Zifahamu aina 7 za limbwata

Mimi wanawake wote waliojarbu kuniwekea hyo Juju a.k.a Limbwata walidunda.
Mmoja alikuja kuniambia kua Mimi Ni kiboko alitembea kwa waganga Zaid ya watatu wakimpa dawa zinadunda..!

Mwingine alipeleka Jina langu na picha kilichowapata yeye na Mganga hawatasahau.
Wakiweka Jina kwa Rada halisomi signal error ..!
Babu Yangu Fundi Sana aliniwekea Kinga nikiwa bado mtoto kichanga kabisa..!
 
Wanawake / Mabinti baadhi wamekuwa watumiaji wazuri wa limbwata kama sehemu ya kuongeza chachu ktk mahusiano yao ya mapenzi.

Zifuatazo ni baadhi ya teknolojia maarufu ama niseme pendwa za limbwata. Waweza kuongeza yoyote ile uijuayo:

KINYAMA : Katika hili, kipande kidogo cha nyama mfano wa mnofu mmoja wa “mshikaki” huwekwa katika uke wa mtaka tiba, kwa muda wa siku kadhaa kulingana na masharti ama maelekezo ya mtaalam husika “fundi”, baadae kinyama hiki hupikwa na sehemu nyingine ya kitoweo kama mboga na kuliwa.

Mlengwa wa limbwata ataathirika mara tu baada ya kula mlo uliohusiha mboga yenye kinyama hiki! Wanaoipenda njia hii wanasema ni ngumu sana kumuagua mwanaume alielishwa kinyama.

MAJI YA MCHELE : Hii ni aina nyingine ya teknolojia ya limbwata. Ni kwamba kwa kutumia njia hii, maji ya kawaida hupelekwa kwa mtaalam kwa ajili ya kazi husika, na kisha maji hayo hurudishwa nyumbani, mwanamke mhusika huyatumia maji ya dawa haya kuoshea uke wake na baadae huyatumia kuoshea mchele ama hata kupikia kabisa!

Limbwata hili hufanya kazi kwa mlengwa baada ya mlengwa kula chakula kilichopikwa kwa maji tajwa! Wanaoipenda njia hii wanasema ni ngumu sana kumuagua mwanaume alienyeshwa maji hayo, na kwamba ili kumuagua lazima apatikane fundi Yule Yule aliefanya yake!

KISOMO : Nyingine. Hii haisemwi sana, ni kama siri kubwa, huwa haijulikani hasa ni aina gani ya “kisomo” hufanyika lakini wateja na wafuasi wa limbwata la aina hii wanakiri kuwa, mwanaume aliesomewa huwa ni zaidi ya kondoo, kwa maana ya kuwa maisha yake yote yaliyobaki yanakuwa ni yale ya “ndio mzee” kwa mwanamke alietengeneza!

Wanaoipenda njia hii wanasema sio nzuri sana kwa vile fundi mwingine yoyote anaweza akafanya kisomo kinyume

KIFARANGA : Hapa mwanamke mhitaji huagizwa na fundi kupeleka kifaranga, na mara nyingi ni cha kuku.

Fundi humfanyia kazi Kifaranga huyu katika karakana yake, namna fundi anavodili na kifaranga hiki ndio ndio kazi halisi ya kumuinamisha mme ama mpenzi wa mtu, kifaranga huyu hubaki ktk himaya ya fundi kwa maisha yake yote, na namna kifaranga huyu anavolelewa na huyu fundi, na kufuata anavotaka mfugaji, ndio hivo hivo mlengwa atakavopelekwapelekwa! Njia hii inachangamoto moja kubwa, usalama na uhai wa kifaranga huwa ni tatizo.

JINA KUNING’INIZWA JUU YA MTI : Hii inafanana na kisomo. Tofauti ni kwamba, baada ya fundi kufanya kazi yake, huku jina la mlengwa likiwa limenuiwa, karatasi lililoandikwa jina hili (jina la mwanaume mlengwa) huenda kuning’inizwa katika moja ya mti mrefu ambao ni sharti uwe mbali na wanapoishi wapenzi ama wanandoa hao, wakati mwingine inahusisha mkoa mmoja hadi mwingine!

Wanasema kusipokuwepo na upepo, mwanaume huwa mjanja mjanja, lkn upepo ukivuma kidogo tu, mwanaume huyu akili huruka na kumuwaza aliemtengeneza! Ili upone kutoka katika limbwata hili, lazima huu mti utafutwe na kikaratasi kikatwe, ndio utapona!

KABURI LA MTOTO : Hapa kuna vitu hufukiwa, kama ilivo limbwata la hapo juu, limbwata hili linahusisha madawa na majina ya mlengwa. Kaburi husika hutafutwa maeneo ya mbali sana.

Madawa na majina ya mlengwa hufukiwa katika kaburi la mtoto. Hapa huponi mpaka kaburi lipatikane na kazi ifanyike hapo!

UNYAYO, KUCHA AMA KINYWELEO : Hapa kuna mchanganyiko wa ufundi unaotumika. Wapo wanaotumia mchanga wa unyayo, wapo wanaotumia kipande cha nywele za sehemu za siri, wengine hutumia hata chupi ya mlengwa.

Yoote kwa yote ni kwamba fundi atadili na mlengwa kutumia aina mojawapo ya nyenzo hizi! Mafundi wengi inasemekana ni wataalamu wa kuagua wahanga wa njia hii!

ANGALIZO.
WANAUME KUWENI MAKINI NA HALI KAMA HIZI NA IKIWA WEWE NI WA YES UJUE TAYARI WASHAKUWEZA
Mpenzi wangu popote ulipo kama limbwata nipe nijiwekee mwenyewe kama dozi ni mara tatu kwa siku ntajiwekea tatizo mnazidisha hadi inakua keroo
 
Mimi wanawake wote waliojarbu kuniwekea hyo Juju a.k.a Limbwata walidunda.
Mmoja alikuja kuniambia kua Mimi Ni kiboko alitembea kwa waganga Zaid ya watatu wakimpa dawa zinadunda..!

Mwingine alipeleka Jina langu na picha kilichowapata yeye na Mganga hawatasahau.
Wakiweka Jina kwa Rada halisomi signal error ..!
Babu Yangu Fundi Sana aliniwekea Kinga nikiwa bado mtoto kichanga kabisa..!
Huyo babu bado yupo hai hadi leo na mimi nifanye taarifa???
 
Mimi wanawake wote waliojarbu kuniwekea hyo Juju a.k.a Limbwata walidunda.
Mmoja alikuja kuniambia kua Mimi Ni kiboko alitembea kwa waganga Zaid ya watatu wakimpa dawa zinadunda..!

Mwingine alipeleka Jina langu na picha kilichowapata yeye na Mganga hawatasahau.
Wakiweka Jina kwa Rada halisomi signal error ..!
Babu Yangu Fundi Sana aliniwekea Kinga nikiwa bado mtoto kichanga kabisa..!
uongo mtupu, na hao waganga labda wale wapiga hela sio halisia.
 
Kuna mtu nataka nimroge tena huyu namchanganyia quote ya kaburi la mtoto mchanga naenda kuifanyia kigoma, ya kisomo naenda kilwa na nyingine nitnafanyia tanga yaani nachanganya mizim na majini mshenzi yule aonje maumivu maana anajifanya hasikii
 
Mimi wanawake wote waliojarbu kuniwekea hyo Juju a.k.a Limbwata walidunda.
Mmoja alikuja kuniambia kua Mimi Ni kiboko alitembea kwa waganga Zaid ya watatu wakimpa dawa zinadunda..!

Mwingine alipeleka Jina langu na picha kilichowapata yeye na Mganga hawatasahau.
Wakiweka Jina kwa Rada halisomi signal error ..!
Babu Yangu Fundi Sana aliniwekea Kinga nikiwa bado mtoto kichanga kabisa..!
Sasa jiandae nina babu yangu ukambani huko. Nitakunyoosha.

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Mie limbwata langu Mahaba tuu...

Mtu fudenge analegezewa macho...
Sauti inalegezwa na kutoka kwa vituo...
Huku anadekezwa kwa Mahaba Matata.....

Aahahahahhahaaaa akijastuka amaliza wiki nzima kwangu .

K’ Platinum.
Naam
 
Back
Top Bottom