Ze Comedy Watinga Mahakamani

kama kweli TBC wanafikiri wana haki na Ze Comedy si waanze kuwatumia kama Ze Comedy halafu waone kama hawatafilisiwa hadi senti ya mwisho?

Duh!!! Mzee Mzima Mengi, kaamua kupapambana hata na vijana wanaojitafutia riziki!!? Kweli la uvumba halina ubani!!!!!
 
Wacheni Haki Itendeke!!!!!!1kama Eatv Wana Haki Waacheni Apate Haki Yao Tuache Ushabiki!!!1na Kama Ni Dhiki Za Ze Comedy Wacha Ziwatie Adabu!!!!awasomi Nyakati Badala Yake Wamekurupuka
Kazi Kweli Kweli!!!!!
 
Mzee Mwanakijiji,

Hilo wanalifahamu ndio maana hawajaanza!!!

Kasheshe upande mwingine, ni hawa watu wa TBC na EATV wangekaa pamoja na kuona how they could reach a compromise bila kuwaharibia hawa vijana. Binafsi naamini tatizo la Ze Comedy limeingia baada ya Manji kuingilia kati. Kama ingekuwa kati ya TBC na EATV ingekuwa ni rahisi sana kwa haja jamaa kukaa pamoja.

Hawa wa Ze Comedy kukubali kutumiwa na Manji wakati wametoka kwa Mengi nadhani ilikuwa ni lack of judgement au ushauri mzuri. Maana hata kama Mengi angetaka kuwaacha waende TBC, ni wazi hayuko tayari kumuacha Manji avune asichopanda.
 
Huyo ndiye MENGI tunayemfahamu baadhi yetu inapokuwa ni kuchagua kati ya PESA na WATANZANIA. Yeye aliwalipa nini RTD alipowachukua kina BROTHER MIKI, NYAISANGA, CHARLES HILLARY, MAJURA, ... Wakaenda wakaanzisha vipindi vinavyofanana na vya RTD na vikarushwa katika MUDA uleule. Lakini, WASANII wetu jifunzeni sana katika hili.
 
Huyo ndiye MENGI tunayemfahamu baadhi yetu inapokuwa ni kuchagua kati ya PESA na WATANZANIA. Yeye aliwalipa nini RTD alipowachukua kina BROTHER MIKI, NYAISANGA, CHARLES HILLARY, MAJURA, ... Wakaenda wakaanzisha vipindi vinavyofanana na vya RTD na vikarushwa katika MUDA uleule. Lakini, WASANII wetu jifunzeni sana katika hili.

samahani mkuu!
je naweza kupata baadhi ya vipindi vilivyokuwa RTD na baadae kufanana na hivyo uvisemavyo vya bwa mengi?
 
Karibu kila muda wa TAARIFA YA HABARI ya RTD, RO nao waliweka muda huohuo; kipindi cha MICHEZO RTD, RO wakaweka muda uleule wakakiita SPOTI LEO; kipindi cha ZILIPENDWA RTD Jumapili, RO nao wakaanzisha muda huohuo,...
 
Karibu kila muda wa TAARIFA YA HABARI ya RTD, RO nao waliweka muda huohuo; kipindi cha MICHEZO RTD, RO wakaweka muda uleule wakakiita SPOTI LEO; kipindi cha ZILIPENDWA RTD Jumapili, RO nao wakaanzisha muda huohuo,...
basi inabidi rtd wangedai hakimiliki ya muda...?
 
Kasheshe upande mwingine, ni hawa watu wa TBC na EATV wangekaa pamoja na kuona how they could reach a compromise bila kuwaharibia hawa vijana. Binafsi naamini tatizo la Ze Comedy limeingia baada ya Manji kuingilia kati. Kama ingekuwa kati ya TBC na EATV ingekuwa ni rahisi sana kwa haja jamaa kukaa pamoja.

Hawa wa Ze Comedy kukubali kutumiwa na Manji wakati wametoka kwa Mengi nadhani ilikuwa ni lack of judgement au ushauri mzuri. Maana hata kama Mengi angetaka kuwaacha waende TBC, ni wazi hayuko tayari kumuacha Manji avune asichopanda.
.....Jamani mnajua huenda hata hawa watoto wa ze comedy hilo bifu la Mengi na Manji walikuwa hawana ahabari nalo lakini ndio jumba bovu limewaangukia wao.. Mi nadhani wazo la kwenda mahakamani sio zuri sana ukizingatia kuwa hapa ni vita ya matajiri wao ndio wanaoathirika na huenda walikubali kufadhiliwa na Manji wakiamini atawabeba kulingana na ndoto zao.

Mi nashauri kuwa Ze comedy kama kuna mkataba wowote waliosainishana na Manji wauvunje haraka (kama vipengele vya mkataba vitaruhusu), then wakae na TBC na kusaini nao mkataba utakaowawajibisha wao kwa 100% kwa TBC, then TBC sasa wafanye mazungumzo na EATV kuhusu umiliki wa jina la kikundi na majina ya wasanii wenyewe ingawa mimi kwa ufahamu wangu hawa akina Mpoki na Joti tuliwafahamu siku nyingi walipokuwa wakiigiza na kikundi kimoja cha kuigiza kabla ya ze comedy haijaanza na waigizaji kama akina Bishanga Bashaija, MonaLisa, Rich Rich, JB, Baba na Mama Abdul, Waridi na wengine wengi. So kuwazuia kutumia na majina yao sio haki hata kidogo.

Hata hivyo huenda hiyo inaweza kupunguza ugumu wa kupata ufumbuzi wa tatizo lililopo vinginevyo hawa jamaa watakula vijisenti vyao walipata then waanze kusaga lami.....Pia nawashauri hawa jamaa wa ze comedy wakifanikiwa kulimaliza hili tatizo la sasa watafute shule wasome mambo ya sanaa na sheria ili kuwa na ufahamu wa masuala ya sheria kuepuka matatizo ya aina hii.
 
Mkuu Kasheshe
Hii Kesi Ndio Itawafumbua Macho Wasanii Na Kujua Umuhimu Wa Kazi Zao!!!shame Tbc 1---------------6
Wawe Makini Ukisema Shame Kwa Eatv Wakati Unaandika Mwishoni Wana Haki Hujaitendea Haki Sanaa Ya Tanzania Lazima Haki Iwe Mbele Kwanza Na Si Ushabiki Tu!!!!!!
Hureeee!!!!! Eatv
 
Mkuu Kipanga Hapa Si Eatv Na Tbc Bali Ni

Manji Na Mengi ..na Hilo Ni Kutokana Na Vijana Kuhakikishiwa Na Mzee Mani Kwamba Mahakamani Wanashinda Walawasiwe Na Wasiwasi Hata Ukiongea Na Akina Joti Wasivyona Ufahamu Wakilewa Wanaongea Yote Na Hivi Karibuni Jamaa Amewahidi Kuwanunulia Gali Lao Special Nakuwanunulia Nyumba Katikati Ya Jiji!!!!kuna Dalali Moja Kapewa Hiyo Ofa!!!!na Muonea Mani Huruma Asije Akanunua Nyumba Ya Million Miasita Pale Sinza Hawajui Vizuri Vijana Hao!!!!
 
Hii ishu inasikitisha sana kwa anayeujua ukweli wa mambo. Wengi watasema lakini ukweli haufichiki kabisa- Nlipata bahati ya kukutana na kikundi/wataarishaji wa mwanzo wa kikundi cha ze comedy few years back na hali zao za maisha hazikuwa hivi at all. Walikuwa wanyenyekevu na watiifu kwa wafanyakazi wa eatv na kufanya wapendwe sana kwa ucheshi wao. Eatv na ze comedy hawakujua hatima ya show na ingefika wapi- the idea was a stand up comedy show that combine different characters in tz. Show za slipway na mnazi moja zikaanza but couldnt be sustained given the logistics za maandalizi, at that time the show wa named "comedy" mara ikabadilishwa internally mara huku mara huku. Baada ya ma producers kupitia mikanda tofauti tofauti ya comedy za sehumu mbali mbali idea ya kustage show ikawa developed and produceds. Kiufupi Eatv made the comedy and gave them the fame, inategemea walikubaliana vipi na wafanye kazi vipi. If a show is produced by a tv station nikimaanisha- graphics, editing, film production, creative inputs and financial support- then its owned by that tv station given it copyrights the name. Kama msanii akitumia jina ambalo limetengenezwa au kuundwa wakati kipindi kipo chini ya tv station then his named is within the rights za tv station. Kwa mfano ujiite swedi as an aka kwenye show na jina lako ni ahmed- ukiamua kuacha huwezi kutumia swedi kwengine bila makubaliano ya mmiliki wa show. Kama msanii alikuja na jina lake tangu awali na akalitumia kwenye show then itategemea na makubaliano kati yake na mtaarishaji wa kipindi. Hili swala nani anamiliki jina lipo chini ya makubaliano kati ya eatv na ze comedy, watu wasifikie mahali kusema fulani yupo sawa au fulani ni mbaya bila ya kujua ukweli. Wahusika wanaweza wakawa na upeo mdogo wa kufikiri nakulijua wala zima la sheria au kuipuuza sheria nzima na kutumia fedha kuweka mambo sawa ila ukweli upo na wahusika wanaujua vizuri sana. Eatv ilikuepo kabla ya ze comedy na itaendelea kuwepe, crew ya ze comedy inajijengea mazingira yakutoweza kufanya kazi na mtu yoyote nchini kwenye nyanja ya mawasiliano ukifahamu historia yao na eatv. Kinachosikitisha ni ukosefu wa utu hata kama mkiwa hamkubaliani kibiashara basi hata utu muupoteze, ni sawa kweli? Niliwakuta mnaomba hela mnunuliwe maji ya viroba na jamaa pale eatv na leo mnamagari- kwani simaendeleo hayo? Sawa mkataba umekwisha basi tumieni diplomacia na unyenyekevu ule ule mliotumia kuanzia muwe sawa na Eatv wala sio ujanja. Hamna asiye wapenda ze comedy na hata mimi wameniburudisha sana, nasijapenda kwao kuacha show iwe eatv au TBC haijalishi. Tuwekane sawa mambo yaendelea kama kawa.
 
Ze Comedy ni kama vile bendera inavyofuata upepe. Wameangalia masirahi zaidi na kusahau utu na hasara zake. Wana tangazo lao mimi linanivutia sana linaseama hivi ' LAMI KWA LAMI MPK NDANI.
 
Ze Komedi wanatakiwa wapambane kwani hiyo ndio njia yao ya kuishi katika show bizness lazima tukubaliane kuwa watu hawaanzii juu. Hao akina Oprah Winfrey walikuwa maskini tu wa kawaida baadae wakaja gundua siri ya mafanikio yao si wao wenyewe bali kupitia watu. Ni nani aliyekuja kujua Michael Jackson angekuja kuutikisa ulimwengu kama sio Diana Ross. Jamaa (THE JACKSONS) walikuwa wanabangaiza katika Night clubs wapate kuishi lakini baadae Diana Ross kawadhamini wakaenda studio ndio wakatoka lazima tukubali changamoto jamani , jamaa walikuwa wanapendwa. Kama wameenda mahakamani basi waachwe wadai haki yao pale walipoona wamepunjwa.
 
Karibu kila muda wa TAARIFA YA HABARI ya RTD, RO nao waliweka muda huohuo; kipindi cha MICHEZO RTD, RO wakaweka muda uleule wakakiita SPOTI LEO; kipindi cha ZILIPENDWA RTD Jumapili, RO nao wakaanzisha muda huohuo,...

Hilo silo ulilolizungumzia pale juu!
 
NO NO NO.
wanunue wakati ni majina yao halisi toka zamani tunamjua Joti,Mpoki sasa wanunue vp?Na jina si hilo wamebadili wanaitwa ZEE COMED.

Wewe huyo Joti, au Masanja ulimjulia wapi? kama sio kupitia IPP-media?
Wakati mwingine muachage uongo, maana wote mnaotoa maoni yenu dhidi ya EATV ni wale ambao MNAWACHUKIA WACHAGA. Maana mnaona Mengi ni Mchaga.
 
Back
Top Bottom