Zitto aache upotoshaji

Zitto aache upotoshaji

ZZK kaileta hiyo habari katika mfumo wa kimbeya, mfumo ule ule wa Twitter na Facebook mfumo wa kusema nasikia.

Yale yale TL akiwa kule Belgium anasema nasikia kwamba hizi ndege ni mbovu, hajui kwamba kuna watu wapo karibu na jiko kuliko yeye aliye sebuleni.
Nani wa karibu na jiko anaweza akamfunga paka kengere..??
Nani huyo? .... Yale maneno.......I WISH ICOULD BE IGP..... unadhani IGP wa sasa atafanya lolote? .... Yale maneno... TUMEKUPA GARI, TUNAKULIPA MSHAHARA, HALAFU UNAMTANGAZA MPINZANI KUWA MSHINDI...!!! Mkurugenzi yupi ataenda tofauti na hayo amneno??

KUKAA KARIBU NA MAHAKAMA SI KUJUA SHERIA....

Ngali K
 
Unaweza kumuambia aache kutumika na kampuni ya Accacia kuudanganya umma na kujenga hofu kuwa maamuzi ya mahakama ya usuluhishi yataigharimu serikali ili hali si kweli kwani kanuni ya 30 ya Arbitration ya LCIA hawachapishi taarifa zao hivyo tumuulize Zitto Zubeir Kabwe kazitoa wapi?

Nimekuwekea hapa hiyo kanuni upitie..

#TuweWazalendo #HawanaChaKuzusha #SerikaliMakini View attachment 856079

Sent using Jamii Forums mobile app
Uongo wake upo wapi,unashangaa sheria hamruhusu lakini yeye kazipataje info?sasa hapo si ungeanza kumsifia njia alizotumia kuokota taarifa maana ukiwa mzalendo wa nchi yako unaweza kufanya hata yale yasio wezekana,wewe uzalendo wako ni kuja kumpinga humu grow up acha utoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata aliposema bomberdie imekamatwa kwa madeni mlisema hivi hivi kwamba ni umbeya,muda utasema,lakini tatizo lenu ni mnasahau mapema sana,hamjifunzi na hamna aibu hata kidogo mambo yanapothibitika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Siasa za unafiki wake. Ukishangilia shida za mtu mnayeishi nae ndani ya nchi moja, huna tofauti na msaliti.

Kikikupata kibaya usije ukalialia ukitaka uhurumiwe. Hakuna siasa mbaya kama zile za kuzungukana, leo tunakula na kunywa pamoja halafu wewe au mimi kesho nakwenda kukuuza tena kwa watu ambao hawana undugu wowote kwetu sisi.
 
Nani wa karibu na jiko anaweza akamfunga paka kengere..??
Nani huyo? .... Yale maneno.......I WISH ICOULD BE IGP..... unadhani IGP wa sasa atafanya lolote? .... Yale maneno... TUMEKUPA GARI, TUNAKULIPA MSHAHARA, HALAFU UNAMTANGAZA MPINZANI KUWA MSHINDI...!!! Mkurugenzi yupi ataenda tofauti na hayo amneno??

KUKAA KARIBU NA MAHAKAMA SI KUJUA SHERIA....

Ngali K
Kuwa karibu na jiko sio lazima uwe karibu na mpishi mkuu, unaweza ukawa mshauri wa mshauri mkuu wa mpishi mkuu.
 
Ma-CCM bhana...

Yaani unaona kabisa wameandika ",,,doeesn't publish WITHOUT halafu una-conclude kwamba hawachapishi?!

Hivi mtu akiandika "... you can't enter the examination room WITHOUT a pen; ina maana wamesema HUWEZI kuingia kwenye chumba cha mtihani?
The problem unachanganya mambo!

Wanaweza wasi-publish but both parties zitakuwa na ripoti husika... Loser and Winner! That having said, Zitto anaweza kupata ripoti toka kwa Loser or a Winner!! Na ikiwa hata government reports with CONFIDENTIAL/TOP SECRET Stamps bado huwa zinawafikia unauthorized eyes, seuze hizo!!

Hoja yako ingekuwa na mantiki IF AND ONLY IF ungekuwa umeiona hukumu husika na kujiridhisha kwamba inasema kinyume na madai ya Zitto!! Kinyume cha hayo, ni wewe ndie unataka kupotosha watu hapa!!
Mkuu chige hujawahi kuniangusha. Nakuelewaga sana.
 
Unaweza kumuambia aache kutumika na kampuni ya Accacia kuudanganya umma na kujenga hofu kuwa maamuzi ya mahakama ya usuluhishi yataigharimu serikali ili hali si kweli kwani kanuni ya 30 ya Arbitration ya LCIA hawachapishi taarifa zao hivyo tumuulize Zitto Zubeir Kabwe kazitoa wapi?

Nimekuwekea hapa hiyo kanuni upitie..

#TuweWazalendo #HawanaChaKuzusha #SerikaliMakini View attachment 856079

Sent using Jamii Forums mobile app
Kujua mapema nako ni jambo jema kwani itatusaidia kujipanga. Zaidi ya hapo ujue hakuna siri ya watu wawili ndio maana hata kinachoitwa siri za serikali huwa kiuhalisia hakuna ndio maana zote au yote yanayopangwa gizani na watu huletwa hadharani na watu hao hao. Siri ni wewe mwenyewe peke yako na Mungu wako. ukishasema "its members" basi hakuna siri tena hapo cha msingi hapo hapo ni kutafuta ukweli badala ya kukomalia kapata wapi kama tatizo lipo haliwezi kufunikwa au kupozwa na siri. After all mwisho wa siku tutalipa tu kama tulivyokuwa tunadaiwa mpaka ndege ikakamatwa. Kwani mwanzo si ilikuwa siri?
 
Ma-CCM bhana...

Yaani unaona kabisa wameandika ",,,doeesn't publish WITHOUT halafu una-conclude kwamba hawachapishi?!

Hivi mtu akiandika "... you can't enter the examination room WITHOUT a pen; ina maana wamesema HUWEZI kuingia kwenye chumba cha mtihani?
Wapeleke shule mkuu mpaka waelewe nasikia mkubwa wao katangaza hadharani kuwa ni kichaa sasa sijui wafuasi wake itakuwaje?!
 
Unaweza kumuambia aache kutumika na kampuni ya Accacia kuudanganya umma na kujenga hofu kuwa maamuzi ya mahakama ya usuluhishi yataigharimu serikali ili hali si kweli kwani kanuni ya 30 ya Arbitration ya LCIA hawachapishi taarifa zao hivyo tumuulize Zitto Zubeir Kabwe kazitoa wapi?

Nimekuwekea hapa hiyo kanuni upitie..

#TuweWazalendo #HawanaChaKuzusha #SerikaliMakini View attachment 856079

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama wameamua ku-disclose hivi vifungu je! By the way na mimi labda niulize hii article umeipaje?
 
Mkuu Masiga, wewe ndio uache upotoshaji, kwa vile nyingi ya arbitrations ni mashauri ya kimataifa ambayo matokeo yake huwa ni final and conclusive, ili hiyo awards iweze kutekelezwa, it has to be registered kwenye domestic laws kwa kusajiliwa Mahakama Kuu yetu ili ziweze kupata forces of law ziweze kutekelezwa. Local laws zetu hazina hiyo clause, hivyo kila mtu atajua, ndio maana tuliijua tozo ya dowans, na kwa taarifa, ililipwa japo kwa siri!. Juzi bombadier zetu zilishikwa Canada, tumelipa!. Hizi pesa za Stan Chart HK, pia tutalipa, unless wawaachie Ruge na Seti wabebe zigo lao.
Acacia kiukweli kabisa, dhamira yangu inaniambia tutapigwa!.
P
Braza P penye ukweli humumunyi maneno! ila maeneo mengine napo huwa unananino kabisa😀😀
 
Tulia wewee! Mzigo umebebwa na mwenyewe. Wewe huuwezi. Acha blabla. Punde hayo yote yatakuwa historia. Na sasa yameanza kuselema!
Man, kwani wakati TANESCO wanaamriwa kuilipa Standard Chartered Hong Kong, huyo "Mnyamwezi" alikuwa wapi?!

Anyway, najua utasema "Mnyamwezi" hawezi kukubali kulipa.. there comes another question: Kwani ilipokamatwa Bombardier yetu nchi Canada kwa madeni ya miaka kadhaa iliyopita hadi serikali ikasalimi amri na kulipa deni; je huyo "Mnyamwezi" alikuwa wapi?!

Hii ngoma kwa "Mnyamwezi" ni ngumu; unajua kwanini?!

1. Unayosema yangewezekana endapo tu Tanzania ingeacha kuitambua mikataba yote ya kimataifa inayowapa wawekezaji kiburi... na hiyo ilikuwa ndiyo hoja ya Tundu Lissu!

2. I believe hata Magufuli mwenyewe anafahamu kwamba hiyo ndiyo solution but the problem ni kwamba, anafahamu akifuata huo ushauri atajiweka pabaya kwenye ndoto zake za Tanzania ya Viwanda!

So, yupo kwenye conflicting objectives... wakati upande mmoja anataka ku-deal na hawa jamaa lakini kwa upande mwingine pia anataka pesa zao! Kujitoa kwenye hii mikataba itakuwa ni sawa na kuwaaambia Wawekezaji "Come to Tanzania at your own risk!?"
 
Hatupo huko sisi tupo makinikiani. Tutashinda?
Tunashinda shinda vipi wakati mchezo waliuharibu wenyewe akina Magu?!

Serikali imewatuhumu Acacia kwamba the so called makinikia kina viwango vikubwa vya madini kuliko vinavyokuwa declared na Acacia wenyewe... WELL & GOOD!!

Baada ya serikali kuamini Acacia wanafanya janja janja, wakaamua kuteua Tume ya Professor kuchunguza ili kufahamu kiwango rasmi cha madini kilichomo kwenye makinikia!

Katika hali ya kushangaza kabisa, Tume ya Mruma ikafanya uchunguzi ule kwa kufungua makontena kadhaa wakiwa WAO TU... yaani upande wa Acacia hawakuhusishwa!!!

Sasa ni mahakama gani inaweza kutumia ushahidi uliotengenezwa na upande mmoja?!

Katika hali ya kawaida, palitakiwa iundwe Tume Huru ambayo both Acacia na Serikali wangekubaliana nayo au hata kupitia ile Tume ya Mruma, Acacia wangeshirikishwa hatua kwa hatua kama waangalizi ili kujiriidhisha hawachezewi fou katika suala la uchukuaji wa sample, kuzipima na kupata matokeo yake!!

Lakini wakati Uchunguzi wa Tume ya Mruma waliufanya peke yao bila kuwashirikisha Acacia, data ZOTE za Acacia walikuwa wanazi-declare baada ya kuwa verified na vyombo vya serikali kama vile Tanzania Mining Audit Agency (TMAA)!

Najua wapo watakaosema TMAA walikuwa wala rushwa... SAWA, lakini si taasisi yenu wenyewe?! Kuna popote ilipokuwa proved kwamba Acacia walikuwa wanawapa rushwa TMAA?!

Ndo narudi kwenye yangu ya mwanzo... issue hapa sio nani ana haki ambae bila shaka ni Tanzania lakini kinachoangaliwa ni sheria!!
 
Kwa hili Lissu ataibuka shujaa. Sijui jiwe ataificha wapi sura yake
 
Mie ninachojua mkuu alisema acacia tunawadai shs trilioni 400. hapa mie najua nina Noah yangu mpyaaaaaaaaaaaaa!
 
Anyway, najua utasema "Mnyamwezi" hawezi kukubali kulipa.. there comes another question: Kwani ilipokamatwa Bombardier yetu nchi Canada kwa madeni ya miaka kadhaa iliyopita hadi serikali ikasalimi amri na kulipa deni; je huyo "Mnyamwezi" alikuwa wapi?!
Hakuna deni lo lote lililolipwa kwa kuzuia bombardier yetu huko Canada. Take it from me. Huo ndiyo ukweli. AGOA hatutajitoa lakini lakini madeni ya kiutapeli tapeli hatutayalipa, yawe ya kimataifa au ya ndani. Yale halali tutayalipa baada ya kuyahakiki. Hiyo ya Standard bank na deni la Tanesco la IPTL serikali yetu haihusiki kwani Tanesco is a limited company. Hivyo hawawezi kukamata dreamliner yetu kwani si mali ya tanesco. Labda waje wakamate kinyerezi one ambayo ndiyo mali ya tanesco. Hakuna watakachotufanya na wala usiwe na wasi wasi. Sana sana watatusifu kwa kusimamia ukweli na kupambana na ufisadi huu wa kimataifa na ule wa ndani.
 
Hahahaa!!

Kwahiyo hata baada ya Bombardier kuwa imeshikiliwa kwa miezi kadhaa unataka kuamisha watu iliachiliwa bure bure!!!

Kwamba, hamlipi madeni ya kitapeli labda unasahau kwamba ni hayo hayo madeni unayoita ya kitapeli ndiyo yalifanya Bombardier ikamatwe!!!

Kwamba, deni la Standard Chartered na TANESCO serikali haihusiki kwa sababu TANESCO ni limited company na kwamba haliwezi kusababisha Dreamliner kukamatwa labda unasahau kwamba deni ambalo lilifanya Bombardier ikamatwe linahusiana na mikataba ya ujenzi wa barabara... sasa sijui barabara na Bombardier wapi na wapi!! Aidha, labda nikukumbushe tu kwamba, TANESCO ni parastatal organisation, 100% owned by the government!

Kwamba, hakuna watakachotufanya ni kwavile kwa makusudi umejisahaulisha walichotufanya kwenye Bombardier mbele ya uso wa JPM!

Kwamba watatusifu, you're probably right... watatusifu pale tutakapojikuta tunaondoa pesa kutoka kwenye bajeti ya maji vijijini na kwenda kulipia madeni!

Labda nimalizie jambo moja... hapa hatuzungumziaa na wala sijazungumzia popote kuhusu AGOA bali MIGA... anyway, I know, it might be a human error! Hata hivyo, lazima nitamke wazi kwamba, lau kama mabilioni tuliyowekeza kwenye ndege tungeyaelekeza kwenye kuhakikisha tunafanya vizuri AGOA basi Tanzania tungepiga hatua kubwa sana and trust me, kwa hilo ningempongeza sana President Magufuli!
 
H
ZZK kaileta hiyo habari katika mfumo wa kimbeya, mfumo ule ule wa Twitter na Facebook mfumo wa kusema nasikia.

Yale yale TL akiwa kule Belgium anasema nasikia kwamba hizi ndege ni mbovu, hajui kwamba kuna watu wapo karibu na jiko kuliko yeye aliye sebuleni.
 
Huyu ZZK hivi kwa nini amejikita kwenye mambo ya scandal za nchi tu? Huyu bwana anatoka mkoa ambao ni masikini kuliko yote Tanzania. Kila kitu, vikiwemo miundo mbinu ya barabara, reli na bandari, huduma za jamii ni hali ya chini. Mbona wabunge wengine wamejikita kutetea mikoa yao? Hawa wabunge wa Kigoma hasa ZZK wana matatizo gani? Inakuwaje aidha wamekaa kimya tuu au wanatetea issues ambazo hazisaidii mkoa directly. Mkoa wa Kigoma umebaki bila maendeleo tangu Uhuru. Mikoa mipya imekuja na kuipita Kigoma kwa sababu vikwazo vya maendeleo ni vingi mno. Inakuwaje wawakilishi wa wananchi wa mkoa huu hawana habari na mkoa wao. Huyu ZZK na wengine waliopita kama kina Kafulila ajitafakari. Kwanza atetee barabara ili mkoa ufikike, asikae kimya SGR inapo chepushwa kwenda Rwanda. Apigie kelele bandari ya Kigoma, apigie kelele meli mpya ziwani na mambo mengine kama hayo. Isitokee akaja kuwa irrelevant kwa wapiga kura wake.
 
K
Nionavyo mimi huyu mheshimiwa anajali maslahi binafsi kuliko ya taifa. Ni kweli alikuwa genuine mtetezi wa raslimali zetu lakini akawa compromized alipoteuliwa na Mh Kikwete kwenye ile tume ya madini. Kwa wenye kumbu kumbu CHADEMA walipinga ZZK kuwekwa kwenye ile tule kwa hofu hiyo hiyo. Na kweli baada ya yeye kuwepo kwenye ile tume mambo yakaanza kubadilika, mawasiliano yake na Rostam Aziz kuhusu mambo ya tume yakawekwa wazi yeye akalalamika sana, Akaja na hoja kuwa ACACIA waruhusiwe kupeleka makanikia nje kwa sababu sio mengi na kununua mitambo ya kuichangua nchini ingekuwa uneconomica kitu ambacho ni tofauti kabisa na msimamo wake kabla kuingia kwenye tume. Kuwa compromised kulimpa uwezo wa kuja kuanza kudai kuwa anafaa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA na ndio ukawa mwanzo wa mgogoro kati yake na viongozi wengine CHADEMA. Ni jeuri ya pesa hiyo. Kwa bahati mbaya sana kwa vile ZZK alikuwa genuine mtetezi wa raslimali za TZ mpaka kufukuzwa kwenye vikao vya Bunge kuna watu wanaamini huyu wa sasa hivi ni yuleyule, very unfortunate. Naamini anachoongea kuhusu kesi kuna ukweli kiasi kikubwa kwa maana yeye na ACACIA sasa hivi ni inseperable.
Kwa kifupi ZZK ni msaliti wa maendeleo ya uchumi wa taifa letu…he is a sell-out!
 
Back
Top Bottom