Zile shuhuda kwenye maombezi ya Manabii

Zile shuhuda kwenye maombezi ya Manabii

Na ni kwanini watu wote ambao huombewa na kupona ni wale wenye magonjwa yasiyoonekana / yasiyo na ushahidi dhahiri (mfano kuumwa kichwa, tumbo, matatizo ya akili nk.)

Sijawahi kuona mtu aliekatika mguu/mkono akapelekwa kwenye maombi kuombewa na mguu ukarudi! Kama Yesu alivyorudisha sikio la yule jamaa.
Umenena vema sana. Utasikia sijui uvimbe tumboni sijui.....! Hakuna hats kiwete mmoja aliyezaliwa kiwete au kipofu aliponywa. Porojo tu za kuwaibia watu pesa kwa kichaka cha sadaka, zaka, matoleo.......
 
Kuna mtu anajtwa nabiu Frank kilawah...huyo ni noma...miujiza ya wazi wazi
Hawana lolote hawa. Niliwahi kupata msala was kupoteza private key ya block chain nikawaendea hawakuwa na msaada wowote. Nikawauliza mbona babii Elisha aliweza kufanya recovery ya lost axe-head, wakaingia mitini. Wapiga dili tu hawana lolote.
 
Haya mambo ni magumu sana mkuu. Mimi nna ndugu yangu tangu mwaka 1995 ame paralyze miguu. Hakuna maombi ambayo hajapelekwa, mafanikio hakuna na always kisingizio kimekua "hana imani"! Hivi mtu mwenye imani anatakiwa aweje?
Wasanii tu. Lakini wapo watu wengi wamepofuka macho ya mioyo yao hawaoni usanii huu. So sad.
 
Unajua kuna uwongo mwingi sana kwenye haya masuala ya kiimani nowdays. Watu wanacheza na psychology yako, wakijua unataka pesa/utajiri na kuponywa certain disease. Kuna mwengine naskia Yuko pale maeneo ya lufungila anaitwa nabii Mussa.

Huyo mafuta yake ya upako yanauzwa Tshs. 15,000/= . Siwezi kuwasemea vibaya watumishi wa bwana Ila kiukweli akili yako changanya na za kuambiwa.

Siku hizi watu hatupendi injili ya kuhusu ufalme wa Mungu tunataka kupokea miujiza ya vitu vizuri vizuri tu.
Kwa hiyo we jomba hutaki kupona ukiwa duniani kama Kuna ugonjwa was kulogwa umetupiwa..au huamini kama Kuna kulogana au uchawi..labda tuanzie hapa..na magonjwa kama hayo unadhani yanaweza kutibika hospitalini jomba..unashauri watu wafanyaje sasa kwa sababu wakienda kule wanapona.
Halaf pia muangalie uhalisia..hivi kweli manabii wanapanga dili na hao woote..na mbona hizo Siri hazifichuki..au wanaambiwa wasiseme..
 
naona umejijibu.
 
Haya mambo ni magumu sana mkuu. Mimi nna ndugu yangu tangu mwaka 1995 ame paralyze miguu. Hakuna maombi ambayo hajapelekwa, mafanikio hakuna na always kisingizio kimekua "hana imani"! Hivi mtu mwenye imani anatakiwa aweje?
Pia inanishangaza, kuna wagonjwa wanaumwa haswaa, yaani ile ya kutisha wanatamani kupona na unavyojua ukiwa mgonjwa unavyokuwa..upo tayari kwa lolote..unaombewa na kumkabidhi yesu maisha maana lkn huponi. Eti huna imani pambav sana hawa watu
 
Hawana lolote hawa. Niliwahi kupata msala was kupoteza private key ya block chain nikawaendea hawakuwa na msaada wowote. Nikawauliza mbona babii Elisha aliweza kufanya recovery ya lost axe-head, wakaingia mitini. Wapiga dili tu hawana lolote.
Duuuh... mkuu na wewe bana..😂😂 yaani ni sawa na mtu apoteze password ya ATM card halafu aende kwa mchungaji amuombee ipatikane 😂😂
 
Pia inanishangaza, kuna wagonjwa wanaumwa haswaa, yaani ile ya kutisha wanatamani kupona na unavyojua ukiwa mgonjwa unavyokuwa..upo tayari kwa lolote..unaombewa na kumkabidhi yesu maisha maana lkn huponi. Eti huna imani pambav sana hawa watu

Labda itakua sisi tulioko hapa ndio hua hatuna imani. Maana kuna watu huwaambii kitu wanakuambia kabisa wameshuhudia kwa macho yao miujiza ikitendeka! Ila kwa upande wangu, familia yangu, ndugu jamaa na marafiki wanaonizunguka, sijawahi kuona. Wanaoumwa wanaumwa, wasipopona wanakufa, wenye shida wapo na shida zao miaka nenda rudi basi ilimradi maisha yanaendelea
 
Huyo ni msabato , jamaa injili Yao imenyooka tatizo kwenye sadaka zao , hatari Sana wao zaka ni 20% na bado michango ya hapa na pale mara sjui makambi full makoro koro
Acha upotoshaji..zaka ni ile ile 10% ya mapato yako halali...hayo mengine ya michango nadhani kila kanisa yapo..mana injili haiwezi kwenda bila kuwezeshwa.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaijua combined budget wewe (Zaka kamili) ...asilimia kumi ni jina tuu lakini ili uonekane umetoa matoleo sahihi inatakiwa angalau 20% .... Means zaka 10% + Sadaka 10% , wanasema sadaka ni ishara ya upendo ,.... Mfano kwenye zaka unatoa moja ya kumi Ila sadaka unaangalia sadaka iliyonona syo kilema , so angalau ianzie kiwango kama cha zaka na Zaid na siyo chini ya hapo ...maana chini ya hapo ni kama umetoa sadaka kilema ... Kama unabisha kamuulize mchungaj wako.... Idea Yao inaweza kuwa ipo vyema tatizo wanaifanya kuwa command hapo ndo tunachengana ,na usipofanya hvi hata uongozi kanisani hupewi, utaambiwa wewe hujamjua Mungu , dini ya Mungu ni kutoa... Mi najua zaka ni command sadaka ni hiari , kuiunganisha sadaka iwe level moja na zaka in term of umuhimu huo ni utapeli .....
Na bado kuna sadaka nyingi nyingi nje ya hyo 20% , makambi ( shukrani), ujenzi kambi, majengo , n.k.... piga mahesabu kama mshahara wako ni 100000 itakutoka sh ngap kwenda kanisani

Issue inakuja zaka yote 10% inaenda conference ,na asilimia 58 ya sadaka inaenda conference , kanisa Mahalia mnabaki na asilimia 42 tuu , inakuwa haitoshi Kwa budget inabid mpeane magori tena huku wao huko conference wakiendesha magari ....
Alaf wanasingizia et watu hawatoi Kwa uaminifu ndo mana kuna michango michango .... Sherehe kama za makambi ni mikakati Tu ya wachungaji kupiga pesa , Kwa taarifa yako kila sku mchungaji akisimama kwenye makambi analipwa 50000 kama posho ndo mana wanakomalia Sana hyo sadaka ....

Mgawanyo wa sadaka na zaka kwenye kanisa upo kuwanufaisha wachungaji na sio makanisa Mahalia ili yafanye vyema.... Matokeo yake mchungaji akisimama kila fungu atakalosoma analielekeza kwenye matoleo..... Hzi dini miyeyusho sana
Injili haiwezi kwenda na kuwafikia walegwa kama haijawezeshwa..toa zaka kamili na sadaka..acha hizo wewe..ndio mana kwenye timu ya Yesu alikuwepo Yuda eskariot ambaye alikua mtunza fedha..unadhani kwa nini walihitaji fedha..acha zako toa sadaka kama huna fanya kazi..sio ku disappoint watu wasitoe kwajili ya kazi ya Mungu..kwanza hata tunachotoa hakiwezi kufikia upendo na mibaraka ambayo Mungu metupatia maishani mwetu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Injili haiwezi kwenda na kuwafikia walegwa kama haijawezeshwa..toa zaka kamili na sadaka..acha hizo wewe..ndio mana kwenye timu ya Yesu alikuwepo Yuda eskariot ambaye alikua mtunza fedha..unadhani kwa nini walihitaji fedha..acha zako toa sadaka kama huna fanya kazi..sio ku disappoint watu wasitoe kwajili ya kazi ya Mungu..kwanza hata tunachotoa hakiwezi kufikia upendo na mibaraka ambayo Mungu metupatia maishani mwetu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungejibu hoja boss , sio kukandiana na kurusha matusi , Iko waz sadaka sio command , ni hiari.... na sio dhambi mtu kutotoa sadaka , kama ni dhambi nipe kifungu , only zaka is command na kutotoa zaka ni dhambi ipo wazi, na huwez kumlazimisha na kumuwekea mtu kiwango cha sadaka kisa umetafsri biblia et ilingane na kafara ya Yesu na izidi na ilingane na kiwango cha zaka , alaf mnakimbilia fungu ooh mtakalolifunga duniani na mbinguni limefungwa , mnataabisha washiriki ...... Kama zaka inapelea njooni na hoja Kwa washiriki wenye kutoa sadaka watatoa ambaye hatatoa basi na sio kuwahukumu na maneno makali yaliyojaa tamaa na uchu wa pesa
 
Mitume na manabii wa zamani walikuwa ni watu wa kuhangaika kutokana na kupata upinzani kutoka kwa wasioamini na watawala waliokuwepo na wengi waliishia kufungwa, kuteswa, kuuawa na hata kuishi kwa kujitenga, lakini wa siku hizi wanashindana kusukuma ndinga kali kama hammer, vogue na kukaribishwa kwenye hafla na watawala kupewa bahasha zilizonona....kuna mmoja huko mbagala ibada ilikuwa haikamiliki bila kumsifia jiwe na nimemsikia ameanza kuhamishia mapambio kwa mama, ukiwa na msimamo wako utasikia ana kiburi cha uzima, sijui kiburi cha usomi....
 
Asilimia kubwa ya watu wanaojiita walokole either wana matatizo ya akili au wanna maovu ya kutisha wanajificha kwenye kivuli cha ulokole
Asee mi nimewanyanyulia mikono[emoji119][emoji119]
 
Back
Top Bottom