Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Status
Not open for further replies.
watu kwa kupenda kupindisha mambo,
hamjaambiwa MSILE ila mmeambiwa MSILE HADHARANI...

Hata hivyo sheria ndio ishapita kifuatacho ni utekelezaji,
Tii sheria bila kushurutishwa.
 
Uhuru wa kuabudu uheshimiwe..kuvumilia imani na taratibu za mwingine ni jambo la msingi. Kumlazimisha asile hadharani ni udhaifu..
Hakuna mkristo anaefunga huku kwaresma
 
wanashangaa ya zanzibar wakati sasa hivi ofisi zote za serikali kama umevaa kimini, suruali ya kubana, jeans ya kuchanwa chanwa, mlegezo, kapelo, nguo inayoacha makwapa wazi, na mfanano wa hivyo.

Huruhusiwi kuingia ndani huoni kama hao nao wanaingilia uhuru wa mavazi?? mbona hamlalamiki.
 
Ndo ujue waislam mambo mengi wanafanya kwa kulazimishwa na sio hiari yao , sasa kama unajiamini umefunga utatamani vipi mtu akijichana mishikaki forodhani kama sio uroho tu?.

Mbona Mbeya na Mwanza kuna wakristo 99.9% na idadi ya watu ni kubwa kuliko hako ka Zanzibar lakini wakristo wakiwa kwaresma hawana ujinga wa kuwafuatilia hao waislam?

Waislam acheni kujifanya so special
 
The principle of how to nurture Upumbavu.

Wanabodi

hakuna sababu yoyote ya kuendelea kujadili Itifaki za kipumbavu zisizo na tija .
kama wameona sheria hiyo mpya ni bora sana .me nashaur tuafiki tu tena kwa moyo usio na kutu.
alafu ifike wakati watunge sheria mpya inatakayowataka wadai haki yao ya msingi ya kuishi mji mtukufu wao ili angalau na sisi huku kibiti tupumue.i.
 
Jamani walichokataza ni kula hadharani ,lakini ukiwa ndani ni ruksa,pale Maisara ukumbi wa CCM na ukumbi wa Magereza na hata hotel kubwa bado hutoa huduma za vyakula na hii sio kitu kipya kwa Zanzibar kipo tokea enzi za Karume tena siku hizi ni nafuu zaidi kuliko miaka ya nyuma,tutake au tusitake Zanzibar ni kama nchi ya Kiislamu ,90.9% ni waisalamu.
  • Kwa nini umkataze asili hadharani?
  • Kwa nini wanawachagulia (wanawapangia) Wakristo mahali pakufanya mambo yao
  • Kupangiana ndio kuondoleana uhuru
 
Jamani walichokataza ni kula hadharani ,lakini ukiwa ndani ni ruksa,pale Maisara ukumbi wa CCM na ukumbi wa Magereza na hata hotel kubwa bado hutoa huduma za vyakula na hii sio kitu kipya kwa Zanzibar kipo tokea enzi za Karume tena siku hizi ni nafuu zaidi kuliko miaka ya nyuma,tutake au tusitake Zanzibar ni kama nchi ya Kiislamu ,90.9% ni waisalamu.


Kama ndivyo basi aliyetoa tamko atoe kama msomi, mbona wewe umeeleweka vizuri kabisa iweje yeye kiongozi wa umma atoe taarifa kimtego, amini usiamini kuna kitu kinatokota chunguni
 
Hivi nchi hii kuna siku inapita bila hawa viongozi wa CCM kuanika ujinga wao hadharani kweli?
 
Hizi ndizo dalili za serikali kuwa na dini.
Ni bora ikatangazwa kimataifa ili wageni wasijisumbue kwenda zanzibar !!!
 
TANZANIA haina dini kwa taarfa yako, .......na zanzibar hawaish waislam pek yao, mambo gani ayo sasa, kula nile mmi wewe ikuume, nikikulingishia sawa lkn, nakul kwa manufaa angu af unamind, nyie vipi??
Kaisome vizuri katiba ya JMT je utakuwa masuala ya katiba na sharia ni ya Muungano na je suala la dini ni la Muungano hamna kwenye katiba ya znz sehemu inayosema serikali haina dini..na huko kula mchana siyo wakiristo pekee yako znz kuna Hindu kibao tangu Enzi na Enzi na kuna waislam kibao ambao hawafungi lakini wote hao hawaruhusiwi kula mchana ni sawa na ukienda India ukila nyama ya ng'ombe hadharani. Kwa hivyo unaona umeenda kwenye ukiristo moja kwa moja
 
Utaratibu wa Kizanzibar lazima uheshimiwe

Mbali ya Sheria Na Taratibu utamaduni lazima uheshimiwe
  • Pohamba usijitoe ufahamu, Ramadhan na mambo yake huo ni utamaduni wa Wazanzibari Waislamu
  • Wazanzibari Wakristo nao wanautamaduni wao ambao umefungamana na ukristo
  • Isitoshe mbona wao Wazanzibari Wakristo hawalazimishi Waislamu wafuate ya kwao?
 
Lakini ni suala ambalo lipo wazi kabisa hata waziri mkuu mstaafu Pinda Kayanza aliwahi kulitolea ufafanuzi, zaidi ya 90% ya wakazi wote ni waislamu..so hapa tunatekeleza tu 'wengi wape'...sidhani kama ni udini!
Wengi wape kwani kufunga ni compulsory kiasi serikali iweke mkazo?? Je toka serikali ina dini au zanzibar sio Tanzania tena maana katiba inasema serikali haina dini ila wananchi wake ndio wana dini..... toka lini ssa serikali idhibiti dini za watu!!
 
Hizi ni Imani habaa....!. Mwenye Imani thabiti hawezi kutamani chakula hata km akiwaandalia wengine
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom