Zebra Crossings in Dar- Whats the point??

Zebra Crossings in Dar- Whats the point??

kama ulikuwepo vile... Mimi nilichogundua niliporudi tz ni kuwa madereva wa Tanzania wana roho mbaya sana. Akikuona unakatisha bara bara yeye ndio anaongeza speed ya gari ili akuwahi . Wana roho ya kinyama sana.

Baada ya miaka mingi, nilirudi bongo juzi and I must say nilinusurika kugongwa na magari mara mbili wakati navuka barabara kwenye zebra crossing. Baada ya siku kadhaa na kulizoea jiji nikagundua kwamba hizo crossings zipo tu kama mapambo na hakuna dereva anayeziheshimu. Ukitaka kuvuka barabara ni lazima usubiri hadi kuwe hakuna magari ndo uvuke hata kama uko kwenye zebra! Hii ina maana kwamba hakukuwa na haja ya kupoteza hela kuweka hii michoro na you might as well vukia barabara popote tu ambapo unaona ni safe.

Ikumbukwe kwamba kwenye zebra crossing ni sehemu salama ambayo mwenda kwa miguu ana haki ya kuvuka barabara na dereva anapaswa kusimama kama kuna watu wanaosubiri kuvuka. Kama wanaosimamia sheria za barabarani wameshindwa kuwabana madereva waheshimu alama za barabarani na kuhatarisha maisha ya waendao kwa miguu, ni bora kabisa waondoe hizi alama barabarani manake zinaweza zikaku mislead ukajikuta umegongwa......

Kana-Ka-Nsungu


karibuni sana bongo ila hamjasema mlikuwa wapi kabla ya kurudi.

ila hiyo ndio bongo bwana nyingine zote cha mtoto, mambo kuwa ndivyo sivyo ni jambo la kawaida sana. na hapo ndio wasomi wanazidi kuongezeka.
 
Asilimia 80 ya madereva wa tanzania hawana leseni au kama wanazo wamezipata kwa deal, hawajazisotea kama ambavyo unasomea ukiwa nchi za wenzetu. Ndio maana ajali bongo haziishi coz watu wamelewa wanaendesha magari tena ya abiria au waendesha pipipiki wamejifunzia mafichoni so alama za barabarani kama zebra, stpo nk. kwao ni mabango tu hayana maana yoyote.
 
Jamani hii kitu ni point. Huhitaji kutoka nje ya nchi urudi kuja kugundua hili.
Mimi nilikulia Tanga na A-town pia. Nilipokuja Dar miaka ya 2002 hivi nikawa nikisimama kwenye zebra ili gari linipishe wala halisimami. Mwenyeji wangu wa hapa Dar nikamuuliza hivi huku Dar mbona magari yanapita speed kwenye zebra?! Yeye akasema ndio hivyo, kua makini tu.
Kweli kabisa aisee huu ni ukweli mtupu. Nadhani na siku hizi mikoani watakua wameshaiga Dar!
 
Mimi huwa nashindwa kuendesha gari Dar, ukiwa na hasira za karibu unaweza kwenda jela kwa ujinga wa madereva wa Dar. Tanzania hakuna madereva na kama wapo hawazidi zaidi ya 2% waliobakia wote sio madereva, wengi wao hawajui sheria za barabarani. Dereva wa Mabasi ya abiria anaovateki kwenye kona au mlima, ukiova teki gari basia ataongeza mwendo ili usimpite, ni hatari sana kuendesha gari Tanzania.
 
NN heshima yako mkubwa, long time man.

Kweli hiyo ya traffic light nayo niliishuhudia mara nyingi tu, yani kama ulivosema hata kama ngoma ni green kwako una proceed with caution. Lakini kwenye round about mimi nilivofunzwa na muingereza hapa (na najua nyumbani tunatumia system zao hawa jamaa) ni kuwa unampa priority mtu aliyeko kulia kwako and am sure hii ni kitu ambayo madereva wengi hawaijui. Tatizo jingine kubwa pia ni matumizi ya honi yasiyo lazima, yani ni kama vile watu wanaendeshea honi, mtu akiwa ana overtake honiii, foleni ikiwa haisogei kila mtu anapiga honi, mtu akimuona msichana mzuri anapita pembeni anatwanga honii tu, kero tupu

wakioana na kupita mtaani honi!
 
Ni upumbavu wa serikali yetu kuweka kila kitu Dar! Upuuzi
 
Asilimia 80 ya madereva wa tanzania hawana leseni au kama wanazo wamezipata kwa deal, hawajazisotea kama ambavyo unasomea ukiwa nchi za wenzetu. Ndio maana ajali bongo haziishi coz watu wamelewa wanaendesha magari tena ya abiria au waendesha pipipiki wamejifunzia mafichoni so alama za barabarani kama zebra, stpo nk. kwao ni mabango tu hayana maana yoyote.

Naomba niseme kwamba nilipata leseni yangu mwaka 2002 na nilikua sijawahi kugusa usukani wa gari!Nilikua sijui hata indicator iko wapi!! Kuna mtu niliskia anaziuza pale traffic makao makuu nikaona why not, back then i was still a student lakini nikaona ninunue tu, I know its wrong! Sasa you can imagine ni wangapi wana leseni kwa style hiyo.
 
Na kwanini watu hawataki kufunga mikanda? mikanda inaokoa maisha wakati wa ajali! Juzi nilipokua naenda mkoa, basi nililopanda lilikua na mikanda lakini I think i was the only passenger aliyefunga mkanda and i could tell watu walikua wananishangaa! Na mkanda wenyewe ulikua na vumbi kishenzi, you could tell ulikua haujatumika for a looong time.
 
nchi yoote ,wananchi wamechanganyikiwa na tumejipa jina sisi wenyewe bongoland, binafsi niko barabarani kitambo sasa, kuna mambo sifurahishwi nayo yanayotokea barabarani, nchi yetu foleni ni tatizo kubwa saana , dereva anapoendesha gari anawaza kukwepa foleni ambayo anahisi iko mbele, mtembea kwa miguu akipshwa kwenye zebra basi ndo anatembea taratibu kabisaaaa naye kuwa kero, mara nyingi hata watoto wangu au nikivusha watoto kwenye zebra, baada ya magari kusimama huwaimiza kukimbia . pikipiki wao wanahaki sawa gari ,lkn kuepuka ajali anapaswa awe na busara, mwendo wake mdogo anasababisha long train nyuma yake, mkikuta foleni mbele yy anapenyapenya kawaaacha, hivyo uendeshaji salama anapaswa achepuke pembeni magari yenye mwendo kasi yampite kuokoa foleni.
 
Back
Top Bottom