Mkapa chini ya Andrew Chenge iliuvurunda vurunda sana Mkataba wa IPTL kama ambavyo ilifanya kwa TICTS! Matokeo yake, kuna kesi kadhaa kati ya TANESCO na IPTL Stuffs lakini asilimia kubwa ya hizo kesi TANESCO wamekuwa wakipigwa chini na kesi ya kwanza kabisa ilikuwa 1997! So since 1997 to 2018, sisi ni watu wa kupigwa chini tu kila linapokuja suala la IPTL!
Uko sawa. Hii ni mizigo mizito. Ndiyo maana sasa tumemwachia mwenyewe mnyamwezi aibebe. Na ameanza kuselema nayo. Kuhamia dodoma inaselema. Stieglers gauge inaselema. Reli ya SGR inaselema. Suala la viwanda linaselema. ATCL inaselema. Na hili la IPTL limeshaanza kuselema. Ndiyo maana waswahili waliwahi kusema "Mzigo mzito mpe Mnyamwezi". Punde mambo yote yatanyooka tu. Tuvute subira.
 
Mbele ya sheria hakuna cha Mnyamwezi wala Mmatumbi...

Mbaya zaidi,kwenye legal ground kwenyewe unakuta wachezaji wao, marefa wao, washika vibendera wao!

"Mnyamwezi" Magu angewaweza hawa jamaa endapo angekubaliana na ushauri wa Tundu Lissu... kwamba, tunajitoa kwanza kwenye mikataba ya kimataifa kisha tunaanza ku-deal nao wenyewe huku huku ndani kwa kutumia Mawakimu Mahakimu wetu wenyewe!

Lakini kwa bahati mbaya sana, serikali na pro-serikali mkaibebea bango kauli ya kwamba TL amesema tutashitakiwa huku mkipuuza kauli ya kwamba tujiondowe kwanza ili kuwavunja nguvu za kwenda kutushitaki kwenye mahakama tusizozitambua! Na hadi leo Pro-serikali huwa wanauliza kwa mbwembwe na mikogo "mbona hawatushitaki basi...!" Yaani wanasahau kwamba kuna shauri London Court of International Arbitration!!

Kumbe basi, ingawaje ni kweli pia tungepata misukosuko kwa kujitoa lakini baada ya kujitoa pasingekuwa na wa kwenda MIGA wala London Court of International Arbitration na badala yake wangeamua kukimbilia Mahakama Biashara Dar es salaam ambako na kwenyewe mahakimu ni wa kwetu!
 
Mbona unaandika huku ukiwa unatetemeka?Hivi FBI inafanyaje kazi?
 
Tulia wewee! Mzigo umebebwa na mwenyewe. Wewe huuwezi. Acha blabla. Punde hayo yote yatakuwa historia. Na sasa yameanza kuselema!
 
Yaani yeye ujinga anaouwaza ni kupatika kwa ripoti si rahisi... badala ya kuwaza KWAMBA THE REPORT NI HEARTBREAKING......

Hustorically.....
1. Samaki wa Magu tulilipa...
2. Kituo cha mafuta kilichobomolewa Mwanza tulilipa...
3. Kituo cha mafuta Mlimani city tulilipa
4. IPTL tunalipa.....

Kwa LAWS za proportionality, wallah na hii ndude tutalipa....
Kwamba ni mtanzania moja tu ndo kusababisha hasara yote hii!!!?

Kama ingekuwa china wangemfanyajeee!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani hata tukiwalipa shida iko wapi? Nchi yetu si masikini. Na tukwalipa hao Acasia tutawatimua nchini kwetu. Kwanza hatuna mkataba nao wo wote. Wahuni tu. This is not their country. Matapeli wakubwa! Tutawalipa kile mnachokiita ushika uchumba cha Barick.
So unakiri Tundu Lissu alikuwa sahihi ee
 
Jamani hivi Watanzania mmesahau uhusiano wa ZZK na ACACIA? Mnakumbuka ile dissertation ya master's degree ya mwanafunzi kutoka Marekani aliyetafiti kuhusiana na mikataba ya madini TZ aligundua nini cha kushangaza? Kea aliyesahau ni kwamba alishangaa kuona kiasi cha pesa alichopewa mbunge ambaye Jimbo lake liko mbali na migodi wa ACACIA na isitoshe huyo mbunge akajengewa kituo cha afya jimboni kwake mbali kabisa na Jimbo lililopo mgodi wa ACACIA. Wajuaji a walipojiuliza sababu wakagundua ZZK alikuwepo kwenye tume ya Rais Kikwete kuhusu mikataba ya madini. Hivyo usishangae ZZK anazo inside information from ACACIA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Point yako ni ipi sasa? Kwamba Zitto ndie aliekwenda kushtaki au? Au ni uongo kuwa hatujashtakiwa?
 
Ogopa sana huo mchezo! Huo mchezo kautumia sana Nimrod Mkono....!!! Hata kwa maamuma kama mimi nilikuwa nafahamu kwamba kesi husika lazima tungepigwa chini lakini pamoja na yote hayo, Nimrodi Mkono alikuwa anawashauri kufungua shauri jipya au kukata rufaa kwa sababu tu anafahamu yeye ataendelea kukunja pesa bila kujali tumeshinda au hapana!!!

GUYS, issue hapa sio nani ana haki bali suala zima la kisheria! Issue ya IPTL ilivurugwa since day one!!

Na serikali ya Mkapa chini ya Andrew Chenge iliuvurunda vurunda sana Mkataba wa IPTL kama ambavyo ilifanya kwa TICTS! Matokeo yake, kuna kesi kadhaa kati ya TANESCO na IPTL Stuffs lakini asilimia kubwa ya hizo kesi TANESCO wamekuwa wakipigwa chini na kesi ya kwanza kabisa ilikuwa 1997! So since 1997 to 2018, sisi ni watu wa kupigwa chini tu kila linapokuja suala la IPTL!

Hatupo huko sisi tupo makinikiani. Tutashinda?
 
Uko sawa. Hii ni mizigo mizito. Ndiyo maana sasa tumemwachia mwenyewe mnyamwezi aibebe. Na ameanza kuselema nayo. Kuhamia dodoma inaselema. Stieglers gauge inaselema. Reli ya SGR inaselema. Suala la viwanda linaselema. ATCL inaselema. Na hili la IPTL limeshaanza kuselema. Ndiyo maana waswahili waliwahi kusema "Mzigo mzito mpe Mnyamwezi". Punde mambo yote yatanyooka tu. Tuvute subira.
Kumbuka yote haya ni madeni tu(mikopo ya kibiashara yenye riba) na usidhani waliomtangulia walishindwa kukopa kwa kiwango hiki bali walizingatia ushauri.

Ni kweli hii miradi na hii mipango yote inaweza kukamilika ili tupate sifa za kisiasa ila mwisho wa siku tutaishia kuwa kama Waethiopia wanaokimbia nchi yao.

Hii miradi imetekelezwa kisiasa zaidi na inagharimu nchi matrilioni ambayo yalipaswa pia kuelekezwa katika sekta nyine muhimu kama kilimo,afya,kulipa madeni ya ndani, ajira, kupunguza mzigo wa madeni ya nje, mikopo kwa wanafunzi, kulipa mafao ya wastaafu,n.k.

Kinachokwenda kutokea huko mbeleni ni serikali kulazimika kutenga matrilioni kila mwaka wa fedha ili kulipa madeni haya huku ATCL ikiendelea kuwa mzigo kwa kukomba pesa za walipa kodi kama ruzuku mbali na hela tulizokopa kununua hizi ndege.

Kufufua ATCL na kuhamia Dodoma ni mifano miwili ya mipango iliyofaa kutekelezwa kwa awamu na si yote kwa wakati mmoja maana hii mipango ni mizigo tu kwa serikali na wala hizo fedha hazitarudi zaidi ya kuwa zimetukima tu kama gharama kwa serikali(ATCL haiwezi kuleta faida leo wala kesho).

Ndio maana wapinzani walishauri serikali ihusishe sekta binafsi katika kutekeleza hii miradi ya matrilioni ili kuipunguzia serikali gharama.

Nyie siku zote huwa ni wabishi alafu mkishaharibu mnaleta propaganda kama sasa kwenye hii issue ya kushitakiwa na Acacia.

Mtakamilisha hii miradi lakini sehemu kuvwa ya mapato ya nchi hii na kwa miaka mingi ijayo itaishia kulipa madeni haya yanayotokana na mikopo hii yenye riba kubwa na hapo ndipo mtakuja kuona hasara ya kutekeleza miradi hii ya matrilioni ndani ya muda mfupi tu ili kupata sifa za kisiasa na msisahau tunakwenda kudaiwa matrilioni mengine kutokana na kesi za kibiashara katika mahakama za kimatifa.

Mnakwenda kupunguza uwezo wa serikali kugharamia wananchi wake katika sekta za kijamii kama afya,elimu,n.k kutokana na madeni haya kwani makusanya ya TRA yatalazimika kutumika kulipa mikopo hii ya matrilioni na mnaweza kuja kujikuta mnalazimika hata kukopa ili mlipe baadhi ya madeni.

Hamuwazi kuzalisha na kubuni vyanzo vipya ya mapato bali mnawaza zaidi kukopa ili mtekeleze miradi ya kuwapatia sifa za kisiasa pasipo hata kuangali mbele.

Endeleeni na mipango yenu ya bila tahadhari mtakuja kuona matokeo yake.
 
Ndugu, kinachokusumbua hapo ni LUGHA tuu, hizi sheria zingeandikwa kwa kiswahili ungeelewa vizuri sana.Hakuna sehemu iliyokata kuchapisha kama umekidhi vigezo.
 
ZZK kaileta hiyo habari katika mfumo wa kimbeya, mfumo ule ule wa Twitter na Facebook mfumo wa kusema nasikia.

Yale yale TL akiwa kule Belgium anasema nasikia kwamba hizi ndege ni mbovu, hajui kwamba kuna watu wapo karibu na jiko kuliko yeye aliye sebuleni.
Hata aliposema bomberdie imekamatwa kwa madeni mlisema hivi hivi kwamba ni umbeya,muda utasema,lakini tatizo lenu ni mnasahau mapema sana,hamjifunzi na hamna aibu hata kidogo mambo yanapothibitika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo shida kwa sababu hiyo pesa ni kidogo sana kama kweli ni haki yao. Kama siyo haki yao tutakata rufaa/review ambayo itaendeshwa na wanasheria wetu kutoka ofisi ya AG badala ya wa kukodi kutoka TLS ambao mara zote huwa tunapigwa! Na ndivyo tutakachofanya kwenye ile hukumu ya Tanesco. Tukishindwa tutalipa.
1.Kama ni kweli hiyo pesa sio ndogo,ni nyingi sana,labda kama hujui hesabu
2.Wanasheria wa AG ni members wa TLS pia,hujui hata maana ya TLS,imeanzishwaje, mahusiano yake na bunge na serikali.Umekalia tu propoganda nyepesi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom