Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Status
Not open for further replies.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imetoa onyo kwa wananchi watakaokula hadharani katika kipindi cha mchana wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma, Khamis Juma Maalim wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua serikali inatoa tahadhari gani kwa watu watakaobainika kula mchana wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kuheshimu kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa makundi yote ikiwemo wa dini tofauti. Alifahamisha kwamba utamaduni huo upo hata kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 wa dini tofauti kuheshimu dini za watu wengine.

Alisema kazi ya kutoa elimu kuhusu ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani imeanza kutolewa na Ofisi ya mufti ambayo ndiyo yenye jukumu la kushughulikia masuala ya mambo ya dini ya Kiislamu.

Alisema kazi kama hiyo imeanza kutolewa na maimamu wakuu wa misikiti mbalimbali Unguja na Pemba ikiwemo katika sala za Ijumaa ambazo hukusanya idadi kubwa ya Waislamu kwa wakati mmoja.

Alikiri kuwepo vijana wengi wanaoacha kufunga katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kula hovyo pamoja na kuvuta sigara. Maalim alisema zipo taarifa kwamba hoteli nyingi hufanya kazi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wateja wake wakubwa ni vijana wa Kiislamu. Waislamu nchini wanatazamiwa kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo ambapo ibada ya funga ni moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu

Chanzo: Habari Leo
=====================================
Nataka kujua kipindi kwa kwaresma mbona hawakutoa tamko hili.

Kwaio wakristo wawe wanajificha wakati wa chakula cha mchana.

Hapana naona kuna harufu ya udini kuanza Zanzibar.
mlishawahi kulalamika juu ya watu kula mchana!
pili, asilimia ngapi huwa mnafunga! huenda hamjaitilia mkazo halafu ikawa na maamuzi tu ya mtu!
 
90% watanganyika ni wakristo ila ua hatuwapangii hawa ndugu zetu kwakuwaheshimu. 90% zanzibar waislam.. Ila wanazarau zile 10%ambazo ua tunaziheshimu sisi.. Basi itabid tuwaletee waislam wao na wao watuletee wakristo wetu... Iii kitu mwalimu hakuitizama vizur
90% hiyo sio tanganyika labda Mbeya pekee! kumbuka coastal region zote muslim ndio wengi!
 
Hivi hawa watu wanafuata katiba na sheria za nchi au ni out of emotions wanatoa matamko ya kipuuzi.
 
zanzibar ni nchi, na inahaki ya kuweka sheria zake. Kwanza hii sio ya leo wala jana, ni toka enzi ya ukoloni.
 
Mantiki ya kawaida inakataa kwamba mtu mzima hata awe kichaa hawezi kushawishika kufanya jambo la kuiga.Mtizame kichaa aliye uchi.Kichaa hawezi kuchomoka kwenda kuvaa nguo kwa sababu amemuona mtu mwingine amevaa nguo tena gubigubi.Na vile vile mtu mwenye akili timamu hawezi kumuona kichaa barabarani akiwa uchi na yeye kunogewa" na kuanza kuvua nguo zake.Hii ndio kusema muislamu mtu mzima mwenye complete senses hawezi kutamani au kutoka udenda na kufungulia funga yake kisa kamuona mtu jirani yake anakula.Kila mara tunasikia na kuona watu wanaiba mbona na sisi hatutoki kwenda kuiba? Ni Mara ngapi tunapita mitaa ambayo wasichana "wanajiuza" miili yao tena wengine sehemu kubwa wakiwa uchi mbona huwa hatukatishi safari zetu na kwenda "kuwanunua" au nasi kwenda kujipanga ili "tununuliwe"? Ikiwa unayo imani ambayo nafsi inapelekeshwa na senses kwa kiasi kikubwa basi hiyo imani inahojika.Religion is not a success equation rather it is a liberation equation.Imani kazi yake kuleta ukombozi au uongofu Wa nafsi.Kuwataka watu wengine kula kwa "timing" ni kufanya Zanzibar ipunguze kiasi chake cha makusanyo kwa muda wote wa mfungo.Kwamba watu wasiohusika na mfungo huo wafanye shughuli zao kwa mang'amung'amu na hivi kushindwa kukidhi mahitaji yao.Kwa hiyo mkuu huu ndio ukweli unaousema hapa.

Mkuu umefahamu vibaya hili suala la marufuku kula mchana katika mwezi mtukufu wa Ramadhan halikuja kwamba wengine wakila wengine watatamani hiyo ni theory yako iliyokushawishi kichwani kwako., Elewa kwamba Zanzibar ukitoa figisufigisu za Muungano Zanzibar ni nchi ya Kiislamu 99%. Lengo hapa ni kuheshimu mwezi mtukufu wa Ramadhan mwezi ambao haukuchaguliwa kwa matakwa ya binadamu ni Mwezi ambao Allah mwenyewe ametutaka kutekeleza Ibada ya funga pamoja na Ibada mbali mbali zilizomo ndani ya Mwezi Mtukufu ikiwemo na kuomba msamaha na toba kwa Mola wetu aliyeumba Mbingu, ardhi na kila kilichomo ndani yake.

Ambaye atakuwa na imani tofauti hajazuiliwa kula lakin imekatazwa hadharani sababu ni ile ile tu kuheshimu Mwezi mtukufu wa Ramadhan. unaweza kujifungia ndani na ukala chakula chako., Pale zamani wakati wa Mtume wetu Muhammad Rehema na Amani ziwe juu yake walikuwepo wachamungu wakubwa sana ambao walikuwa na watumwa wenye imani tofauti ambao wanaishi nao ndani walikuwa wakiwapa chakula kama kawaida na kula lakin haikuwa hadharan., mpaka pale watumwa wale wengine waliingia katika uislamu moja kwa moja. kwa msingi huu hapa sio kutamanishana chakula, ni kwamba huu mwezi ni mwezi mwengine ambao Allah ameuchagua kuwa ni mwezi Mtukufu. Vipi utakula mchana kweupe ramadhani?

Unajuwa wakiristo wanapinga sana hili kwasababu wanataka uhuru wa kula mchana kweupe Ramadhan lakini pia mpaka leo wanashindwa kuleta hoja za kuipinga Mwezi mtukufu wa Ramadhani. La msingi hapa kama utaleta hoja watu wale mchana Ramadhan basi ni vyema ukaleta na hoja madhubuti kwanza kutokubali Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Allah atuongeze zaidi na zaidi Amin.
 
Mantiki ya kawaida inakataa kwamba mtu mzima hata awe kichaa hawezi kushawishika kufanya jambo la kuiga.Mtizame kichaa aliye uchi.Kichaa hawezi kuchomoka kwenda kuvaa nguo kwa sababu amemuona mtu mwingine amevaa nguo tena gubigubi.Na vile vile mtu mwenye akili timamu hawezi kumuona kichaa barabarani akiwa uchi na yeye kunogewa" na kuanza kuvua nguo zake.Hii ndio kusema muislamu mtu mzima mwenye complete senses hawezi kutamani au kutoka udenda na kufungulia funga yake kisa kamuona mtu jirani yake anakula.Kila mara tunasikia na kuona watu wanaiba mbona na sisi hatutoki kwenda kuiba? Ni Mara ngapi tunapita mitaa ambayo wasichana "wanajiuza" miili yao tena wengine sehemu kubwa wakiwa uchi mbona huwa hatukatishi safari zetu na kwenda "kuwanunua" au nasi kwenda kujipanga ili "tununuliwe"? Ikiwa unayo imani ambayo nafsi inapelekeshwa na senses kwa kiasi kikubwa basi hiyo imani inahojika.Religion is not a success equation rather it is a liberation equation.Imani kazi yake kuleta ukombozi au uongofu Wa nafsi.Kuwataka watu wengine kula kwa "timing" ni kufanya Zanzibar ipunguze kiasi chake cha makusanyo kwa muda wote wa mfungo.Kwamba watu wasiohusika na mfungo huo wafanye shughuli zao kwa mang'amung'amu na hivi kushindwa kukidhi mahitaji yao.Kwa hiyo mkuu huu ndio ukweli unaousema hapa.

Mkuu umefahamu vibaya hili suala la marufuku kula mchana katika mwezi mtukufu wa Ramadhan halikuja kwamba wengine wakila wengine watatamani hiyo ni theory yako iliyokushawishi kichwani kwako., Elewa kwamba Zanzibar ukitoa figisufigisu za Muungano Zanzibar ni nchi ya Kiislamu 99%. Lengo hapa ni kuheshimu mwezi mtukufu wa Ramadhan mwezi ambao haukuchaguliwa kwa matakwa ya binadamu ni Mwezi ambao Allah mwenyewe ametutaka kutekeleza Ibada ya funga pamoja na Ibada mbali mbali zilizomo ndani ya Mwezi Mtukufu ikiwemo na kuomba maghufira na toba kwa Mola wetu aliyeumba Mbingu, ardhi na kila kilichomo ndani yake.

Ambaye atakuwa na imani tofauti hajazuiliwa kula lakin imekatazwa hadharani sababu ni ile ile tu kuheshimu Mwezi mtukufu wa Ramadhan. unaweza kujifungia ndani na ukala chakula chako., Pale zamani wakati wa Mtume wetu Muhammad Rehema na Amani ziwe juu yake walikuwepo wachamungu wakubwa sana ambao walikuwa na watumwa wenye imani tofauti ambao wanaishi nao ndani walikuwa wakiwapa chakula kama kawaida na kula lakin haikuwa hadharan., mpaka pale watumwa wale wengine waliingia katika uislamu moja kwa moja. kwa msingi huu hapa sio kutamanishana chakula, ni kwamba huu mwezi ni mwezi mwengine ambao Allah ameuchagua kuwa ni mwezi Mtukufu. Vipi utakula mchana kweupe ramadhani?

Unajuwa wakiristo wanapinga sana hili kwasababu wanataka uhuru wa kula mchana kweupe Ramadhan lakini pia mpaka leo wanashindwa kuleta hoja za kuipinga Mwezi mtukufu wa Ramadhani. La msingi hapa kama utaleta hoja watu wale mchana Ramadhan basi ni vyema ukaleta na hoja madhubuti kwanza kutokubali Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Allah atuongeze zaidi na zaidi Amin.
 
Mkuu umefahamu vibaya hili suala la marufuku kula mchana katika mwezi mtukufu wa Ramadhan halikuja kwamba wengine wakila wengine watatamani hiyo ni theory yako iliyokushawishi kichwani kwako., Elewa kwamba Zanzibar ukitoa figisufigisu za Muungano Zanzibar ni nchi ya Kiislamu 99%. Lengo hapa ni kuheshimu mwezi mtukufu wa Ramadhan mwezi ambao haukuchaguliwa kwa matakwa ya binadamu ni Mwezi ambao Allah mwenyewe ametutaka kutekeleza Ibada ya funga pamoja na Ibada mbali mbali zilizomo ndani ya Mwezi Mtukufu ikiwemo na kuomba maghu**** na toba kwa Mola wetu aliyeumba Mbingu, ardhi na kila kilichomo ndani yake.

Ambaye atakuwa na imani tofauti hajazuiliwa kula lakin imekatazwa hadharani sababu ni ile ile tu kuheshimu Mwezi mtukufu wa Ramadhan. unaweza kujifungia ndani na ukala chakula chako., Pale zamani wakati wa Mtume wetu Muhammad Rehema na Amani ziwe juu yake walikuwepo wachamungu wakubwa sana ambao walikuwa na watumwa wenye imani tofauti ambao wanaishi nao ndani walikuwa wakiwapa chakula kama kawaida na kula lakin haikuwa hadharan., mpaka pale watumwa wale wengine waliingia katika uislamu moja kwa moja. kwa msingi huu hapa sio kutamanishana chakula, ni kwamba huu mwezi ni mwezi mwengine ambao Allah ameuchagua kuwa ni mwezi Mtukufu. Vipi utakula mchana kweupe ramadhani?

Unajuwa wakiristo wanapinga sana hili kwasababu wanataka uhuru wa kula mchana kweupe Ramadhan lakini pia mpaka leo wanashindwa kuleta hoja za kuipinga Mwezi mtukufu wa Ramadhani. La msingi hapa kama utaleta hoja watu wale mchana Ramadhan basi ni vyema ukaleta na hoja madhubuti kwanza kutokubali Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Allah atuongeze zaidi na zaidi Amin.

Asante kwa kuchangia.Sasa hebu tueleze mantiki ya kidini ya kukataza waislamu kutokula hadharani mchana wakati Wa Ramadhani? Mtume alipokataza watu wasijilie hadharani alitaka kufundisha nini hasa? Kuna picha humu zinawaonyesha waislamu wakifuturu nje jioni.Je, Mtume alitaka kufundisha nini kuruhusu watu wale hadharani jioni?
 
Wagalatia ndio maana mnaambiwa watu walimuua mwana wa mungu wa pekee ili nyie mkombolewe, na mnaitikia aamin !
 
Mfano wako ni sahihi ila je, Kwani Zanzibar ni nchi ya kiislamu mpaka nifuate masharti?

Mbona mikoa ya Lindi na Mtwara, waislam ni Wengi lakini hakuna masharti hayo?
Nenda mafia uwone wanasharti mpaka kuishi pale chief
 
Huku ni kulazimishana kutii imani, kufunga au kutokufunga itoke moyoni mwamhusika sio kulazimishwa, kufunga kwasababu ya kulazimishwa hakumpi mtu thawabu bali mateso na dhambi mara mbili.
Tunawaona wengi wanakwenda kuswali kwasababu ya kuohofia/kuogopa macho ya watu, hapa hakuna swala wala thawabu.
Ukitaka dini yako iheshimiwe basi nawe uiheshimu dini ya mwenzio kwanza, sio kumtisha/kumuogopesha asile hadharani kwakuwa wewe umefunga, huku ni kuingilia imani ya mtu mwingine kwa nguvu maana yeye alipofanya kwaresma yake hakukutangazia nini chakufanya ila alikuacha ukatenda hata yale ambayo hayakumpendeza, hichi ndicho kipimo cha imani ya mtu.
Ikiwa umefunga ukimuona mtu anakula unatamani au unakasirika ni dhahiri hukufunga kwa imani ila shinikizo tu, bora ukala maana huna unachokifanya.
 
Wagalatia ndio maana mnaambiwa watu walimuua mwana wa mungu wa pekee ili nyie mkombolewe, na mnaitikia aamin !

Mkuu mbona umeacha kujibu hoja ya msingi? Tunajadili hapa maudhui ya kula hadharani.Jikite hapo.Tukimaliza ndio tuanze hili la Yesu.
 
Lakini ni suala ambalo lipo wazi kabisa hata waziri mkuu mstaafu Pinda Kayanza aliwahi kulitolea ufafanuzi, zaidi ya 90% ya wakazi wote ni waislamu..so hapa tunatekeleza tu 'wengi wape'...sidhani kama ni udini!
Muhimu sana kuiheshimu 10% iliyobaki kutokuilazimisha kufuata ya 90% maana huu sio uchaguzi ila imani za watu.
 
zanzibar ni nchi, na inahaki ya kuweka sheria zake. Kwanza hii sio ya leo wala jana, ni toka enzi ya ukoloni.
Hawajui kuwa Zanzibar enzi za mkoloni pombe unakata leseni ya kukuruhusu kunywa
 
Znz ikifika kipindi cha ramadhani, ukienda dukani kununua vyakula vya fast food hawakuuziiw(mfano soda, mikate, maji)...
Na hata ukishikwa na kiu, ukasema uende kuomba maji kwenye nyumba hawakupi.
Inshort wanabana mianya yote ya watu kula mchana, unakuta vyakula vinauzwa hotels za kitalii tu,
Na hata kama ni mkristo, wakikuona unakula njiani wanaweza kukufanyia vurugu,
Sasa hii ni imani au kulazimishana imani mkuu? Kama wewe unafanya yako kwa kuitengeneza pepo yako inakuuma nini mimi kutoitaka pepo wakati hatutohukumiwa pamoja?
 
Mkuu mbona umeacha kujibu hoja ya msingi? Tunajadili hapa maudhui ya kula hadharani.Jikite hapo.Tukimaliza ndio tuanze hili la Yesu.
unazungumzia kula hadharani jioni wakati wa kufungua, wakati zuio ni la mchana wakati watu wamefunga !
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom