Waziri wa Madini: Toyota Land cruiser STK 327 (Tume ya madini) hii gari inatumika vibaya kuokota Rushwa na kuwanyanyasa wachimbaji wadogo Chunya

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,828
21,457
Leo ninatuma namba ya gari nikijiamini kuwa gari hiyo inamilikiwa na Tume ya madini.

Huko gari liliko Kila siku linatumika kukusanya rushwa na kusumbua wachimbaji wadogo.

Gari Hilo linafanya ukusanyaji wa rushwa usiku na mchana, siku za kazi na siku za sikukuu.

Bosi wa Tume ya madini Chunya pokea ujumbe huu na utambue kuwa hustahili kufanya na kusimamia watanzania wanachofanyiwa.

Kila siku ni kufunga karasha za wachimbaji wadogo Kwa kuweka ribbon nyekundu na bila kutoka 700,000 ribbon nyekundu haifunguliwi.

Kwa siku gari Hilo linazunguka kufunga makarasha zaidi ya 20 .

Tume ya madini tunaomba magari ya ukaguzi yatembee na dispatch book ili mtu akifungiwa karasha asainishwe na aelezwe sababu za kufungiwana faini ziwe wazi zijulikane.

Unyanyasaji ni mkubwa sana wilaya ya Chunya.

Gari hiyo litembeena vyombo vya ulinzi na usalama kwani Sasa linatembea na afisa wa Tume wawili kukusanya fedha za kupeleka kwao kwakuonea wachimbaji wadogo.

Kilio hiki kimfikie Katibu Mkuu wizara ya Madini.

Wachimbaji wanachimba madini kwenye maeneo yenye Leseni za utafiti huko Chunya na yametengwa Kwa ajili ya wachimbaji wadogo, ila hawataki kuondoa leseni ya utafitiili wachimbaji wawe huru kupewa leseni zao walizoomba kwenye maeneo ya utafiti japo serikali ilikwisha kubali, wao wanazunguka kukusanya rushwa TU.

Tunaomba waziri afuatilie jambo hili.
 
Badala ya kulalamika,mngeboresha Kwanza miundo mbinu ya mashimo yenu mnakochimbua ayo madini.

Mnaacha mashimo wazi,mnaendelea kuchimba na mnajua kabisa huu Ni msimu wa mvua, na lolote linaweza kutokea yakaporomoka.

Sasa Mnataka Mpaka mfukiwe na vifusi ndo mje kulalamika kwamba serikali Ina zembea haikuchukua hatua?

Kisha muanze kutusumbua rambirambi
 
Badala ya kulalamika,mngeboresha Kwanza miundo mbinu ya mashimo yenu ya migodi maana huu Ni msimu wa mvua.

Mnataka Mpaka mfukiwe na vifusi uko migodini ndo mje kulalamika kwamba serikali Ina zembea haikuchukua hatua?
CC: Makonda
 
Kwa hiyo hizo rushwa wanazopokea hao watu wa madini ndio zinaboresha hayo mashimo, au Sio!?
 
Tatizo haki vifo vya wachimbaji wadogo vinatokea kwenye maeneo yaliyokuwa naleseni za utafiti na serikali ilisha toa maelekezo zigawiwe wachimbaji wadogo.
Sasa huku wanaingia kama wakimbizi na ili hali nchi ni Yao.
Mwenye namba ya Makonda ili itolewe Kwa wachimbaji ili waeleze rushwa ilivyozidi kwenye uchimbaji mdogo .
 
Leo ninatuma namba ya gari nikijiamini kuwa gari hiyo inamilikiwa na Tume ya madini.

Huko gari liliko Kila siku linatumika kukusanya rushwa na kusumbua wachimbaji wadogo.

Gari Hilo linafanya ukusanyaji wa rushwa usiku na mchana, siku za kazi na siku za sikukuu.

Bosi wa Tume ya madini Chunya pokea ujumbe huu na utambue kuwa hustahili kufanya na kusimamia watanzania wanachofanyiwa.

Kila siku ni kufunga karasha za wachimbaji wadogo Kwa kuweka ribbon nyekundu na bila kutoka 700,000 ribbon nyekundu haifunguliwi.

Kwa siku gari Hilo linazunguka kufunga makarasha zaidi ya 20 .

Tume ya madini tunaomba magari ya ukaguzi yatembee na dispatch book ili mtu akifungiwa karasha asainishwe na aelezwe sababu za kufungiwana faini ziwe wazi zijulikane.

Unyanyasaji ni mkubwa sana wilaya ya Chunya.

Gari hiyo litembeena vyombo vya ulinzi na usalama kwani Sasa linatembea na afisa wa Tume wawili kukusanya fedha za kupeleka kwao kwakuonea wachimbaji wadogo.

Kilio hiki kimfikie Katibu mkuu wizara ya madini.

Wachimbaji wanachimba madini kwenye maeneo yenye Leseni za utafiti huko Chunya na yametengwa Kwa ajili ya wachimbaji wadogo, ila hawataki kuondoa leseni ya utafitiili wachimbaji wawe huru kupewa leseni zao walizoomba kwenye maeneo ya utafiti japo serikali ilikwisha kubali, wao wanazunguka kukusanya rushwa TU.

Tunaomba waziri afuatilie jambo hili.
Wanaweza kuta wanakusanya wanapelekea Ikulu,
 
Hii gari na bosi wake huku Chunya, wachimbaji wadogo hawataki kuiona ikizungukia mislo na makarasha tena.

CCM wilaya ya chunya, hii Gari inawaharibia kura na uchaguzi mkuu 2024
 
Ninaishukuru Jf , sana.

Tume ya madini imechukua hatua nasi wananchi na wachimbaji wa madini tumeridhika na hatua ya kusimamisha unyama ulikuwa unafanywa na Gari hili na mabosi wake.

Tunashukuru Tume ya madini Kwa kusikia kilio cha wachimbaji wadogo wadhahabu Chunya.

Tunaomba gari hili nibakie liliko kwani lilisababisha usumbufu, wizi, rushwa na ukimbizi Kwa baadhi ya wachimbaji wadogo.
 
Walifika mpk kwangu ifwenkenya hao majambazi na STK yao
 
Back
Top Bottom