Watu wanaosema tunamrudishia Rais mchakato wa Katiba wanachangamsha Genge

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,131
Mjumbe wa Kikosi Kazi cha Prof. Mukandala Mhe. Zitto Kabwe yuko mubashara kipindi cha Kipima Joto ITV.

SWALI: Ripoti ya Kikosi Kazi kuhusu Demokrasia ya Vyama Vingi. Je, imejibu matarajio ya wananchi?

Karibu!



=======

Zitto Kabwe

Kwa mazingira ya Tanzania, mchakato wowote hauwezi kumkwepa Rais, wanaoongea wanachangamsha genge tu.

Tulichopendekeza kikosi kazi, Rais wa Tanzania kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar kuunda jopo la wataalam sababu mchakato wa Katiba ni wa kisheria.

Watu wanaosema tunamrudishia Rais mchakato wanachangamsha tu genge.

Deodatus Balile
Kuwepo kuaminiana, inavyoonekana vyama vya upinzani vimejeruhiwa, ndo maana hata Rais alisema hiyo siyo amri, sisi tumeonesha njia, ukisema Rais unamkwepa ipo siku tu utamhitaji.

Mimi ukinuiliza, mapendekezo haya ya kikosi kazi yanatoa mwanga. Mjadala wa kitaifa utarahisisha jambo hili, hata wabunge watakuwa sehemu ya mjadala wa kitaifa, Bungeni ni kupitia tu hivyo hawawezi kwenda kinyume cha mapendekezo ya mjadala wa kifaifa.

Nitoe wito, muda huo ukifika siyo muda wa kususa. Waje watoe maoni

Zitto Kabwe
Mchakato wa katiba unaongozwa na Sheria ya mabadiliko ya katiba, naona tunatiana tu hofu isiyo na msingi.

Wito wangu, hatua muhimu kuliko zote ni muswada wa mabadiliko ya katiba. Hatuwezi kujenga hoja barabarani, zinajengwa mezani. Taifa linajengwa kwa majadiliano, halijengwi kwa kukimbiana.

Deodatus Balile
Ikiwa kila mtu anakuja na kauli za iwe mvua iwe jua lazima apate anachotaka hatutafika. Tunataka mazungumzo, na yeyote anayedhani ana nia njema na nchi yetu aje na mapendekezo yanayopelea kwenye kikosi kazi, inaweza kuchukua muda.

Zitto Kabwe
Katiba yetu na sheria zetu hazikatazi mikutano ya hadhara, kikozi kazi kimesema katiba inaruhusu, ni haki ya chama cha siasa ndiyo maana tumesema iendelee, iruhusiwe kwa mujibu wa kisheria.

Mwanzoni kulikuwa na katazo, kwa waliokuwa wanalitekeleza walikuwa wanavunja sheria na sisi pia tuliokuwa tunatii agizo hili tulikuwa tunavunja sheria.

Tuliona kuna sheria zinaweza kutumika vibaya, mwaka 2019 yalifanyika mabadiliko, sehemu inayotoa haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano kikachomekwa kipengele cha polisi kuingilia mikutano. Kikosi kazi kinataka hicho kipengele kiondolewe.

Tuligundua pia kuna kanuni za vyama vya siasa za mwaka 2019, kuna masharti ya hovyo sana. Kikosi kazi kikasema sheria hizi zifanyiwe marekebisho.

Rais anaweza kuamka na kuchagua makamishna wa tume ya uchaguzi, kikosi kazi kimesema hapana.

Matokeo ya Rais yahojiwe kwenye mahakama ya juu pindi itakapoanzishwa.

Uchaguzi uliopita baadhi ya wagombea walikatwa kwa sababu za kipuuzipuuzi tu, mapendekezo ya kikosi kazi ni kuwa watu wakienguliwa pasipo kufuata taratibu wahusika wawajibishwe kisheria.
 
Kikosi gani? Kama kile cha karakana ya ibilisi ya bwana fulani aliye tenguliwa ukuu wa wilaya na kuyumikia kifungo?
 
Agusie na umuhimu wa tozo kwenye kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja. Ni mchumi yule hiyo hoja inamfaa
 
Kiukweli kiwango cha uelewa wa mambo makubwa kwa Watanzania wengi ni mdogo, hivyo hauko peke yako wengi wenye avarage understanding, wako kama wewe, kati ya wapinzani wote waliopo sasa, Zitto ndio the one and only capable kuwa rais wa JMT na nchi ikabaki salama!. Zitto ni Mzalendo wa kweli, Baada ya kumsikiliza leo, nimebaini haya...
P

Sio nchi ikabaki salama, sema wezi wa CCM wakabaki salama. Nchi kubaki salama inategemea nguvu ya vyombo vya dola chini ya kiongozi aliyeko madarakani.

Kwa nchi ya watu waoga kama yetu, rais anaweza kufanya lolote na asifanywe lolote, na kumuogopa Rais hiyo ndio tafsiri ya nchi kubaki salama.
 
Sio nchi ikabaki salama, sema wezi wa CCM wakabaki salama. Nchi kubaki salama inategemea nguvu ya vyombo vya dola chini ya kiongozi aliyeko madarakani. Kwa nchi ya watu waoga kama yetu, rais anaweza kufanya lolote na asifanywe lolote, na kumuogopa rais hiyo ndio tafsiri ya nchi kubaki salama.
Kiukweli tushukuru sana Mungu, kuna watu waligombea urais, kama wangepata, by now taifa letu lingeisha sambaratika!. ZZK ndie mpinzani pekee ambaye kwa sasa anaweza kuwa rais wa JMT na tukabaki salama, intact.
P
 
Kiukweli kiwango cha uelewa wa mambo makubwa kwa Watanzania wengi ni mdogo, hivyo hauko peke yako wengi wenye avarage understanding, wako kama wewe, kati ya wapinzani wote waliopo sasa, Zitto ndio the one and only capable kuwa rais wa JMT na nchi ikabaki salama!. Zitto ni Mzalendo wa kweli, Baada ya kumsikiliza leo, nimebaini haya...
P
Hapa hakuna suala la uelewa bali nimehoji wa Zitto.

Zitto kama Zitto hana uwezo wa kuliunganisha taifa, hana uwezo wa kuongoza taifa huyu kwa vigezo vyote ni mwanasiasa nja.
 
Kiukweli tushukuru sana Mungu, kuna watu waligombea urais, kama wangepata, by now taifa letu lingeisha sambaratika!. ZZK ndie mpinzani pekee ambaye kwa sasa anaweza kuwa rais wa JMT na tukabaki salama, intact.
P

Kama Magufuli alituongoza kama wake zake na bado taifa liko vile vile ukiacha uhasama uliopo, ni nani atashindwa kuongoza nchi hii kwa utashi wake? Na yoyote ambaye hatafuata aliyeko madarakani atakacho, anapotezwa tu.

Hii ni presidence iliyowekwa tayari. Kubaki intact sio kwa wananchi kupenda, bali ni kwa madaraka ya Rais, penda usipende.
 
Back
Top Bottom