tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,039
ZIMAMOTO NA UOKOAJI TANGA WAPEWA MAGARI MANNE MAPYA
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, amekabidhi magari manne mapya kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani humo, huku magari mengine manane yakitarajiwa kufika hivi karibuni ili kukamilisha idadi ya magari 16 yatakayoongeza ufanisi wa utendaji kazi wa jeshi hilo.
Soma pia: Moto Kiwanda cha Mafuta na Vipodozi cha Mamujee, Tanga
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Balozi Dkt. Batilda alisema magari hayo ya kisasa yamelenga kuboresha uwezo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika shughuli za uokoaji na kuimarisha utendaji kazi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Aidha, aliwataka Wakuu wa Wilaya na Halmashauri zote mkoani Tanga kusimamia ipasavyo matumizi ya magari hayo na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuchoma mashamba bila kuchukua tahadhari, vitendo ambavyo vimesababisha uharibifu wa mazingira na athari kwenye nguzo za umeme.
Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tanga, Mrakibu Mwandamizi Kattala Issa, alisema magari hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa ADEX, na kwamba wanatarajia kupokea magari mengine manane pamoja na boti ya uokozi kabla ya kumalizika kwa mwaka huu.
Kati ya magari manne yaliyopokelewa: Moja ni ambulance kwa ajili ya kuwahudumia majeruhi katika matukio ya ajali, Rescue Tender ni gari maalum kwa shughuli za uokoaji, Commanding Car hutumiwa na Kamanda wakati wa operesheni za zimamoto.
Wananchi wa Jiji la Tanga wameelezea furaha yao kwa ujio wa magari hayo na wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha huduma za dharura, huku wakiahidi kuyatunza magari hayo ili yadumu kwa muda mrefu.