Zebra Crossings in Dar- Whats the point??

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,259
1,195
Baada ya miaka mingi, nilirudi bongo juzi and I must say nilinusurika kugongwa na magari mara mbili wakati navuka barabara kwenye zebra crossing. Baada ya siku kadhaa na kulizoea jiji nikagundua kwamba hizo crossings zipo tu kama mapambo na hakuna dereva anayeziheshimu. Ukitaka kuvuka barabara ni lazima usubiri hadi kuwe hakuna magari ndo uvuke hata kama uko kwenye zebra! Hii ina maana kwamba hakukuwa na haja ya kupoteza hela kuweka hii michoro na you might as well vukia barabara popote tu ambapo unaona ni safe.

Ikumbukwe kwamba kwenye zebra crossing ni sehemu salama ambayo mwenda kwa miguu ana haki ya kuvuka barabara na dereva anapaswa kusimama kama kuna watu wanaosubiri kuvuka. Kama wanaosimamia sheria za barabarani wameshindwa kuwabana madereva waheshimu alama za barabarani na kuhatarisha maisha ya waendao kwa miguu, ni bora kabisa waondoe hizi alama barabarani manake zinaweza zikaku mislead ukajikuta umegongwa......

Kana-Ka-Nsungu
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
85,460
2,000
Nini kwenye crosswalk....watu wana run red lights kama vile hazipo!

Ukiwa unaendesha gari halafu ukafika kwenye stoplights huku upande wako imewaka taa ya kijani basi slow down and proceed with caution.

Madereva wa Dar huwa wanakatiza tu saa ingine bila kujali rangi ya taa iliyowaka upande wao.

Kwa ujumla watu wanaendesha kwa kufuata sheria zao wenyewe na si zile za usalama barabarani.

Pia, kwenye roundabouts nyingi hakuna alama zinazoonyesha ni yupi mweye right of way na yupi anatakiwa ku yield. Yaani ni shaghalabaghala tu.

Watu wakifika kwenye hizo roundabouts ni kuchomekeana tu.

Kwa kweli uendeshaji wa Dar kwa kiasi kikubwa ni hatarishi sana.
 
Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
4,416
2,000
Lawlessness state, imelelewa imekuzwa na sasa imezaa,,, ni mambo ya ajabu sana na ujinga nimewahi kumzaba kibao dereva mmoja alimgonga mtoto sema hakuuumia sana na kale katoto kalikua kanapita kwenye zebra,yaani ni ujinga mtupu watu wanajifanyia tu wanavyojisikia...
 
Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,259
1,195
Nini kwenye crosswalk....watu wana run red lights kama vile hazipo!

Ukiwa unaendesha gari halafu ukafika kwenye stoplights huku upande wako imewaka taa ya kijani basi slow down and proceed with caution.

Madereva wa Dar huwa wanakatiza tu saa ingine bila kujali rangi ya taa iliyowaka upande wao.

Kwa ujumla watu wanaendesha kwa kufuata sheria zao wenyewe na si zile za usalama barabarani.

Pia, kwenye roundabouts nyingi hakuna alama zinazoonyesha ni yupi mweye right of way na yupi anatakiwa ku yield. Yaani ni shaghalabaghala tu.

Watu wakifika kwenye hizo roundabouts ni kuchomekeana tu.

Kwa kweli uendeshaji wa Dar kwa kiasi kikubwa ni hatarishi sana.
NN heshima yako mkubwa, long time man.

Kweli hiyo ya traffic light nayo niliishuhudia mara nyingi tu, yani kama ulivosema hata kama ngoma ni green kwako una proceed with caution. Lakini kwenye round about mimi nilivofunzwa na muingereza hapa (na najua nyumbani tunatumia system zao hawa jamaa) ni kuwa unampa priority mtu aliyeko kulia kwako and am sure hii ni kitu ambayo madereva wengi hawaijui. Tatizo jingine kubwa pia ni matumizi ya honi yasiyo lazima, yani ni kama vile watu wanaendeshea honi, mtu akiwa ana overtake honiii, foleni ikiwa haisogei kila mtu anapiga honi, mtu akimuona msichana mzuri anapita pembeni anatwanga honii tu, kero tupu
 
Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
49,965
2,000
kama ulikuwepo vile... Mimi nilichogundua niliporudi tz ni kuwa madereva wa Tanzania wana roho mbaya sana. Akikuona unakatisha bara bara yeye ndio anaongeza speed ya gari ili akuwahi . Wana roho ya kinyama sana.
 
Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,259
1,195
kama ulikuwepo vile... Mimi nilichogundua niliporudi tz ni kuwa madereva wa Tanzania wana roho mbaya sana. Akikuona unakatisha bara bara yeye ndio anaongeza speed ya gari ili akuwahi . Wana roho ya kinyama sana.
SI, on the other hand nafikiri madereva wengi wanakua frustrated kwa muda wanaokaa kwenye foleni so akipata kaupenyo ka kunyagia wese, anakanyaga tu, hajali cha mwenda kwa miguu wala muendesha baiskeli.
 
Anheuser

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
1,950
1,225
kwenye roundabouts nyingi hakuna alama zinazoonyesha ni yupi mweye right of way na yupi anatakiwa ku yield. Yaani ni shaghalabaghala tu.
Hapo unakosea kidogo, kwenye circle sheria inajulikana na haina haja ya vibao, kama ambayo kwenye blind intersection hakuna vibao vinavyosema nani apite kwanza kwa sababu, again, sheria inajulikana.

In a circle you yield to the vehicle already in the circle, and you enter the circle going anti-clockwise, that is "keep left."
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
85,460
2,000
Hapo unakosea kidogo, kwenye circle sheria inajulikana na haina haja ya vibao, kama ambayo kwenye blind intersection hakuna vibao vinavyosema nani apite kwanza kwa sababu, again, sheria inajulikana.

In a circle you yield to the vehicle already in the circle, and you enter the circle going anti-clockwise, that is "keep left."
Zipo roundabouts zenye stop signs/yield signs na kwa maoni yangu hizo signs zinasaidia sana kuliko kutokuwepo.
 
PrN-kazi

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
2,896
1,225
hii inaonyesha ni namna gani wafanyakazi wengi hawatekelezi ipasavyo majukumu yao ya kazi waliopangiwa; Askari wa usalama barabarani mojawapo ya majukumu yao ni kuhakikisha watumiaji wa barabara wanatii na kuheshimu alama za barabarani ikiwemo na Michoro ichorwayo juu ya sakafu ya barabara (e.g Zebracrossing) lakini wanalala tu wakisikia Wapenda maendeleo wanataka kufanya maandamano ya amani wanakuwa wachungu. Polisi kwakweli hawakizi haja.
 
Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,259
1,195
Hapo unakosea kidogo, kwenye circle sheria inajulikana na haina haja ya vibao, kama ambayo kwenye blind intersection hakuna vibao vinavyosema nani apite kwanza kwa sababu, again, sheria inajulikana.

In a circle you yield to the vehicle already in the circle, and you enter the circle going anti-clockwise, that is "keep left."
Tatizo kubwa la madereva wengi bongo ni kutojua sheria na sababu kubwa ni- leseni za kununua au kutokua na leseni kabisa, hata sisi tunaoandika humu wengi hatujui sheria za barabarani so kama unajua sheria yoyote unayoona itasaidia imwage tu hapahapa mkuu..
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
85,460
2,000
Tatizo kubwa la madereva wengi bongo ni kutojua sheria na sababu kubwa ni- leseni za kununua au kutokua na leseni kabisa, hata sisi tunaoandika humu wengi hatujui sheria za barabarani so kama unajua sheria yoyote unayoona itasaidia imwage tu hapahapa mkuu..
Mimi nadhani hata kwenye hizo roundabouts kungekuwa na alama kama hizi za ku yield ingesaidia sana.
 
cacico

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
8,377
1,250
tulikuwa kwenye jam ya morroco, driver mbele yangu aliachia brake na gari ilirudi nyuma without him noticing!! akanigonga taa ya kulia ikavunjika, nikashuka kwenye gari kwamba tulipane, akanijibu japo kuna jam, ningetakiwa kukaa 10metres away from him! hubby wangu alikuwa amekaa tu kwenye gari anamsikiliza pumba zake, ghafla alishuka akamnasa vibao, akamuuliza unalipa au twende polisi?? akatoa pesa ya taa hapo hapo na tukaondoka!

so its true drivers wapo rough, na wanawaonea zaidi wakina mama, lol!
 
pererge

JF-Expert Member
Nov 8, 2012
570
225
mojawapo ya round about zisizokuwa na adabu ni ile ya pake kwenye mnara wa askari kwa upande wa kutokea posta mpya na wakosa adabu ni madereva wa daladala wanaotokea posta mpya wao huingia tu hata kama kuna gari limeshaingia kwenye nzunguko, this shows how primitive most of daladala driver are!
NN heshima yako mkubwa, long time man.

Kweli hiyo ya traffic light nayo niliishuhudia mara nyingi tu, yani kama ulivosema hata kama ngoma ni green kwako una proceed with caution. Lakini kwenye round about mimi nilivofunzwa na muingereza hapa (na najua nyumbani tunatumia system zao hawa jamaa) ni kuwa unampa priority mtu aliyeko kulia kwako and am sure hii ni kitu ambayo madereva wengi hawaijui. Tatizo jingine kubwa pia ni matumizi ya honi yasiyo lazima, yani ni kama vile watu wanaendeshea honi, mtu akiwa ana overtake honiii, foleni ikiwa haisogei kila mtu anapiga honi, mtu akimuona msichana mzuri anapita pembeni anatwanga honii tu, kero tupu
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
85,460
2,000
mojawapo ya round about zisizokuwa na adabu ni ile ya pake kwenye mnara wa askari kwa upande wa kutokea posta mpya na wakosa adabu ni madereva wa daladala wanaotokea posta mpya wao huingia tu hata kama kuna gari limeshaingia kwenye nzunguko, this shows how primitive most of daladala driver are!
Afadhali wewe ni shuhuda wa hilo.
 
Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,311
2,000
Pia, kwenye roundabouts nyingi hakuna alama zinazoonyesha ni yupi mweye right of way na yupi anatakiwa ku yield. Yaani ni shaghalabaghala tu.

Watu wakifika kwenye hizo roundabouts ni kuchomekeana tu.

Kwa kweli uendeshaji wa Dar kwa kiasi kikubwa ni hatarishi sana.
Zamani kwenye round about tulikuwa na bango likisema PLEASE GIVE WAY TO TRAFFIC ON YOUR RIGHT........hii mambo ya chuma chakavu imevibeba
 
Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
15,103
2,000
Karibuni bongo wenyewe tumezoea. 2008 nilienda Maryland nikakuta maajabu huko. Ukisimama tu pembezoni mwa barabara hizi za mtaani, magari yanasimama uvuke. Kwa kuwa nimetoka bongo sikuelewa nilidhani nimeshakosea kwa hiyo nikasogea nyuma mbali, nikaona binadamu wote wananishangaa. Nikajakuelewa somo Washington siku tatu baadaye kuwa kule kwa wenzetu punda wana maana

Hapa kwetu unakoswakoswa pale pale kwenye zebra crossing na dereva atakupa bonge la tusi ''mamaako ana mimba eeh?!'' (akimaanisha kwamba umeona hata ukifa ni sawa kwa hiyo unaleta mchezo mbele yake) na abiria waliomo ndani hawabaki nyuma, utasikia wanamsifia dereva ''hakujui mama yule''
 
pererge

JF-Expert Member
Nov 8, 2012
570
225
sasa ndugu hapa tutamfundisha nani sheria? Jambo la ajabu sana ni kwamba madereva wa magari ya serikali (STK na SU) ndio vinara wa uvunjaji wa sheria za barabara. mfano mmoja; pale wizara ya ardhi kuna kibao kinaonyesha kuwa usiingie na gari kuelekea kivukoni ila upitie barabara ya magogoni (pembeni ya ikulu) hawa jamaa huwa wanakatiza tu bila woga na kuleta usumbufu kwa watembea kwa miguu, na kibao chenyewe wameshakigonga hawahawa jamaa wa STK.
Tatizo kubwa la madereva wengi bongo ni kutojua sheria na sababu kubwa ni- leseni za kununua au kutokua na leseni kabisa, hata sisi tunaoandika humu wengi hatujui sheria za barabarani so kama unajua sheria yoyote unayoona itasaidia imwage tu hapahapa mkuu..
 
Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
12,459
2,000
kama ulikuwepo vile... Mimi nilichogundua niliporudi tz ni kuwa madereva wa Tanzania wana roho mbaya sana. Akikuona unakatisha bara bara yeye ndio anaongeza speed ya gari ili akuwahi . Wana roho ya kinyama sana.
SI, on the other hand nafikiri madereva wengi wanakua frustrated kwa muda wanaokaa kwenye foleni so akipata kaupenyo ka kunyagia wese, anakanyaga tu, hajali cha mwenda kwa miguu wala muendesha baiskeli.
Hapo kwenye bold ndipo penye shida, sababu zinafanana.
Hata kwa kuangalia sura za watu tu, watu wa Dar wako frustrated sana na maisha kuliko wa mikoani (mijini). Pita kituo cha daladala then uangalie sura za watu, utaamini ninachoongea. Hata driving ya Dar ni ya kipumbavu sana. KKN, ukitaka uvuke kwa usalama kwenye pundamilia kwa kutembea polepole, basi ufanye hivyo uwapo mikoani, sio Dar. Madereva majuha wa Dar watakuua. I' sorry to say this.
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
31,211
2,000
mojawapo ya round about zisizokuwa na adabu ni ile ya pake kwenye mnara wa askari kwa upande wa kutokea posta mpya na wakosa adabu ni madereva wa daladala wanaotokea posta mpya wao huingia tu hata kama kuna gari limeshaingia kwenye nzunguko, this shows how primitive most of daladala driver are!

yaani kabisa kabisa kabisa..... inabidi uwapishe tu wapishe
 
Top Bottom