Kwa wale wenzangu wasomaji wa Tovuti , Forum na Blogu mbali mbali za kitanzania watakuwa wamesoma habari hii inayohusu Mmiliki wa Blogu moja maarufu kutiwa mikononi mwa vyombo ya kisheria , Kazi iliyokuwa inafanywa kwa Karibu sana kati ya Wataalamu Mbali mbali wa masuala ya Mawasiliano , Jeshi la Polisi pamoja na Vyombo vingine vya Nje .
Kukamatwa Mtu huyu imekuwa habari njema sana kwa wale wote ambao kwa namna moja au nyingine walidhilishwa au kuharibiwa majina na mambo mengine mengi sana katika jamii zao wengine kufikia hatua za kupoteza kazi , urafiki , ndoa kuvunjika na mambo mengine mengi ambayo hayaandikiki Hapa .
Katika maoni ambayo nimeyasoma mpaka sasa hivi wengi wanasema huyo mtu ni raia wa uingereza aliwahi kukana uraia wa Tanzania siku nyingi kidogo haijulikani ni kwa sababu gani hata hivyo kuna kesi nyingi za watu ambao wazazi au ndugu zao kuwa katika nafasi kubwa nchini kuukana uraia wa nchi hii na kuamua kuhamia nchi za watu baada ya kuona walichofanya sio sahihi na kinaadhari za baadaye kwahiyo huwa wanawahi pamoja mifano mingi iko lakini siku zao zinahesabika kwa sababu hakuna aliyetayari kuona uhuni huu ukiendelea , kuendelea kuharibu vizazi vyetu .
Wengine wanasema Nchini mwetu hamna sheria za Mitandao kwahiyo ni ngumu kumshitaki akipata mwanasheria mahiri basi ni rahisi yeye kuepuka yote aliyofunguliwa juu yake ukizingatia kwamba yeye ni mwana wa kiongozi mmoja wa zamani Nchini Mwetu .
Kama yeye hana makosa kama wengi wanavyofikiri kuna mambo hapa tunaweza kuyajadili , kumbuka ule mtandao yeye ni mali yake , unaposajili kitu mitandao kama ile unahusika na chochote kinachowekwa ndani ya mitandao hiyo kama hahusiki na chochote ndani yake basi kuna mengine tunaweza kuuliza
Mwanzo watu walilalamika kuhusu mtandao huu , wakatoa taarifa katika google ambao walisajili blogu yake ya zeutamu , alikiuka baadhi ya masharti ya google , kumbuka unaposajili blogu yako unawajibika kwa chochote kilichokuwa ndani ya blogu hiyo nakama unaweka picha za ngono mfano unatakiwa utoe ripoti kwa google waitambue .
Ilifungiwa baada ya taarifa hiyo kutolewa kwa muda wa siku kadhaa , iliporudishwa tena , Bwana Utamu akaendeleza kile kile alichokatazwa na google pamoja na wadau wengine , google wakaamua kufungia blogu hiyo moja kwa moja .
Akaamua kuhamia WordPress kwa ajili ya blogu yake hiyo , hapo nadhani ndio alikutana na mtu aliyemtengenezea version ya Sasa hivi ya Tovuti pamoja na kuweka baadhi ya vitu vingi vingi matangazo na kadhalika , mbaye yuko Houston huyu mtu anaonekana ni mshirika mkubwa wa Bwana Utamu kutokana na Rekodi zilizokwepo katika mitandao kadhaa iliyolink na Tovuti Husika .
Jambo lingine la kuangalia ni jinsi alivyoandika barua ya kwanza kabisa blogu ilivyofungiwa kujisifu jinsi wanavyochuma pesa kila siku kutokana na mapato ya matangazo na biashara zingine wanazozifanya kutokana na blogu hiyo kwa siku walisema ni zaidi ya dola 200 .
Njia nyingine iliyoweza kumtia matatani ni Yale matangazo ya Black Ads mara nyingi wale huwa wanalipa pesa kwa account za watu wenye majina binafsi kwahiyo kwa mpelelezi anaweza kufuatilia blackads na kujua mapato ya Tovuti husika yanalipwa kwa nani na namba zake za account , na kodi analipaje mtu huyo kwa jina la nani .
Kitu kingine ni kwamba kama yeye atakuwa hana makosa kutokana na hayo niliyoandika huko juu basi kosa lake kubwa ni kuruhusu wengine kuweka picha na taarifa zingine katika blogu yake bila kuwa na idhini au kuchambuliwa kama zina ukweli wowote au vidhibitisho vyovyote hata pale alipotakiwa kuziondoa taarifa hizo alikacha kufanya hivyo .
Kwa kuwa atakuwa na rekodi za wale wote waliokuwa wanatuma maoni na wale wote walioshiriki katika kutuma picha za wengine katika mtandao wake basi atatoa taarifa hizo kwa vyombo husika ili watu hao wote wakamatwe na kufikichwa katika vyombo vya sheria na sheria ichukue mkondo wake .
Hapa wako wanafunzi wengi wa chuo cha usimamizi fedha hawa walishiriki kwa kiasi kikubwa kumchafua mwenzao , rekodi zao lazima zitakwepo katika Blogu ya zeutamu , kwahiyo katika kazi hii kuna wengi sana watakaoshikiliwa na vyombo vya dola .
Haya ni maoni yangu tu