Zigo la rushwa ya rada kichwani kwa Chenge
· Kampuni iliyouza yakiri kutumia rushwa
· Ni BAE, yatozwa faini ya dola milioni 400
· Mpira warudishwa kwa serikali ya Tanzania
Kampuni ya British Aerospace (BAE Systems) ya nchini Uingereza iliyoinyonya Tanzania kwa kuiuzia rada kwa bei kubwa kulinganisha na thamani yake halisi, imetozwa faini ya dola za Marekani milioni 400 (Sh. bilioni 535), baada ya kukiri kutumika rushwa katika ununuzi wa rada hiyo.
Rada hiyo ilinunuliwa na Serikali ya Tanzania kwa Paundi milioni 28,000 (Sh. bilioni 70), baada ya baadhi ya mawakala kushirikiana na kampuni hiyo kuongeza thamani ya bei ya rada hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana jana jioni kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), sehemu ya fedha za faini hiyo, zimeamriwa kurejeshwa Tanzania kutokana na kununuliwa kwa rada hiyo.
Taarifa hiyo ilimkariri Mkurugenzi wa BAE Sytem, Dicky Oliver, akikiri kuwa walifanya makosa kutumika rushwa katika ununuzi wa rada hiyo, lakini akasema faini waliyotozwa ni kubwa mno, ambayo haijawahi kutokea katika historia ya Uingereza.
Hata hivyo, taarifa hiyo ilimkariri Oliver akisema kwamba, amefurahishwa na adhabu hiyo kwa vile itakuwa imefunga mjadala unaohusu kashfa hiyo.
Alisema amejifunza kutokana na adhabu waliyopewa na kuongeza kuwa wanaiachia serikali ya Tanzania kuwachukulia hatua watakayoona inafaa watu waliohusika katika kashfa hiyo. Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM), anatuhumiwa kuhusika na kashfa hiyo alipokuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) wakati rada hiyo inanunuliwa.
Gazeti la The Guardian la Uingereza liliwahi kuandika kuwa, katika uchunguzi wa Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa (SFO) ya Uingereza, iligundulika akaunti moja inayohusishwa na Chenge ikiwa na zaidi ya dola za Marekani milioni 1 (Sh. bilioni 1.2) iliyopo kwenye Kisiwa cha Jersey, nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, SFO ilimchukulia Chenge kuwa mtu anayeweza kuwa shahidi muhimu katika uchunguzi wa zabuni ya ununuzi wa rada hiyo.
Gazeti hilo liliandika kwamba, SFO inatarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo ili kuangalia iwapo zina uhusiano na zile zinazoaminika kutolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada hiyo mwaka 2002.
Uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa moja ya mambo yaliyokuwa yanafuatiliwa ni kujua iwapo fedha zinazoaminika kuwa za Chenge, zina uhusiano na zile zilizotoka katika Kampuni ya BAE System.
The Guardian katika habari yake hiyo, liliripoti kuwa, taarifa hizo zinakuja ikiwa ni miaka mitatu tangu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kwa kushirikiana na SFO na taasisi za uchunguzi za Uswisi na Jersey zilipoanza kuchunguza kuhusu kashfa nzima ya ununuzi wa rada.
Gazeti hilo lilimkariri Chenge akikiri kwamba fedha hizo ni zake, ambazo baadaye alipohojiwa na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam aliziita kuwa ni "Vijisenti".
Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, alipoulizwa na waandishi wa habari mjini Dodoma siku moja baada ya taarifa za Chenge kumiliki fedha hizo, alisema "Hata angeuza ng'ombe wake wote walioko Bariadi asingeweza kuwa na fedha kiasi hicho".
Wakati akihojiwa na gazeti hilo, Chenge alitumia fursa hiyo kukanusha kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha hizo na kashfa nzima ya ununuzi wa rada, uliofanywa wakati yeye akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
"Jambo la wazi linalotaka kuonekana hapa ni kwamba mimi nilipokea kwa lengo la kujinufaisha mwenyewe fedha za rushwa kutoka BAE. Huu ni uongo," alisema Chenge.
Aidha, gazeti hilo lilimkariri Chenge akisema kuwa, wakati rada hiyo ilipokuwa ikinunuliwa, yeye alihusika kwa kiwango kidogo sana katika mchakato mzima, kwani jambo hilo lilishughulikiwa na wizara nyingine na uamuzi ukaidhinishwa na Baraza la Mawaziri.
Alilazimika kujiuzulu uwaziri wa Miundombinu, baada ya kutolewa tuhuma dhidi yake za kumiliki kiasi hicho kikubwa cha fedha.
Takukuru kwa upande wake imekuwa ikieleza umma kuwa inasubiri kupata maelekezo kutoka SFO ili ichukue hatua dhidi ya Chenge.
Wakati Takukuru ikieleza hayo, Waziri Sophia alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni akisema kwamba, SFO imemsafisha Chenge.
Hata hivyo, baadaye taasisi hiyo ilikana kumsafisha mwanasiasa huyo dhidi ya kashfa hiyo.
Serikali ya awamu ya tatu iliinunua rada hiyo ya gharama kubwa licha ya kutahadharishwa na aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Uingereza, Clare Short, kuwa rada hiyo ilikuwa ya gharama kubwa kwa nchi maskini kama Tanzania.
CHANZO: NIPASHE