jokaKuu
1.Zimbabwe walikuwa na mkataba wa mafunzo ya kijeshi na Uingereza mpaka miaka ya 1998. Kwa msingi huo, wakati machafuko yanaendelea Ndembele, Uingereza ilikuwa ndiyo supplier mkuu wa silaha za Zimbabwe.
2.Ushirikiano wa kijeshi kati ya Zimbabwe na Uingereza ulikuwa mzito kiasi cha Special Forces[SAS] ya Uingereza kufundisha Paratroopers wa Zimbabwe. Wakati vita ya FRELIMO vs RENAMO imechachamaa majeshi ya Zimbabwe yaliweza hata kupata bunduki za Kiingereza ambazo ni mpya, na hazijasambazwa kwa vikosi vyote vya Uingereza.
3.Si kweli kwamba majeshi ya Zimbabwe yalikuwa yanalinda reli ya Beira na hayakushiriki katika vita dhidi ya FRELIMO vs RENAMO. There was so much defections in Frelimos army. Ilibidi Zimbabwe abebe mzigo mkubwa wa kuhakikisha Msumbiji haichukuliwi na Renamo. JWTZ ilikuja kutoa ushirikiano baada ya kifo cha Samora.
1. Zimbabwe hawakuwa na mkataba na UK sijui ulitiwa saini lini unaweza kufafanua hili? Kitu ambacho hakina ubishi ni wanajeshi wa Tanzania ambao walikuwa kule baada ya uhuru anbao walikaa hadi mwaka 1987 na kuanza kupunguzwa pamoja na wahandisi wa simu kutoka Tanzania.
2. Sio kweli kwamba waingereza walishirikiana kuwafundisha para wa kizimbabwe, Zimbabwe walikuwa wanalinda Beira Corridor na mara chache chache sana waliwafuata Renamo kwenye kambi zao na walikuwa wamepewa jukumu la kulinda bwawa la Kabora Basa ambalo ndio lilikuwa target kubwa ili kuikomoa Mozambique. Kama kweli wewe ulikuwa Zimbabwe wakati ule utakumbuka michango iliyokuwa inakusanywa kwenye supermarkets kwa ajili ya shughuli hiyo.
4.Vita ya FRELIMO vs RENAMO ilidumu kwa muda mrefu kuliko vita vya Congo. Sasa imekuwaje vita ya Congo iathiri uchumi wa Zimbabwe kuliko vita ya Msumbiji? Hiyo reli wanayodai Zimbabwe alikuwa akiilinda ilikuja haribika kabisa kwa hujuma za Renamo.
5.Ni nani alikuwa akiwasaidia RENAMO na UNITA kama siyo South Africa na Marekani?
6.Machafuko ya Ndebele yaliisha kwa Mugabe na Nkomo kusaini mkataba wa amani na kuunganisha vyama vyao mwaka 1987. Sasa kwanini miaka 20 down the road watu wanajaribu kutoneka makovu ya matatizo yale? Mugabe alishaomba radhi kutokana na mauaji yale. Inasikitisha sana kwamba BBC,UK,USA na MDC wamegeuza mauaji yale kuwa mtaji wa kisiasa wa kumuondoa Mugabe madarakani.
4. Kwanza hebu tupe miaka ya hizo vita halafu lazima ufahamu kwamba vita ya Mozambique ilikuwa rahisi kwa sababu wanapakana na ile ya Congo ilibidi wawe wana-airlift silaha pamoja na chakula sasa wewe piga hesabu hapo.
5. Kila mtu anafahamu hivyo.
6. Hayo makubaliano hayakuwa mwaka 1987 yalikuwa baada ya hapo. Wewe unampenda Mugabe je, unahabari ameua watu wangapi wasio na hatia? Kwa sababu Mugabe ni kipenzi chako lolote analofanya ni sawa tu. Ni sawa na Dito alivyoua wewe unaona ni sawa tu kwa sababu alikuwa mkuu wa mkoa lakini Klerlu alipouawa na Mwamwindi ilikuwa sawa Mwamwindi kunyongwa na kukaa jela miaka kadhaa.
Wazungu kusema sio hoja sio wazungu wote wenye roho ya korosho, mbona Sweeden waliendelea kuisaidia tanzania wakati IMF na WB walitususa?
7.Zimbabwe imetumbikia ktk tatizo la madeni baada ya kukaribisha ushauri wa uchumi toka nchi za magharibi, IMF na WB. Tukubaliane kwamba hakuna aliyemshikia kiboko Mugabe kuchukua ushauri huo. Vilevile tukubaliane kwamba mpango wa Structural Adjustment Programme[SAP] ulikuwa na athari mbaya sana kwa uchumi wa Zimbabwe.
8.Hii MDC ilikuwa kama juwata ya Zanu-PF. Mwanzoni walikuwa wakipinga sana huu mpango wa SAP na athari zake kwa sekta ya viwanda Zimbabwe. Kitu kinachonishangaza ni jinsi walivyogeuka na kuwa pro-west.
9.Labda niulize swali dogo: Mugabe ametaifisha mashamba, sasa kwanini viwanda hata vile visivyotegemea mazao ya mashambani viathirike?
10.Bado naendelea kuuliza: Inakuwaje nchi yenye ukame, njaa, uhaba wa umeme, uhaba wa mafuta, inflation ya kutisha, ilazimishwe ku-service deni lake kwa vyombo vya fedha vya magharibi. Kwangu mimi hiyo ni hujuma na mauaji.
11. Peter Ngumbulu[Mtanzania] alikuwa Head wa Africa desk mpaka mwaka 2006. Wakati wake ndipo kura ya kuipa Zimbabwe budgetary support ilipigwa. Nchi zote zilipiga kura kwamba Zimbabwe ina-qualify, lakini fedha hizo hazikutolewa kwasababu ya veto ya UK na USA. Ndiyo maana Peter Ngumbulu akalalamika kwamba uamuzi wa kuinyima fedha Zimbabwe ulikuwa wa kisiasa.
12.IMF na WB wakikuwekea vikwazo basi huwezi kukopa popote pale ktk nchi za magharibi. Vilevile hizi kauli mbiu za BBC na Tony Blair zinafukuza wanaotaka kuwekeza Zimbabwe. Kwa kifupi, Tony "amemshika pabaya" Bob.
7. SAP unayoongelea kwa Zimbabwe ni mwaka gani? Na hayo madeni nimeuliza ni ya katika kipindi kipi? Vile vile nani aliwatumbukiza kwenye hiyo kasheshe kama siyo huyu rafiki yako Mugabe?
8. MDC hawakuwa kama JUWATA (Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania) walikuwa ni ZCTU (Zimbabwe Congress of Trade Union) vitu viwili tofauti kabisa. Hawakuwa na uhusiano kama wa JUWATA na CCM. Acha uongo?
9. Uchumi wa Zimbabwe ulikuwa umeshikwa na Wazungu ambao ndio walikuwa wanalima na kufanya biashara zote i.e. Viwandani, kwenye machimbo ya migodi n.k. hawa ndio walikuwa wanadrive economy pamoja na kampuni kama Old Mutual ambayo inamiliki almost 70% ya majengo yote bora pale Harare na miji mingine, hawa ndio walikuwa wanunuzi wa shares kwenye Zimbabwe Stock Exchange ambayo ilikuwa ndio imeshika nafasi ya pili kwa kuwa good bourse in Afrika baada ya South Africa. Hawa ndio waajiri wakubwa Zimbabwe wanunuzi wa Tabaco walikuwa wankuja kununua moja kwa moja kwa mkulima na kukubaliana bei kwenye soko kila mwaka, uliza leo nani tena analima tumbako? Sasa hawa wakiweka silaha chini unakuwa huna kitu. Wengi wao wameacha kulima na kuishi kwenye nyumba zao za mijini na wengine kwenda Zambia na South Africa.
10. Hakuna anayewalazimisha kulipa deni kama hawalipi hawatapewa nyingine ndiyo sheria za kibenki Uki-default hawakupi tena ni uchaguzi wako hizo ni sheria zao waulize WB na IMF.
11. & 12. Unaongelea huyu jamaa 2006 hiki ni kichekesho uchumi wa Zimbabwe ulianza kuporomoka 1994 baada ya kuanza kwenda Congo, Tanzania ni nchi moja iliyowaonya lakini Mugabe alifikiri anafahamu zaidi yetu leo hii anapata umeme wa bure kutoka South Afrika pamoja na mafuta. Sasa UK na USA ndio wenye pesa ni lazima watoe kwa masharti yao sioni unalilia nini hapa, kwani wamekulazimisha kwenda kukopa? Zimbabwe kuna Gold nyingi tu uliza sasa mbona hawachimbi tena? tena wao walikuwa wanazitengeneza wenyewe kuziweka kwenye bullion pale pale Zimbabwe, unakwenda kuwauzia pale benki, walikuwa na kampuni yao ya uchunguzi wa madini yote kule Masasa njia ya kwenda Mutare. Hata WTZ wengi walikuwa wanakwenda kuuza Tanzanite in the 1990 na walikuwa wanalipwa USD 100 kwa carat na wanunuzi wakubwa walikuwa wako Borrodale kwenye kijiji cha SAM Levy karibu na race course.
13.Waafrika tuna tabia ya kusahau kwa haraka sana. Miaka ya 60/70 Tanzania tulivunja uhusiano wetu na Uingereza kwasababu ya wao kukataa kumuwekea vikwazo vya uchumi na kijeshi Ian Smith.
Tanzania hatukuvunja uhusiano na UK huu ni uongo siku zote Tanzania imekuwa ikionekana as bad boy kulinganisha na Kenya kwa sababu ya policies za JK Nyerere (RIP) na hilo sio kwa ajili ya ukombozi tu vile vile utaifishaji wa mashamba ya Mkonge, nyumba za msajili wa Majumba pamoja na Azimio la Arusha na mambo yote tuliyokuwa tunafanya kwa hiyo UK walikuwa hawatupendi na ndio kisa cha wao kuwasaidia zaidi Kenya na vile vile usisahau Tanzania haikuwa koloni la Mwingereza kwa hiyo ilikuwa vigumu wao kuwa na uhusiano mzuri ndio, mpaka leo UK wanaenda na kupendelea Kenya kuliko Tanzania (Bad boy).
14.Uingereza walimbwaga Ian Smith baada ya Nigeria/Obasanjo kutishia kutaifisha visima vya mafuta vya British Petrolium[BP] vilivyoko Nigeria. Bila hivyo, "mechi" kati ya Smith na Zanu/Mugabe ilikuwa imalizwe kwa mtutu wa bunduki, kama ilivyokuwa kwa Mreno kule Msumbiji.
jokaKuu acha uongo Ian Smith kama umesoma vitabu vyake na kuangalia all documentaries kuhusu mazungumzo ya uhuru wa Zimbabwe Lancaster break ilitokea baada ya kuwa na break kwenye ule mkutano na Tongogara (RIP) alipokuwa anaongea na Ian Smith Tongogaraakamwambia kuwa mama yake ndiye alikuwa house girl wa Ian Smith family wakati walikuwa wadogo na yeye Tongogara alikuwa bado mdogo na anamkumbuka, ndio ilipofikia hapo Ian Smith akaona kuwa kumbe anapigana na watu ambao wanamfahamu fika na kusoften msimamo wake lakini ndio jinsi Mugabe aliporudi Mozanbique alipoandaa mpango wa kumu-eliminate kwa njia ambazo aliendelea nazo hata alipokuwa rais (road carnage)
15.Ili Mugabe aondoke kwa kutumia vikwazo vya Uchumi, UK na USA wanapaswa kumtishia Thabo Mbeki na vikwazo. That way, Mbeki atalazimika kumuondoa Mugabe pale, lakini kitakachotokea baadaye only GOD knows.
16.MDC hawataki uchaguzi mwaka 2008, lakini wanataka iundwe serikali ya mpito itakayojumuisha ZANU-PF na MDC. Hilo ndilo sharti kuu la MDC, na Mugabe hataki kulisikia.
15. Sasa Mbeki yanamtokea puani yeye anafadhili mwizi ambaye hataki kukubaliana na wanacnhi wake sio MDC pekee ambao hawantaki hivi sasa natumaini umesikia hata hao ZANU PF wamemkatalia ule mpango wake wa kutawala hadi 2010 tayari kuna mpasuko huko na ataondoka tu hivi karibuni.
Habari za uhakika umeme sasa ni kwa saa nne tu kila siku South Afrika yanawashinda!
16. mbona unageuza Mugabe ndio alikuwa hataki uchaguzi 2008 kwa kubadili constitution lakini amekataliwa unasoma udaku wake mzee?
Mkandara
Kwanza nimpongeze Jokakuu kwa kuongoza maneno yangu. Maanake niliposema Frelimo basi mzee ukarudisha miaka nyuma hadi kabla ya Uhuru miaka ambayo hata wapigania uhuru wa Zimbabwe wenyewe Patriotic Front - PF hawajikusanya.
Mzee wangu tunazungumzia wakati wa uhuru wa Zimbabwe na sio nyuma ya hapo na hiuyo chunvi umeiweka ktk kifungu cha kwanza na cha pili kwa sababu ktk kipindi hicho nilikuwa nakwenda sana Zimbabwe karibu kila mwezi. na nimekaa sana mitaa ile miaka hiyo unayozungumzia.
Inaonyesha habari nyingi unazipata toka magazeti ya hao jamaa sasa nakuomba ipitie hii taarifa ambayo wengi wetu tunaikubalia kama ndo chimbuko la mgogoro wa Zimbabwe na nchi za Magharibi....
http://www.sum.uio.no/publications/p...003_03_lee.pdf
Nitashukuru sana kama utanambia habari hii na maelezo yangu yanatofautiana vipi...
Wewe source yako ni wrong na huyu jokaKuu sioni sababu ya kumpongeza mbabaishaji sijarudisha miaka nyuma wewe unaongelea FRELIMO wakati unachanganya na RENAMO na miaka ya kupata uhuru hebu soma ulichoandika halafu uone mwenyewe jinsi ulivyojichanganya. Zimbabwe walikuwa kule kulinda Beira corridor tu muulize mtu yeyote yule kule Zimbabwe atakuambia hivyo, jokakuu nime-rebutt mambo yake mengi tu, Kama wewe kweli kipindi hicho ulikuwa Zimbabwe niambie mpambe wa Mugabe alikuwa anaitwa nani na alitoka nchi gani? Niwekee kwenye PM. Hii ni kukuonyesha tu kwamba hizi ni information kutoka jikoni sio kama wewe unavyofikiri.Hiyo pdf ni baada ya mwaka 2000 mimi nina original info.