Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Status
Not open for further replies.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imetoa onyo kwa wananchi watakaokula hadharani katika kipindi cha mchana wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma, Khamis Juma Maalim wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua serikali inatoa tahadhari gani kwa watu watakaobainika kula mchana wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kuheshimu kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa makundi yote ikiwemo wa dini tofauti. Alifahamisha kwamba utamaduni huo upo hata kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 wa dini tofauti kuheshimu dini za watu wengine.

Alisema kazi ya kutoa elimu kuhusu ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani imeanza kutolewa na Ofisi ya mufti ambayo ndiyo yenye jukumu la kushughulikia masuala ya mambo ya dini ya Kiislamu.

Alisema kazi kama hiyo imeanza kutolewa na maimamu wakuu wa misikiti mbalimbali Unguja na Pemba ikiwemo katika sala za Ijumaa ambazo hukusanya idadi kubwa ya Waislamu kwa wakati mmoja.

Alikiri kuwepo vijana wengi wanaoacha kufunga katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kula hovyo pamoja na kuvuta sigara. Maalim alisema zipo taarifa kwamba hoteli nyingi hufanya kazi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wateja wake wakubwa ni vijana wa Kiislamu. Waislamu nchini wanatazamiwa kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo ambapo ibada ya funga ni moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu

Chanzo: Habari Leo
=====================================
Nataka kujua kipindi kwa kwaresma mbona hawakutoa tamko hili.

Kwaio wakristo wawe wanajificha wakati wa chakula cha mchana.

Hapana naona kuna harufu ya udini kuanza Zanzibar.
Huu ni ubaguzi wa wazi wazi
Over!
 
Hivi kiti moto nikila adharani Zanzibar nikiwa mtalii wanaweza kunifunga kwa sheria ipi ??
Watalii wanakamua kwa kwenda mbele.hotelini lakini.wanaheshimu utamaduni wa wazanzibari.
 
Naona SMZ wamesema clear statement kama isemeavyo ATAKAE KULA HADHARANI, kwa maana hukatazwi kula ila usile hadhania kula nyumbani kwako au tafuta pahala salama kisha kula, dini inatambumbua kwa waisilamu wasiweza kufunga ambao ni waginjwa au wasafiri, pia ambao wasio waisilamu, kwa hiyo hakazwi kula mtu yeyote ramadhani ila kula pahala salama,
 
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imetoa onyo kwa wananchi watakaokula hadharani katika kipindi cha mchana wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma, Khamis Juma Maalim wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua serikali inatoa tahadhari gani kwa watu watakaobainika kula mchana wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kuheshimu kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa makundi yote ikiwemo wa dini tofauti. Alifahamisha kwamba utamaduni huo upo hata kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 wa dini tofauti kuheshimu dini za watu wengine.

Alisema kazi ya kutoa elimu kuhusu ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani imeanza kutolewa na Ofisi ya mufti ambayo ndiyo yenye jukumu la kushughulikia masuala ya mambo ya dini ya Kiislamu.

Alisema kazi kama hiyo imeanza kutolewa na maimamu wakuu wa misikiti mbalimbali Unguja na Pemba ikiwemo katika sala za Ijumaa ambazo hukusanya idadi kubwa ya Waislamu kwa wakati mmoja.

Alikiri kuwepo vijana wengi wanaoacha kufunga katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kula hovyo pamoja na kuvuta sigara. Maalim alisema zipo taarifa kwamba hoteli nyingi hufanya kazi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wateja wake wakubwa ni vijana wa Kiislamu. Waislamu nchini wanatazamiwa kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo ambapo ibada ya funga ni moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu

Chanzo: Habari Leo
=====================================
Nataka kujua kipindi kwa kwaresma mbona hawakutoa tamko hili.

Kwaio wakristo wawe wanajificha wakati wa chakula cha mchana.

Hapana naona kuna harufu ya udini kuanza Zanzibar.
Inaonekana umeleta habari usiyoielewa, ushaambiwa huo ni utamaduni wa toka kabla ya mapinduzi, unasemaje tena kwamba tumeanza harufu ya udini?
 
Tofauti ya Uislamu na Ukristo ndio iko hapo; Kwa Mkristo kwanza akifunga inatakiwa kua SIRI yake yeye na Mungu wake na pia hatakiwi kuanza kuwalemea wengine kwasababu ya FUNGA yake kwa maana ya mwajiri au hata watu wa nyumbani kwake. Tena anatakiwa kuendelea ku provide everything kwa watu wa nyumbani mwake kama kawaida Refer to Isaya sura ya 59 na pia afungapo hakiwi kuonesha mnyonge ili ahurumiwe, kwa Lugha ya Yesu hapo alitolea mfano wa Mafarisayo kwamba wafungapo hutaka watu wajue kua wamefunga but kwa mcha Mungu wa kweli Yesu alitaka iwe siri kati ya mfungaji na Mungu wake.
Kuzuia wengine wasile eti kwa kigezo cha kuwatamanisha sidhani kama kina maandiko ya Kimungu (anyway siijui sana Kurani) zaidi ya mafundisho na hofu tu za wanadamu.
 
Znz ikifika kipindi cha ramadhani, ukienda dukani kununua vyakula vya fast food hawakuuziiw(mfano soda, mikate, maji)...
Na hata ukishikwa na kiu, ukasema uende kuomba maji kwenye nyumba hawakupi.
Inshort wanabana mianya yote ya watu kula mchana, unakuta vyakula vinauzwa hotels za kitalii tu,
Na hata kama ni mkristo, wakikuona unakula njiani wanaweza kukufanyia vurugu,
Kufunga kwa kulazimisha watu ni unafiki ambao Mungu hautaki.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom