Zinduna Talk Show: Leo mjengoni nipo na BADILI TABIA~~~~!

Zinduna Talk Show: Leo mjengoni nipo na BADILI TABIA~~~~!

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Posts
2,377
Reaction score
3,394
avatar45959_18.gif

BADILI TABIA

Habari zenu wana JF popote mlipo.

Kama nilivyowaahidi wiki iliyopita. Katika kipindi cha leo, tutakuwa na BADILI TABIA mjengoni ambaye baada ya kunizungusha sana, hatimaye amekubali mualiko wangu na kuja hapa Studio kwa mahojiano haya ambayo yatasawiri zaidi kwenye maisha yake binafsi na kazi zake za mapema.

Line za ku-post Comments ziko wazi, Mwana JF yeyote anaweza kutumia fursa hii kumuuliza BADILI TABIA swali lolote na yeye bila shaka atayajibu mwaswali yenu kwa kadiri atakavyopata muda.

Kwa kuanza ninayo maswali kumi na tano ambayo ningependa kumuuliza BADILI TABIA:

1. Je umezaliwa msimu gani?

2. Hebu nipe historia yako ya hapa JF kwa kifupi, yaani ulifahamuje kuhusu JF, ulijiunga lini na ni nini kilikusukuma hadi ukajiunga na JF?

3. Je Ulifahamuje kuhusu tendo la kujamiiana? Yaani ni nani alikufundisha kwamba hiyo kitu downthere ina matumizi mengine mbali na yale ya kutabawali?

4. Je Umewahi Kutendwa?

5. Je umeolewa? Kama umeolewa, Je una watoto wangapi, na kama hujaolewa, Je ni nini mustakabali wako wa maisha ya uzeeni?

6. Hebu nipe kwa kifupi kuhusu maisha yako ya shuleni, yaani ni changamoto gani ambazo ulikabiliana nazo kama mwanamke na leo hii ukiangalia ulipotoka unajiona kama shujaa.

7. Ukipata fursa ya kuwa waziri wa elimu ni kitu gani ungependa kukibadilisha kuhusu mfumo wetu wa elimu kwa ujumla?

8. Katika taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii ya kuanzia April 2011 hadi April 2012, kuhusiana na tatizo la mimba mashuleni kamati hiyo ilisema.

Nitanukuu:

"Mheshimiwa Spika,kuna usemi kuwa "ukimuelimisha mwanamke umeelimisha jamii nzima'' utafiti unaonesha kuwa uwiano wa wanafunzi wa kike na wakiume hupungua kadri wanavyoendelea na masomo ingawa wakati wa uandikishaji idadi ya wanafunzi wa kike huwa ndio kubwa. Kwa mujibu wa ripoti ya (Basic Education Statistic in Tanzania 2007-2011), katika shule za msingi idadi ya wanafunzi wa kike ni asilimia hamsini (50%) na idadi ya wanafunzi wa kiume ni asilimia hamsini (50%). Elimu ya sekondari idadi ya wanafunzi wa kike ni asilimia arubaini na tano (45%) na wa idadi ya wanafunzi wa kiume ni asilimia hamsini na tano(55%), vyuo vikuu wanafunzi wa kike ni asilimia thelathini na nne (34%) na wanafunzi wa kiume ni asilimia sitini na sita (66%).

Mheshimiwa Spika, Kamati inaamini kuwa idadi ya wanawake nchini ni kubwa zaidi ya wanaume, na mchango wao katika maendeleo ya nchi ni mkubwa, hivyo ni wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa vikwazo vinavyosababisha wanafunzi wa kike wasiendelee na masomo vinashughulikiwa na kupewa kipaumbele."

Mwisho wa kunukuu.

Swali: Je wewe unadhani serikali inapaswa kujivunia kwa uwiano huo? Je wewe ungeshauri nini kifanyike ili kuondoa kabisa tofauti hiyo na kuweka uwiano sawa?

9. Je ni tukio gani liliwahi kukuhuzunisha sana?

10. Je ni tukio gani liliwahi kukufurahisha sana?

11. Je unapenda kuvaa nguo za aina gani?

12. Je unapenda chakula cha aina gani?

13. Je ni jambo gani umewahi kulifanya kwa faida ya nchi yako na ambalo hata ukifa litabaki kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo?

14. Je ni mwana JF gani unavutiwa na post zake, yaani ukiona jina lake tu kama ame-post thread unashawishika kuifungua ili kujua kilichomo?

15. Una ushauri gani kuhusu hiki kipindi cha Zinduna Talk Show?

Haya nakaribisha maswali yenu wadau na hivi punde BADILI TABIA atakuja kuyajibu maswali yenu.

Karibuni sana
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na maswali yako yote napenda kuongeza yafuatayo,

1.0 Kipindi anajiunga na JF anafikiri nini mpaka akaamua kujiunga na ID ya BADILI TABIA????

2.0 Yeye ni mpenzi wa nini hasa katika maisha yake,yaani kitu ambacho kinampotezea muda mwingi kufikiri asipokifanya?? Mfano kama ni mnywaji basi asipokunywa akili yake anikiwa labda inawaza huko mpaka anywe, au kama ni JF member kama haja log in basi hajisikii au hata kama hajamuona mwandani wake akili haitulii n.k

3.0 Akiwa kama JF member ameshawahi kusikia kuhusu kitu kinachooitwa Multiple IDs???? Kama ameshewahi kusikia yeye kama anafikiri nini chanzo cha hicho kitu????

4.0 Kama angepata kuonana na Invisible angemshauri nini kwa mustakabali mwema wa JF.
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na maswali yako yote napenda kuongeza yafuatayo,

1.0 Kipindi anajiunga na JF anafikiri nini mpaka akaamua kujiunga na ID ya BADILI TABIA????

2.0 Hujamswalika kama yupo single au laaaah ila mafisimaji yaliyopo humu ndani tujiandae kama mkono utakatika????

3.0 Yeye ni mpenzi wa nini hasa katika maisha yake,yaani kitu ambacho kinampotezea muda mwingi kufikiri asipokifanya?? Mfano kama ni mnywaji basi asipokunywa akili yake anikiwa labda inawaza huko mpaka anywe, au kama ni JF member kama haja log in basi hajisikii au hata kama hajamuona mwandani wake akili haitulii n.k
Mzee wa Rula, hapo kwenye BOLD hebu soma swali langu la tano, naona jana ulikuwa kwenye EPIQ BONGO, hujalala umekesha na ndio maana hujasoma maswali yangu kwa ufasaha.
 
Last edited by a moderator:
Ningependa kuwashukuru wasaidizi wangu waliofanikisha interview hii, kwa upande wa mavazi yaani aliyenipendezesha mimi na BADILI TABIA ni cacico yeye analo duka lake maeneo ya Mbagala Maji Matitu, kwa upande wa nywele ni Aunt snowhite, yeye anayo saloon yake pande za Kipalang'anda, vipodozi ni gfsonwin akisaidiwa na charminglady na Madame B. Kwa upande wa fundi mitambo yupo Young Master akisaidiana na Mentor, na C6 . Anayefanikisha kurusha matangazo haya ni Bujibuji akisaidiwa na Nicas Mtei na pia Jiwe Linaloishi.

Kuna wale wanaowatuletea maji ya kunywa makoo yakikauka. Yupo Ciello, Kaunga, nivea, Yummy na lara 1.

King'asti
yeye ndiye Director wa kipindi hiki.
 
Last edited by a moderator:
Mzee wa Rula, hapo kwenye BOLD hebu soma swali langu la tano, naona jana ulikuwa kwenye EPIQ BONGO, hujalala umekesha na ndio maana hujasoma maswali yangu kwa ufasaha.

Swali hilo tayari nimeshalifuta. Si unajua tulikuwa tunasherekea ushindi.
 
Last edited by a moderator:
wadau hapa tunamalizia malizia kumpamba BT... tunatakata awafunike washiriki wote Walopita... tuna Products za MAC na ORiFLAME
 
Huyo uliyemtaja hapo juu, sihusiki ukipigwa BAN
MODS sitakuwa liable na maswali yatakayoulizwa kama yataleta rabsha.

Zinduna usiogope tehe tehe court of appeal si ipo???? Nitaalika mawakili wa kufa mtu kama Blaki Womani, PakaJimmy, Asprin, na huyo kijana anayechipukia Filipo. Mpaka hapo naamini nitakuwa nime escape from Sobibo.
 
Last edited by a moderator:
Qst for BT,
I have enjoyed gettin to know you as a person, and find your surprisingly matured for .......
Either i have no doubt you have the skills, focus, and so forth .
Also you have an intellectual attitude capacity with various kind of ambitions.
Sasa ili misifa yote hiyo niliyokupa nitambue bado unayo na haijapungua ni utakaponijibu swali langu dogo sana!
Na endapo utanijibu kiusahihi na fasaha, zawadi itakuhusu .
Nakuuliza usikiapo msemo "NJIA YA MELI , AU PALIPOPITA MELI HAPAACHI ALAMA" By the way
unaelewa nini ? Rejea kua semi hiyo imekaa kitafsida zaidi .
 
Back
Top Bottom