Ushauri: Kuwe na List maalumu ya wala rushwa na wapokea rushwa

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,749
Rushwa ni tatizo kubwa sana na imefika wakati wa kuwa na daftari maalumu la wala rushwa wote na watoa rushwa wote ambao wamepelekwa mahakamani na kuthibitishwa.

Hiyo list iwe ma majina na namba zao za NIDA. Lakini watoa mikopo na huduma nyingine wawe wanaweza kuangalia hiyo database kwa kutumia NIDA zao.

Rekodi zao zikae kwa miaka mitano lakini kuwe na vitu vya kijamii kama ambavyo wafanye kwa muda huo ili kutolewa kwenye hii list.

Vitu hivyo ni pamoja na kuchukuwa mafunzo ya uzalendo, kutokuwa na kesi yeyote mbaya kwa miaka 5 na kupata watu 5 ambao wanaweza kuthibitisha hawa walarushwa na watoa rushwa wamebadilika.
 
Back
Top Bottom