Zimbabwe Election: Progress & Results

Zimbabwe rivals to attend SADC summit




Kama mnakumbuka mkutano wa mwisho wa SADC Mugabe aliondoka kwa kutokubalina na wenzake na kugombana na Mwanawasa, sasa hii ni kwa mara ya kwanza Zimbabwe inakuwa na watarajiwa marais wawili naona mambo yanamwendea kombo BOB Karigamombe Mugabe. Safari hii MDC wamemshika pabaya.
 
Masikini Tsvangirai Africa imebadilika baada ya Kibaki kufundisha Marais wenzake jinsi ya kukaa kwenye madaraka. '

Huyu nafikiri mwisho ataishia kuwa PM asiye na meno.
 

Hawa hawa ndio waliotoka Dar na tamko la kuwa bega kwa bega na komredi Mugabe! Hakuna la maana litakalotokea katika mkutano huo. Wote ni paper tigers! Tungojee kuangalia waafrika wenzetu wakithibitisha ile dhana ya kuwa sisi hatuna tofauti na wanyama. Tumefanya hivyo Rwanda, Sierra Leone, Liberia, Sudan, Mozambique, Angola, Somalia, Uganda, Kenya, Afrika ya Kusini, Zaire na kwingineko itakuwa Zimbabwe? Watakatana mapanga, watatumbua matumbo ya watoto, watawachoma moto jirani zao, watabaka mabinti zao ndipo hao viongozi wetu watakapoona aibu. Mungu alinusuru bara letu. Mungu ainusuru Zimbabwe!
 
Fundi, when you look what is unfolding in Africa on a daily basis, you may end up crying. Inasikitisha na kuumiza sana. Sijui tusaidiwe vipi au tujisaidie vipi.

Unajua I was saying to myself ikitokea leo, Rais wa World Bank na IMF wakiwa waafrika, Katibu Mkuu wa UN akawa Mwaafrika, na OBAMA akawa raisi wa Marekani, I honestly DONT think that the situation on our continent can ever improve!

Sijui nani alituroga! Nimejaribu kutafuta jawabu sipati! What went wrong with US AFRICANS!

But I seriously believe that EVEN WE WANANCHI have contributed to put ourselves in this predicament. Why do we keep on sending back these corrupt and incompetent public officials in powers? we are equally responsible.
 
kwa nini mugabe hataki kuachia madaraka?
hili ndilo swali nililojiuliza kwa kipindi kirefu sana, na hivi majuzi nimekuja kukutana na jibu ambalo kwa kiasi fulani limenifungua.

jibu hilo nililokutana nalo ni kuwa mugabe anamtafuta mtu ambaye atamrithi sera zake haswaa. mugabe anachokipinga maishani mwake ni kuwa kiongozi wa nchi halafu bado unakuwa unaongozwa na wazungu ambao kwa namna 1 au nyingine alipambana na kuhakikisha anawatimua na zimbabwe inakuwa huru.

na kinachopelekea mugabe awaite wapinzani ni vibaraka ni kuwa MT ameweka wazi kuwa moja ya vitu ambavyo atahakikisha anavipa kipaumbele ni pamoja na kuwarudishia wazungu mashamba yao ambayo kwa sasa yapo mikononi mwa wazawa...sasa binafsi sioni sababu ya kumchukia mugabe eti kwa kuwa kawaita wapinzani vibaraka.

ni kweli kuwa viongozi wengi wa africa ni vibaraka wa wazungu, na kinachoelekea kwa baadhi ya nchi za kiafrica ikiwemo tanzania ni kurudisha mamlaka kwa wazungu.

ninaporudisha mawazo yangu nyuma nimegundua hali ngumu ya huko zimbabwe inayolalamikiwa na wengi ni kutokana na vikwazo alivyowekewa mugabe, kwa sababu kabla ya vikwazo zimbabwe ilikuwa na hali nzuri tu ya kimaisha.

ni wazi kuwa vikwazo hivi vilitokana na sera za mugabe kukataa kuwa kibaraka wa wazungu kama ilivyo kwa nchi nyingi za africa ikiwemo tanzania.

mugabe anapinga kwa nguvu zote mambo kama yanayotokea hapa tanzania ya kuchimba madini mwadui na kwenda kuyachekecha uingereza.

kama waliweza kuleta mashine za kuchimbia madini kwa nini washindwe kuleta machekeche ya kuchujia?...anahoji robert "bob" mugabe na kupelekea kuchukiwa na mataifa mengi ya wazungu.

wengi wa watu waliompigia kura kibaraka MT ni wale vijana ambao hawakuwepo siku ile ambayo bob marley alitumbuiza katika sherehe za uhuru wa nchi, na hawa wamepandikizwa sera za uongo kuwa endapo kibaraka MT ataingia ikulu basi wao watakuwa na nafasi za kuingia ulaya kama vijana wengine wa kiafrika.

na wale waliompigia kura mugabe ni wazee wanaojua madhara ya kuwa kibaraka na wazee waligombea uhuru.

na moja ya kauli zake ninazozikumbuka ni alisema "siwezi kuwaachia nchi wapinzani nikiwa hai". na mimi kwa hilo namuunga mkono.
 
MDC wame-arrange national wide strike on Tuesday 15/04/2008 ili kuona matokeo. Agalau yakiwekwa tuone jinsi mzee mzima alivyogaragazwa.
 
kuwashawishi makamanda wa ZDF wamkumbali Tsivangarai ni kazi ngumu kama kushawishi Wamaasai wamteue Laigwaanan ambaye hajatahiriwa wala kupitia jando.

Nakubaliana na wewe mkuu..tena sio Laigwanani tu..pia Orumeki.
 
Zambia summit to tackle Zimbabwe





I can guarantee you that Mugabe will come up with SADC being used by The West just wait. Keep in mind the talks between JK and Bush three days ago.
 
Mugabe kugoma kwenda kushiriki kwenye kikao cha usuluhishi huko Zambia ni ishara kubwa kuwa support yake kutoka kwa akina Mbeki, Kikwete na wengine wachache imeingiwa upupu.

Alichoamua sasa hivi ni 'kulidondokea jambia' lake mwenyewe bila kujali alichofanya kabla ya hapo kihistoria. Liwe na liwe maana hamna anaye muunga mkono kuanzia ndani ya nchi na hata nje.

Wakuu kwenye kikao hicho huko Zambia nao wasingekuwa na tamko lolote la ajabu...sana sana wangesema tu kuwa matokeo ya uchaguzi yatolewe na kila pande iheshimu matokeo hayo. Sasa hapo akina MDC wangesema nini.... maana matokeo tayari yako adulterated. Kugomea uchaguzi mwingine wowote nafikiri ni move nzuri, though inaweza ku-back fire iwapo nzongwe anarudi na kuendeleza uasi wa hali ya juu. Tatizo au niseme uzuri uasi kama huo ukitokea, ndiyo utakuwa mwisho wa Mugabe.... sasa sijui kama huo utakuwa mwisho au mwanzo wa maisha mema kwa Wazimbabwe...

SteveD.
 
Mimi ni Frateline Kashaga, Nipo hapa Mji mkuu wa Finland, nina wiki moja tangia nianze masomo yangu ya PhD in Develöopment Studies-University of Helsinki-Finland, naomba nipewe email ya kitila mkumbo ili niweze kumsaidia maana anapotosha ukweli kuhusu Mugabe,Pia rafiki yangu Kitila inaonekana yeye anakasumba kuwa ili uchaguzi uwe huru na haki ni lazima opposition popote pale dunia ushinde sio kweli halafu , Kitila katika uchambuzi wake unaonyesha mapungufu katika kuangalia nguvu za ubepari dunia, kwa mfano mugabe anachukiwa sana na mataifa makubwa ya kibepari yakiongozwa na marekani na Uingereza, Imperialism inachangia kuaharibu kwa makusudi uchumi wa Zimbabwe, Kwa kweli Mugabe ni mfano wa kiongozi ambaye anaweza kusema No to imperialism
Kitila acha kasumba, wewe ni msomi jaribu kuchambua mambo kwa mapana yake acha ushabiki wa kisiasa.
 

Frateline, natumaini atapata ujumbe akija online, akichelewa sana nenda kwenye Private Message (pm) umwandikie ujumbe. By the way, karibu jamvini na ninakutakia masomo mema huko uliko.


SteveD.
 


Karibu barazani mkuu MSOMI FRATELINE. Ila kwanza kafungue thread ya kwanza kabisa on the rules of the forum! Utapata mwanga zaidi.

Stev D, Mugabe kesharikoroga. Na ukweli ni kwamba his days are numbered sema tuu anaona kwamba itakuwa aibu kuondoka madarakani kwa kushindwa uchaguzi. Kinachotokea hapa kila mtu is watching na he is just postponing problems. To go he will go! Kama akipoteza support ya wenzake wa SADC things will continue tightening up. Infact personally I dont expect much from SADC or AU..ni wale wale....a club of old and hungry MEN of yesterday! na kumbuka kwamba next year South Africa wana uchaguzi na vyovyote vile..its highly unlikely atakayekuwa mrithi wa Mbeki atam-baby sit Mugabe kama Mbeki anavyofanya. Kwa sababu wengi South Africa wako opposed na sera za Mbeki za quite diplomacy....on Zim

We are headed for interesting period in the politics of Africa. Ukiangalia Kenya, Zimbabwe one can not have thought of their current plight. Yaani Africa majanga yanapokezana. Wakati Burundi, Rwanda, Liberia nk wanajaribu kurecover..ndo hawa the so called powerhouse wanaingia kwenye matatizo. Inasikitisha. Lakini yooooote comes back to one thing: Greedy and selfshness.
 

Mkuu Gangchomba pole kwa kuwa gizani. Kwa utangulizi tu naomba nikuambie kwamba mimi nimeishi zimbabwe kwa miaka kumi na nne (85 -99). Nna ndugu, affiliation and links na wazimbabwe. Na toka nimeondoka nimekuwa nikienda huko at least twice a year. Wewe ni mmojawapo wa watu wengi and especially in Africa ambao mmekuwa mkipumbazwa na uongo na uzushi wa Mugabe na wenzake. Well ntaanza kudurusu hoja zako moja baada ya nyingine

1. kuwa mugabe anamtafuta mtu ambaye atamrithi sera zake haswaa
Kumbuka zimbabwe is not a private property of Mugabe and therefore he has no such right. Wanannchi ndio waamuzi wa nini wanataka.

2. kinachopelekea mugabe awaite wapinzani ni vibaraka ni kuwa MT ameweka wazi kuwa moja ya vitu ambavyo atahakikisha anavipa kipaumbele ni pamoja na kuwarudishia wazungu mashamba yao ambayo kwa sasa yapo mikononi mwa wazawa

Hili wewe umelitoa wapi? MT anachosema ni kwamba akichukua madaraka atafanya land auditing kujua wamiliki wa wote wa mashamba waliochukua ni kina nani. kwa taarifa yako most of them ni senior govt officials including some ambao ni ndugu zangu. Pia anakumbusha kwamba kuna watu waliyanunua hayo mashamba kihalali baada ya uhuru na wakamilikishwa kihalali na serikali basi kuna haja ya kufanya reconciliation ili haki ipatikane.

3. ninaporudisha mawazo yangu nyuma nimegundua hali ngumu ya huko zimbabwe inayolalamikiwa na wengi ni kutokana na vikwazo alivyowekewa mugabe, kwa sababu kabla ya vikwazo zimbabwe ilikuwa na hali nzuri tu ya kimaisha.

Ndugu yangu naona kinachokusumbua hapa ni uelewa wa nini hasa maana ya vikwazo. Well vikwazo ambavyo kwa kiingereza inaitwa sanctions viko aina nyingi kwa ufupi tu ntataja baadhi

- Diplomatic sanctions - kutokuwa na ubalozi katika nchi husika au high ranking govt visits - Mfano ni marekani na EU wameimeiwekea cuba vikwazo vya aina hii.

- Trade sanctions - Kutokufanya biashara na nchi husika unless kwa masharti fulani mara nyingi hii huwa pia ni kulinda viwanda vya ndani vya muweka vikwazo. - mfano marekani mwaka 2002iliiwekea China vikwazo vya aina hii kuhusu masuala ya importation ya chuma.

- Economic sanctions - Hii ndio inaweza kuwa aina kubwa na baba ya vikwazo kuliko zote maana hii huwa ni total ban ya kufanya biashara, makubaliano ya kibiashara au hata mipango ya baadae ya uchumi na nchi husika. In short hakuna kuleta hakuna kupeleka. Hii bongo tukipigwa miezi miwili tu na nchi za magharibi tunasurrender. South Africa, Iraq na North Korea zimewahi kuwekewa vikwazo vya aina hii.

- TARGETED SANCTIONS - Hii ndio aina ambayo viongozi wa Zimbabwe wamewekewa (From 2002 na 2004 list ikaongezwa) inawatarget individuals ambao ni viongozi wa Zimbabwe wasiende Ulaya marekani na Australia, wasifanye biashara huko wala kuwa na akaunti. Nia ni nzuri kwa sababu wao walikuwa wanaharibu nchi na kutukana mataifa ya magharibi lakini kila kukicha wanashinda huko.Soma hapa kuona list na taarifa zaidi - http://www.delzwe.ec.europa.eu/en/eu_and_country/targeted_sanctions.htm

Sasa hao akina Mugabe wanataka kwenda kufanya nini kwa ma-imperialists?

4. mugabe anapinga kwa nguvu zote mambo kama yanayotokea hapa tanzania ya kuchimba madini mwadui na kwenda kuyachekecha uingereza
Hii alisema wapi na lini? Ok Hivi ndugu unafahamu processing ya madini au unajisemea semea tu kama baadhi ya magazeti ya Bongo? Nani alikwambia madini hupelekwa nje kuchekechwa? Nadhani wewe unafikiri processing ni kama ile ya wachimbaji wadogo wadogo. Zimbabwe kuna gold - process zote hufanyika nchini, kuna nickel the same way, kuna coal, chuma, diamonds etc.

5. wengi wa watu waliompigia kura kibaraka MT ni wale vijana ambao hawakuwepo siku ile ambayo bob marley alitumbuiza katika sherehe za uhuru wa nchi, na hawa wamepandikizwa sera za uongo kuwa endapo kibaraka MT ataingia ikulu basi wao watakuwa na nafasi za kuingia ulaya kama vijana wengine wa kiafrika.

Hivi wewe ndugu unafahamu kwamba mpaka by 1997/98 wazimbabwe walikuwa wanaingia marekani, australia, canada na nchi zote za ulaya bila visa? Hali iligeuka baada ya kina mugabe kuharibu nchi na hivyo watu kuanza kuondoka kwa fujo in short wale jamaa ni nationalistic kinoma hali ikitulia tu watarudi jkaribu wote kwao. Hivi unataka kuniambia miji ya Harare, Bulawayo, Mutare, Masvingo Gweru n.k WANAKA VIJANA TU??? Maana huko upinzani umezoa kura mijini kwa zaidi ya 70%

6. na moja ya kauli zake ninazozikumbuka ni alisema "siwezi kuwaachia nchi wapinzani nikiwa hai". na mimi kwa hilo namuunga mkono
Hii inaonyesha ni jinsi gani ulivyo mtupu na mpo wengi in my beloved Tanzania. Wapinzani si wananchi?????????
 

Wimbo wa kuwa ni chuki za mataifa ya kibepari ndizo zilizotufikisha sisi waafrika pamoja na wazimbabwe hapa tulipo zimeanza kuchosha. Huyo Mugabe anasemaje no to imperialiasm? Kwa kuwanyang'anya wazungu mashamba na kuwapa rafiki zake? kwa kuwabomolea nyumba wasio na hatia kwa ajili tu wali'support' wapinzani? Kwa kuwatumia wa Korea Kaskazini kuwashika adabu wamatebele ili wasimuunge mkono Joshua Nkomo? Ni Mugabe yupi unayemzungumzia? Wakati umefika wakuangaliana wenyewe na kuwatosa wale ambao wanatufanya kuonekana vichekesho dunia nzima! Kwa bahati mbaya, Mkuu, mawazo kama yako ya kufungia macho maovu yakitendwa na mmoja wetu ndiyo yanayofanya wengine watubeze kwa kusema 'Ndivyo Tulivyo!' Wengi wetu tumechoka.

Amandla!
 

Ujumbe makini sasa muungwana Fundi. Indeed we are tired by these empty and hopeless slogans za akina Mugabe na wenzake!

We are tired. Tufanye nini hawa wazee walielewe hilo? Hivi unajua juzi jamaa aliniandikia email from Harare....anakwambia Yaani Mugabe alikuwa hana anything wakati wa campaign zaidi ya lawama dhidi ya Bush, Brown na Imperialism! Yaani inashangaza na kusikitisha.

Hivi wazee what do you think is the likley scenerio kwa jinsi mambo yanavyoenda Zimbabwe? hata kutoa matokeo? au ni Bush anasababisha?..hahahah..ndivyo tulivyo!
 

Kijana Frateline, kwanza karibu hapa jamvini ambapo huwa tunamkoma nyani gladi. Pili hongera sana kwa masomo yako ya PhD na ninakutakia kila la heri.

Inaonekana theories za imperialism zimekuingia. Hata hivyo ninaamini baada ya kula vitu hapo in the next 6 months utakuwa umeshaanza kuwa pragmatic. Ninasikitishwa sana na kijana kama wewe ambaye uwezo wako naujua ni mkubwa mno wa kuelewa mambo kwa kitendo cha kuendelea kumuona Mugabe ni kiongozi shupavu. Ushupavu gani huo wa kuogopa kushindwa kwenye uchaguzi? Ushupavu gani huo wa kukalia matokeo ya uchaguzi nyumbani kwake? Kijana,get real- Mugabe is a hero turned monster; don't be enslaved by history.

Hapo Finland kuna wazimbabwe wengi sana, ongea nao kwa makini ili uelewe jinsi Mugabe alivyoitenda vibaya nchi yao. Kama wewe unaamini katika utawala wa demokrasia na katika serikali kuwatumikia wananchi, ninaamini utafika mahala utatubu kwa kuunga mkono yale anayoyafanya Mugabe kwa watu wake sasa hivi.

Anyway, kila la heri mdogo wangu, noa kichwa hicho na urudi Tanzania tuendelee na mapambano.

email yangu ni hii: kitilam@yahoo.com

Best wishes
 
Hivi maneno ya NN yanaweza kuwa kweli"waafrika ndivyo tulivyo" . Yaani kuna watu bado wanamuona mugabe ni hero? At least not these days. Guys let us be serious na kam uhero ni namna ile basi Africa tumekwisha na is a shame. Huyu mtu ambaye anajifanya anauenzi uafrica wakati majina ya mitaa na maeneo ya Harare yote ni yale yale ya kizungu, System ni zile zile za kizungu? hata anapokaa yeye kunaitwa Borrowdale, Kuna Malrbrough, St. Marys, Highfield, Mt Pleasant, Greendale, Rotten row ave, Bath st. Kambi kuu ya jeshi inaitwa King George VII. Naweza kuonekana sina pointi kwa hili lakini kumbukeni kama kweli unataka africanisation unatakiwa kubadili fikra, Kuanzia kubadili majina na hili mwalimu alifanikiwa sana. huu uafrika wa Mugabe mimi siuamini kabisa. Maana ana nchi toka 1980 lakini amekuwa bize na imperialists, uafrica kuanzia 2000, why? Jamani siasa za miaka ya 60 zinamsaidia nini mpiga kura aliyezaliwa 1990? Kwa sisi tunaomjua Mugabe kwa karibu kiasi ni kawaida yake kujifanya mwafrika saana, akilemewa na jambo na hasa na wapinzani wake. Don't get fooled Mugabe is a desperate liar and dictator simple. Na anachokieneza sasa ni racism siyo africanism.
 
Mugabe hostage to his own system
"WHEN you join in a political fight by way of an election you must be prepared to lose," President Mugabe told a rally in Nyanga, just three days before the elections.

"You must accept it. If Zanu PF wins you must accept it, if you (MDC) win we will accept," he said.
We almost believed Mugabe's assurances that he was ready to play fair. On Election Day, he reiterated his assertions, saying he would not sleep with a "clear conscience" knowing he had won the elections through rigging.

"There was no language of rigging in this country until the (arrival of the) MDC," he said in Nyanga. That may be true semantically. After all, even as people in Matabeleland and the Midlands were being brutalised under curfews and a state of emergency in the 1980s and were beaten and had their homes burnt down during the 1985 elections for supporting PF-Zapu, nobody cared to raise the flag about rigging or human rights violations.

Mugabe was such a fine guy then. His "principled" stand against apartheid South Africa's brutalities against blacks placed him beyond reproach. It provided him with a convenient cloak for his atrocities against political rivals at home. Up to now, you still get political analysts who talk of that grim era as Zimbabwe's golden hour - low inflation, a good exchange rate and the orgy of consumption!

There was no rigging until Mugabe encroached onto white commercial farms in 2000 and we are all paying the price for that voluntary blindness to what Mugabe has always been.

I am stating this because of the serious claims of "vote-rigging" in what the state media now call a "stalemate" in the presidential election results, notwithstanding Zanu PF's cynical antics about being more sinned against than sinning.

The Zimbabwe Electoral Commission has not disclosed what President Mugabe and MDC-T leader Morgan Tsvangirai each got. It is duplicitous for anyone to speculate about a stalemate, a re-run or a run-off. The simplest thing would have been to let the electorate know the results; a run-off would then suggest itself if no party demanded a recount.

So what became of Mugabe's promise that they would accept the election results? Where are those results? Why has the ZEC stopped the pretence of scrutinising them?

It reinforced another campaign statement by Mugabe just before the elections. He warned Bulawayo residents against voting for the MDC because that would be "a wasted vote… there is no way we can allow them to rule this country. The MDC will not rule this country."

Those who care can rewind to the Defence Forces statement in 2002 and just before the March 29 elections and the essence is clear. How does one reconcile Mugabe's promise to accept the results with this categorical denial of an MDC government?

The contradictions suggest a leader who has become hostage to the patronage system which he initially created to secure his power. There are bigger forces than Mugabe in this electoral debacle and those forces cannot be dealt with through brash Western diplomacy. Now whether there will be an election re-run or a run-off, you can add a lot of blood-letting to the final equation.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…