Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,273
- 6,637
Zile tetesi kuwa Tanzania ina mahusiano mabaya na nchi za magharibi zimeonekana sio za kweli. Maana ziara aliyofanya waziri kabudi imezaa matunda.
Ziara hii pia imechochea kuanza kwa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta toka Hoima Uganda hadi Tanga nchini Tanzania.
Mradi ambao utazalisha ajira 4700 na kulipatia taifa la Tanzania mapato makubwa yatayotokana na kusafirisha mafuta kupitia bomba hilo.
Pia kampuni ya Total itajenga viwanda vya kusafishia Petrol . Mbali na haya waziri kabudi alionana na jumuia ya wafanya biashara ya Ufaransa-Medef. Alikutana pia na wadau wa utalii ambao watakuja kuwekeza hapa nchini.
Hivyo ni wazi kuwa Taifa letu bado lina mahusiano mazuri ya kidiplomasia tofauti na walivyodai baadhi ya wadau wa siasa hapa nchini.