Zitto Kabwe: Wahariri waulizeni CHADEMA wana mikakati gani ya kumtoa Mbowe jela

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
50,121
36,628
Zitto Kabwe kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo amewambia wahariri wa vyombo vya habari kuwa amefanya sana jitihada kumtoa Mbowe jela na Mbowe mwenyewe alibariki jitihada za Zitto kupambana kumtoa jela.

Zitto anasema kuwa CHADEMA wanamuona Mbowe kama mwenyekiti yeye ana muona kama kaka yake ambaye yuko gerezani!

Zitto ametaka wahariri wawatafute viongozi wa CHADEMA wawaulize wamefanya jitihada gani kumtoa Mbowe jela?

My opinion!

Zitto anaona wazi kuwa njia ya Chadema kutumia mahakama kumpambania Mbowe haiwezi zaa matunda kamwe na ana hakika haitozaa na ndio maana anaona njia ya kumuombea msamha kwa Rais ndio njia bora na anawaona Chadema hawafanyi lolote liwezekanalo kumtoa Mbowe!

Zitto anaona Mbowe amefanya kosa tofauti na sisi tunavyo ona? Zitto anajua zaidi kuzidi sisi?

Zitto anawezaje kujitenga na hoja ya kutaka kutumika na CCM kama daraja la kumtafutia Rais umaarufu....kwa kutengeneza tatizo na kulitatua na kujipigia makofi?

Zitto ni kweli anaamini Mbowe ni gaidi?

=========

Zitto Kabwe amesema:

"Sakata la Freeman ni moja kati ya vitu vinavyoniumiza sana, Freeman amenilea, ninavyomuona yupo jela simuoni kama Mwenyekiti wa CHADEMA, namuona kama Kaka yangu, nimefanya jitihada kuhakikisha anatoka Jela na kila nilichofanya kina ruhusa ya Mbowe, nimeenda Jela na nimeongea nae kumuambia nataka kufanya hivi akaniambia fanya"

"Wao wanamuona Mwenyekiti wao yupo Jela Mimi namuona Kaka yangu yupo Jela huo ndio utofauti, Wahariri waulizeni wenzetu wana mikakati gani ya kumtoa Mbowe nje ya Jela, Mimi naamini tulichofanya Dodoma (kumuomba Rais Samia amsamehe Mbowe) isingeleta kelele zilizopigwa, leo tungekuwa na Mbowe nje, naamini hivyo"
 

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
13,598
26,384
Ni kuzidi kumtia moyo tu kwa sababu kwa hali ilivyohakuna namna zaidi ya kucheza na vifungu vya sheria vinginevyo liwekwe shibikizo ambalo kwa hakika litachukuliwa kama vitendo vya kigaidi tena
 

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
8,928
29,360
Zitto ni mnafiki na shetani mkubwa, CHADEMA wanazo mpaka taarifa za Zitto akichonga na maafisa wa serikali kuhakisha kesi inayomkabili Mbowe iishie kwa Mbowe kufungwa kimahakama. Ushahidi upo.

Pia Zitto aache uongo, Mbowe hajamtuma mtu mwingine yoyote kumtafutia msamaha wa kutoka jela. Mambo yote ya Mbowe yanasemewa na yeye mwenyewe Mbowe, Familia yake, Viongozi wa Chadema au Mawakili wake, na wote hao wamekuwa na msimamo unaofanana.

Zitto aiche Chadema na mambo yake, aendelee na siasa zake za kuilamba viatu CCM na serikali ya Mama Samia.
 

Skylar

JF-Expert Member
Nov 10, 2021
1,596
3,851
Zitto kabwe kiongozi wa chama cha ACT wazalendo amewambia wahariri wa vyombo vya habari kuwa amefanya sana jitihada kumtoa Mbowe Jela na Mbowe mwenyewe alibariki jitihada za Zitto kupambana kumtoa Jela

Zitto anasema kuwa chadema wanamuona Mbowe kama mwenyekiti yeye ana muona kama kaka yake ambaye yuko gerezani!

Zitto ametaka wahariri wawatafute viongozi wa chadema wawaulize wamefanya jitihada gani kumtoa Mbowe Jela?

My opinion!

Zitto anaona wazi kuwa njia ya Chadema kutumia mahakama kumpambania Mbowe aiwezi zaa matunda kamwe na ana hakika haitozaa na ndio maana anaona njia ya kumuombea msamha kwa Rais ndio njia bora na anawaona chadema hawafanyi lolote liwezekanalo kumtoa Mbowe!

Zitto anaona Mbowe amefanya kosa tofauti na sisi tunavyo ona? Zitto anajua zaidi kuzidi sisi?

Zitto anawezaje kujitenga na hoja ya kutaka kutumika na CCM kama daraja la kumtafutia Rais umaarufu....kwa kutengeneza tatizo na kulitatua na kujipigia makofi?

Zitto ni kweli anaamini Mbowe ni gaidi?

View attachment 2110118
Kwani Rais anaruhusiwa kuingilia uhuru wa mahakama? Au hao chadema wana ruhusa ya kuingilia uhuru wa mahakama?

Labda kuna ambalo hatulifahamu na ingekua vizuri kama bwana Zitto angetufahamisha
 

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,502
11,510
Ndg. Zitto bado anaamini...

kwamba Mbowe ni gaidi
Kwamba alivyomuombea msamaha Freeman kwa Rais Samia Dodoma. Ilikuwa aachiwe huru.
Kwamba kelele zetu za kumwambia hajatumwa na CHADEMA, wala Mbowe kumuombea msamaha kwa Rais Samia zinasababisha Mbowe kusota mpaka sasa!?

Ni ujinga wa zitto kichwani kwake
 
6 Reactions
Reply
Top Bottom